saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 602
- 1,407
Kwa mliofanikiwa kufuatilia tukio la jana Disemba 22, 2022 la kuanza kujaza maji Bwawa la JNHPP wamesema mradi utakamilika lini. bahati mbaya mimi umeme ulikuwa umekatika sikuweza kufuatilia kwenye TV.
Hadi kufikia jana Naibu Waziri wa Nishati alisema Bunge lililopita la Novemba kuwa mradi utakwisha Juni 2023 japo kwa mujibu wa Mkataba ilikuwa mradi ukamilike Juni 2022.
Kwa mliosikiliza tukio la jana wamesema mradi utakamilika lini na kuanza uzalishaji.
Rejea mkanganyiko uliotokea bungeni baina ya Spika, Dk. Tulia Ackoson, Naibu Waziri wa Nishati Byabato na Waziri Simbachawene ambao wote walishindwa kulieleza Bunge tarehe rasmi ya kukamilika kwa mradi.
Spika alimuagiza Waziri Mkuu atoe taarifa rasmi ya mradi huo bungeni au sehemu yoyote nje ya bunge kuwaeleza watanzania ukweli kuhusu kumalizika kwa mradi huo.
Swali la mwisho madai ya Serikali kwa Mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors ya Trilioni 1.5 za kuchelewesha mradi nayo wamesemaje kwenye tukio la jana.
Mungu Ibariki Tanzania.