Mlinzi wa Ofisi ya Ruto Apatikana Amefariki kabla ya kuandikisha taarifa kuhusu sakata ya Jeshi

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Feb 21, 2020

Afisa wa Polisi anayehudumu katika Afisi ya Naibu Rais William Ruto (Harambee Annex) na ambaye alihitajika kuandikisha taarifa kuhusiana na sakata ya bilioni 39 inayomkabili waziri wa zamani Rashid Echesa alipatikana siku ya Alhamisi akiwa amefariki katika mtaa wa Imara Daima, hapa jijini Nairobi.

Mwili wa afisa huyo ulikuwa na alama ya risasi kichwani.
Afisa huyo inasemekana alikuwa kazini siku ambayo aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa alizuru afisi ya naibu rais William Ruto akiandamana na jamaa wawili raia wa kigeni katika sakata ya kununua vifaa vya kijeshi kwa kima cha shilingi bilioni 39.


Afisa huyo alikuwa miongoni mwa maafisa wa Jumba la Harambee Annex waliohitajika kuandikisha taarifa kuhusiana na mkutano wa Echesa katika afisi hiyo.

Maafisa wa ujasusi wanasema afisa huyo alikuwa bado hajaandikisha taarifa yake au kuhojiwa na maafisa wa upelelezi.


Katibu wa mawasiliano katika afisi ya naibu rais David Mugonyi, awali alikuwa ametuma taarifa kwamba afisa huyo wa AP alikuwa hajafika kazini kuanzia siku ya Jumatano baada ya kutakiwa kufika mbele ya maafisa wa DCI na kwamba juhudi za kumsaka zilikuwa zimeanza. Mwili wake ulipatikana dakika chache baadaye.
Bado haijabainika ikiwa afisa huyo alijiua au aliuawa na kama alijiua, alifanya hivyo kwanini na ikiwa aliuawa ni nini kilichochea mauaji y
 

Attachments

  • Screenshot_20200221-212146.png
    Screenshot_20200221-212146.png
    69.8 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200221-212141.png
    Screenshot_20200221-212141.png
    51.7 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200221-212134.png
    Screenshot_20200221-212134.png
    113.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom