Mliofanya ufisadi wa Rada bilioni 214 hamtopata amani kamwe!!! Mtaishi kwa hofu na majuto.

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Messages
500
Points
1,000

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined May 3, 2018
500 1,000
Hivi unajisikiaje kuendesha gari ya bei mbaya au kuishi kwenye jumba la kifahari ( Mansion) ulilojenga kwa wizi wa kodi ya mama muuza maandazi! au mama muuza nyanya na mboga mboga pale soko mjinga! Kinachoumiza zaidi ni kwamba baadhi ya waliohusika na wizi huu wa mapesa haya bado Wapo tena wengine wakiendelea na vyeo mbali mbali serikalini na huku wakilipwa mishahara minono kutokana na kodi zetu .

Mi nawambia roho za watanzania zinanung'unika juu ya pesa zao na mtalaaniwa pamoja na vizazi vyenu vyotee!!.Mkitaka mpone laana hiyo rudisheni fedha za Watanzania! Mnaozani pesa ndo kila kitu jiulizeni ni matajiri wangapi tumewapoteza hivi karibuni, huku wakiwa wameacha maradio,maTV house, na biashara nyingine kubwa?

Tunajua mmeweza kukwepa hukumu kwasababu ya mapesa yenu lakini kamwe hamtoweza kukwepa hukumu ya Mungu. Rudisheni hiyo fedha haraka mkatubu ili msamehewa na Mungu pamoja na WTZ. Pesa ya wizi ni laaana. Fanyeni maamuzi kabla Mungu hajachukua uhai aliowaazima kwa mda tu.

Mungu mbariki Rais wangu Magufuli,azidi kufanya mambo mema kwa ajili ya taifa hili zuri na teule TZ.
 

Wong Fei

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2016
Messages
3,935
Points
2,000

Wong Fei

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2016
3,935 2,000
NA WALE WALIOPITISHA SHERIA YA UBAGUZI YA VYETI FEKI LAKINI WENGINE WANAACHWA NAO WAPO KUNDI GANI? UNAMTUMBUA MWALIMU KWA VYETI FEKI LAKINI UNAMUACHA MWANAJESHI MWENYE VYETI FEKI. MHALIFU NI MHALIFU TU HAIJALISHI CHEO CHAKE.
VIPI KUHUSU AJIRA ZA WALIMU KUFUTWA 2015 NALO NI JAMBO JEMA?
KUNYAFA MIKUTANO CCM RUKSA ILA WAPINZANI WAKIFANYA MIKUTANO NI KOSA.
WASALIMIE WATU WASIOJULIKANA
 

Forum statistics

Threads 1,382,624
Members 526,405
Posts 33,832,188
Top