Fred Mwakitundu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 227
- 383
Taarifa kutoka Moshi zinapasha kuwa,Mahakama Kuu kanda ya moshi imemtia hatiani Hamisi Chacha aliyekuwa mlinzi wa shule ya sekondari ya scolastica baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi mwanafunzi Humphrey Makundi mwaka 2017.
Mwanafunzi huyo alikuwa anasoma kidato cha pili alishambuliwa na mlinzi huyo Novemba 6 mwaka 2017 na mwili wake ukatupwa mtoni mita 300 kutoka ilipo shule hiyo huku katika maelezo yake kwa mlinzi wa amani akidai baada ya kumpiga kwa ubapa wa panga na kupoteza fahamu,alipewa maelekezo na mmiliki wa shule hiyo,Edward Shayo kwenda kutupa mwili huo mtoni.
Shayo ni mshitakiwa wa pili kwenye kesi hiyo wakati mwalimu wa nidhamu Laban Nabiswa ambaye ni raia wa Kenya ni mshitakiwa wa tatu na wawili hao wamekutwa na kosa dogo la kuficha taarifa.
Jaji Firmin Matogolo anasoma hukumu muda huu na punde mambo yatakuwa tayari hapa
=====
UPDATES;
Mahakama Kuu imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa mlinzi wa shule ya Scolastica, Hamis Chacha kwa kosa la kumuua aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Humprey Makundi

MOSHI: Mmiliki wa shule ya Scolastica na wengine wawili wafikishwa mahakamani
Mmiliki wa Shule ya Scolastica, Moshi na wengine wawili wamefikishwa korti wakisubiri kusomewa mashtaka ya mauaji ya mwanafunzi Humphrey Makundi Mwanafunzi huyo alitoweka shuleni katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6 na baadaye mwili wake ukaokotwa Mto Ghona, umbali wa mita 300 kutoka shule...
www.jamiiforums.com