FAJES
JF-Expert Member
- Oct 29, 2017
- 714
- 628
Mungu si Athumani, maana amekuwa akishusha thawabu zake kwa muda wa takribani miaka mitano sasa tangu nilipoanza kupataa namna ya kujiingizia kipato changu na kumudu gharama za kuishi. Kwakweli niwe muwazi kuwa maisha siyo mteremko sana na wala sipati pesa nyingi sana lakini pesa nazopata zinawezesha kugharamia mahitaji yote ya muhimu na kubakiza vichenji vya hapa na pale. Sasa changamoto ni kuwa, kwa muda wa miaka mitano sasa nikijifanyia tathmini sijafanikiwa kumiliki kitu chochote kama asset, siyo nyumba wala ardhi. Yaani chenji zote nazopata zinaishia kusaidia ndugu na jamaa.
Ukweli ni kuwa, nimetokea familia maskini na watu wengi kwenye circle yangu bado wana maisha magumu sana. Sasa kwakweli nakuwa na moyo wa huruma sana pale mtu anapokuja na kulia shida zake halafu nimnyime pesa kwa kisingizio kuwa nafanya savings. Huwa navuta kumbukumbu wakati ule nilipokuwa sina kitu na maisha yalivyokuwa magumu kisha napata huruma sana. Kwahiyo mtu akija, awe ndugu ama rafiki endapo atasema ana shida flani huwa naichukuwa kama shida yangu na kumsaidia. Huwa nashindwa kabisa kuwanyima hawa jamaa zangu. Kuna wakati nilisema labda nijifanye bahili na niwe na moyo mgumu lakini badae nikashindwa kabisa maana moyo ulikuwa unaniuma sana na nikawa kama nakuwa guilty kwakushindwa kumsaidia jamaa yangu. Huwa najiuliza hivi huyu ndugu akifa na ameomba pesa labda ya matibabu au chakula si nitaenda masibani na kumzika, kisha nitasema ni ndugu yangu wa karibu na nilimpenda sana? Sasa iweje nishindwe kumsaidia sasa akiwa hai?.
Hii tabia imenifanya nishindwe kufanya savings kabisa ili kujiendeleza kiuchumi na kutanuka zaidi. Yaani unakuta kwa mwezi nina requests za ndugu na jamaa zipo pending zakutosha. Unakuta nyingine nazi-hold hata miezi 4 kabisa kutokana na kuelemewa. Ikifika mwisho wa mwezi naanza ku-clear moja baada ya nyingine kama mtu anavyolipa mishahara watu wake. Nikipiga hesa kiasi nachosaidia watu kwa mwaka mpaka huwa najishangaa nimewezaje kutoa kiasi chote hicho. Lakini pamoja na hayo, kwakweli Mungu hajawahi kunipungukia kabisa. Sijawahi kukosa kabisa wala kupungukiwa. Ila ndio hivyo sina savings za kusema wala sima mali nayomiliki. Sasa swali langu, wale mliofanikiwa kutoboa kwa kuwa 'mabahili' mnawezaje kumudu hisia zenu pale jamaa zenu wanapoomba msaada kwenu na kuamua kuwakazia?