Mlinzi wa mgodi wa Bilionea Laizer auawa na wasiojulikana, saba washikiliwa

Hapo target ilikuwa ni Bilione Laizer, niliwahi kusikia kuwa walikuwa kwenye mkataba watu watatu katika shimo lake, yaani yeye Saniniu, mdogo wake na jamaa mwingine mmoja.

Baadae walipoona shimo linatema kuanzia kwenye miaka ya 2016- yeye na mdogo wake wakakubaliana kumrudishia jamaa pesa zake alizojoin nazo katika mkataba so wakabaki wawili tu wanaomiliki mgodi yaani yeye Saniniu na mdogo wake.

Labda jamaa ameona amefanyiwa uhuni akaamua kufanya hayo.
si wamekubaliana lakini shida iko wapi?
 
Nimesoma habari hiyo kutoka katika ukurasa wa ripota wa billionea huyo, Millard Ayo.

Kwa kuwa JF ni kisima cha watu makini, hebu tujaribu kuelezana nini hasa inaweza kuwa sababu ya yeye kuuwawa?

=======

Watu wasiojulikana wamemuua Manace William Lemoringeti, mlinzi wa mgodi wa Bilionea Saniniu Laizer huku jeshi la polisi kupitia kwa kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Paul Kasabago likisema linawashikilia watu saba kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Kwa upande wa msemaji wa familia hiyo, Loshii William Lemoringeti, ameiomba serikali kuingilia kati suala hilo hasa jeshi la polisi ili kupata chanzo halisi cha kifo cha ndugu yao.

CHANZO: Millard Ayo
Hivi Merarani hakuna wafuasi wa CHADEMA wapewe hii kesi?
 
Hapo target ilikuwa ni Bilione Laizer, niliwahi kusikia kuwa walikuwa kwenye mkataba watu watatu katika shimo lake, yaani yeye Saniniu, mdogo wake na jamaa mwingine mmoja.

Baadae walipoona shimo linatema kuanzia kwenye miaka ya 2016- yeye na mdogo wake wakakubaliana kumrudishia jamaa pesa zake alizojoin nazo katika mkataba so wakabaki wawili tu wanaomiliki mgodi yaani yeye Saniniu na mdogo wake.

Labda jamaa ameona amefanyiwa uhuni akaamua kufanya hayo.
Saninu alinunua eneo yeye mwenyewe mdogo wake hana kitu,anamiliki 25% tu ya huo mgodi,kuna ruta anamiliki 8%,wachimbaji 10,mchina anamiliki 65% na ndio amewekeza kuanzia juu mpka hapo ulipofikia....hata mawe ya juzi mchina kachukua % yake
 
Yule jamaa alivyotolewa alianza kumsema vibaya sana laizer kuwa hakummalizia pesa zake na longolongo zingine nyingi

Ukifika mgodini utasikia mengi
Laizer anamiliki pml,kwahiyo yeye ndio mwenye eneo hizo zingine ni story tu...huyo mlinzi waliomuua ndio wanajua sababu.
Wachimbaji wa huo mgodi wengi choka mbaya hata mlinzi nae alikua hana kitu.
Watu walidhibiti mawe mwanzo mwisho istoshe hata 10% ya wachimbaji wamepewa kidogo na malalamiko yameshapelekwa wizara ya madini
 
Yule jamaa alivyotolewa alianza kumsema vibaya sana laizer kuwa hakummalizia pesa zake na longolongo zingine nyingi

Ukifika mgodini utasikia mengi
Hakummalizia kwani mkataba wa mauziano wa hisa ulikuwa ni wa awamu? Na mkataba si unaweza ukaupeleka mahakamani for enforcement? Shida ya nini?
 
Nimesoma habari hiyo kutoka katika ukurasa wa ripota wa billionea huyo, Millard Ayo.

Kwa kuwa JF ni kisima cha watu makini, hebu tujaribu kuelezana nini hasa inaweza kuwa sababu ya yeye kuuwawa?

=======

Watu wasiojulikana wamemuua Manace William Lemoringeti, mlinzi wa mgodi wa Bilionea Saniniu Laizer huku jeshi la polisi kupitia kwa kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Paul Kasabago likisema linawashikilia watu saba kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Kwa upande wa msemaji wa familia hiyo, Loshii William Lemoringeti, ameiomba serikali kuingilia kati suala hilo hasa jeshi la polisi ili kupata chanzo halisi cha kifo cha ndugu yao.

CHANZO: Millard Ayo
Inasemekana Wajeda wanaolinda Ukuta wa Mirerani ndo wameua, Polisi wameshindwa kuwakabidhi ndugu mwili kwenda kuzika, Wananchi wa Mirerani wanaandamana kudai wapewe mwili
 
Back
Top Bottom