Mlio omba mkopo heslb angalieni hapa mjifunze mapemaaa

nimejifunza umenikumbusha enzi za 1st year kweli buum noumaaa unaweza ukawaza kununua meli asee
 
Hope sa hz hata ka unapata bumu tena,utakuwa una nidhamu nalo!
 
Expand hii ukijazia na vituko vingine ulivyofanya au kukutana navyo hapo UD kuhusu wanafuzi na matukio mengine kisha andika kitabu. kinaweza kusomwa sana
 
hata mimi siamin kama laki 5 inaweza kusababisha mtu asitulize akili

kwa neno moja SI KWELI
 
Halafu huwa nashaangaa wanachuo kugoma wakati bumu wanatumia kwa 'luxuries' halafu wanasema pesa haitoshi!!!
 
MADHARA YA KUPAPATIKIA BUMU HAYA HAPA HADHARANI
Naitwa XXX mimi ni mwanafunzi niliyemaliza Bwiru secondary. Ninaishi njombe, nilitamani sana kusoma chuo kikuu chochote hapa Tanzania na wakati wote huwa namwomba Mungu anisaidie nipate chuo ambacho ningeweza kupata mkopo kwakuwa familia yangu haikuwa na uwezo. Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumatano ndipo matokeo ya kidato cha sita yalipo tangazwa, nilikimbilia internet café nikiwa na shauku kubwa yakujua matokeo yangu. Nilifurahi sana tena sana yaani siwezi kuelezea kiwango cha furaha nilichokuwa nacho siku hiyo nilipoangalia jina langu na kuona nimepata division one ya point 10. Furaha ilitawala zaidi nilipofika nyumbani na kuwapa taarifa ya matokeo yangu………………SIKU ZILISONGA BAADAYE NILIOMBA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA NIKACHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO HIKO BAADA YA HAPO NILIJUTA………endelea
Nakumbuka siku natoka nyumbani baada ya nasaha za wazazi na marafiki baba alinipatia shilingi elfu hamsini ikiwa ni pamoja na nauli yangu. Nilipofika jijini Dar es salaam nilifikia kwa rafiki yangu aliyekuwa akisoma mwaka wa pili DIT(Dar es salaam Institute of Technology), kwa kweli ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika katika hili jiji, baada ya siku tatu nilienda kuripoti chuo na nikapatiwa fomu za usajili…..SASA NAANZA KULIJUA JIJI…..nilipozunguka kwenye jengo moja hapa chuoni nilikuta jina langu limebandikwa ubao wa matangazo nilikuwa nimepangiwa kuishi hostel za mabibo, nilienda mpaka kwenye hostel nilikopangiwa………..NAENDELEA KUSONGA MBELE….Sasa mimi ni mwanachuo nahii naithibitisha baada ya kupata kitambulisho cha chuo, baada kama siku mbili hivi ndipo nilipopata taarifa ya kwamba tunahitajika tukasaini majina yetu ilitupewe mkopo(bumu), nilifanya hivyo na kwa mara ya kwanza nilipewa shilingi 500,000/= cash mkononi, aisee akili ziliniruka ghafla nikawa kama nimechanganyikiwa, nilimkumbuka mama nyumbani kisha baba baadae marafiki, aisee nilijiona nami ni kati ya wale matajiri wanao julikana hapa Tanzania…Kitu cha kwanza nilichokumbuka ni kumtumia mama shilingi laki moja kisha baba nikamtumia shilingi elfu hamsini baada ya hapo nikabakiwa na shilingi 350,000/= nikawa napiga hesabu niifanyie biashara gani hii hela iliniweze kupata zaidi……..Nilienda kwanza hostel kupumzisha akili baadaye wazo la kununua redio kubwa aina ya SUB HOOFER likanijia nilimwomba rafiki yangu anipeleke wanapouza subhoofer, nilipelekwa sehemu moja inaitwa Mlimani city nikanunua subhoofer shilingi laki moja na nusu, baada ya kurudi hostel nilikuwa nimebakiwa na kama shilingi laki moja na arobani elfu akili yangu bado haikuwa imetulia nilitamani ni stop kwanza chuo ili nimalizie hizi pesa, baada ya wiki kadhaa kupita tulitangaziwa test namba moja nakumbuka nilipata 2/10, hapa sasa nikastuka kidogo japo haikunitisha sana, kufikia mwezi wa kumi na moja mwishoni tukaambiwa tufungue akaunti ili mkopo wa pili uweze kuwekwa kwenye akaunti zetu, mama yangu uwiiii! hapa sasa ndio nikawa mwendawazimu……..ENDELEA…. Nakumbuka mkopo wa pili niliwekewa kwenye akaunti yangu shilingi laki tatu kama na arobaini hivi sikumbuki vizuri ila kusema kweli walinichanganya sana na hizi hela zao ikapelekea hata baadhi ya lecture siendi….Mitihani ya semester ya kwanza ilitangazwa na nakumbuka nilipata suplimentary tatu za core courses

Hapa sasa akili ikaanza kufanya kazi baada ya kuambiwa na wenzangu kwamba iwapo sitoweza kuzifaulu course hizo nitafukuzwa chuo na mbaya zaidi sitopewa tena mkopo. Nilianza kukesha kama bundi na huwezi amini semester ya pili nilifaulu vizuri sana ila niliandikiwa nimediscontinue due to min GPA point.. Aisee niliumia sana yaani sana nilipowauliza wenzangu nini kinachofuata waliniambia niende nikaongee na mwalimu wa kila somo nililofeli kama anaweza kunisaidia, nilifanya hivyo ila ilishindikana nikapewa ushauri kama nitakuwa na hela kidogo kama laki moja nimpe mwanafunzi mwenzangu ampelekee mwalimu wa somo ili aweze kunisaidia, niliuza subhoofer yangu shilingi elfu tisini na tano nikaongezea na hela yangu kisha nikampa mwanafunzi mwenzangu akampelekea mwalimu , mwalimu alikula hela yangu kisha akaniambia niwe mvumilivu atarekebisha kwenye profile ya matokeo yangu……ENDELEA…. Siku moja ikanibidi niende ofisini kwa mwalimu ambaye alipewa hela yangu baada ya kuona hakuna jipya kwenye profile yangu ndipo nilipokutana na maneno hayaaa: SIKILIZA KIJANA MIMI SIKUTAMBUI KWA KIPINDI HIKI, MATOKEO NIMESHATOA KAMA HUJARIDHIKA NENDA KA-APPEAL ALAFU WARUDIE KUSAHIHISHA MTIHANI WAKO: mwalimu aliongea kwa ukali huku akiniangalia usoni bila hata ya huruma… daaaaa! Nilichoka ile mbaya, sasa niliona dhahiri ya kwamba mimi sio tena mwanachuo baada ya majina bumu la tatu yalipotoka nilipoingiza kadi yangu ya ATM ilimezwa kwa sababu nilisahau password nilipoingia ndani niliambiwa akaunti yangu haina fedha ya kutosha kuweza kupewa salio, nikawaambia naombeni basi hata hiyo kadi yangu walinipa kadi yangu nikaondoka. MIMI MWENZENU SILIPENDI BUMU NI TOFAUTI NA WANAFUNZI WENGINE NAJUUUUTA KUPATA BUMU.
USHAURI
Jamani kama hujui matumizi ya hela ya mkopo unayopewa pliiiiizi nenda kwa dean of student omba ushauri. CHUO SINA TENA NILIRUDI ZANGU HOME NIKISUBIRI MWAKA MWINGINE NIFANYE APPLICATION UPYA.
***************ASANTENI KWA KUNISIKILIZA**********
..SIJUI KAMA KUNA KITU UMEJIFUNZA KUTOKA KWANGU KAMA BADO UTAJIFUNZA UKIPATA BUMU…

nani amekufundisha kutunga stori za kusadikika?
 
stori yako ni nzuri ila hapo kwenye red hapo!!! ulikua unasemea ya fom 4 au??? ILA TUMEJIFUNZA...THNX ALOT!!!
 
Nimekuelewa mheshimiwa,ila umenichanganya kwa division uliyopata ni one au two,au ulipigwa penati ya GS, pia ilitakiwa ujiulize kwanza ni kiasi gani unaifahamu PESA?......... Na unaposema BUMU hulipendi sio kweli Ila tu huna jinsi ya kupata tena hilo bumu.
 
nimejifunza umenikumbusha enzi za 1st year kweli buum noumaaa unaweza ukawaza kununua meli asee

kweli mwanangu! Ila jamaa story yake imenisikitisha sana, thanx a lot bro, cjui kama ntakaonja ka boom, lakn ntafanya ile ya 0-1-1!
 
Hongera kwa kuwa m2nzi bora ila mi kama mhakiki lazima nikukosoe kidogo. Haswa pale uliposema'siwezi kuelezea kiwango cha furaha nilichokuwa nacho siku hiyo nilipoangalia jina langu na kuona nimepata division one ya point 10'
Advance hakuna 1 ya 10 kaka mwisho huwa ni 9 nawasilisha:!
 
Ulikuwa na kiwewe toka mwanzo ndo maana wahenga walisema, "Maskini akipata ****** huliambwata."
 
Back
Top Bottom