Mlinga awataja mawaziri waongo bungeni yupo na Mwijage, adai wanatoa majibu kufurahisha bunge lkn hakuna kitu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,566
2,000
Mbunge wa jimbo la Ulanga mkoani Morogoro, Goodluck Mlinga amefunguka na kuwataja baadhi ya mawaziri wa awamu ya tano na kusema ni waongo wamekuwa wakitoa majibu bungeni kuwaridhisha wabunge na spika lakini si watekelezaji ya kile wanachokisema.

Mlinga amesema hayo leo bungeni na kumtaja Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kusema kuwa wamekua wakitoa majibu ya uongo bungeni na ambayo hawayafanyii kazi.

"Mhe Spika Mawaziri wetu wamekuwa wakitoa majibu mazuri ambayo yanaturidhisha sisi wabunge, kwa mfano majibu ya mjomba wangu Mwijage anatoa majibu kana kwamba Mungu yupo hapa lakini wakitoka hapa yale majibu hawatekelezi huko, lakini ukimbana sana atakwambia kuwa akitoka bungeni ataongozana na wewe mpaka jimboni kwako lakini mkishamaliza bunge hata simu hapokei na hilo suala la kuja jimboni halipo" alisema Mlinga

Mbunge huyo aliendelea kutaja Mawaziri ambao ni waongo "Mhe mwingine ni Kalemani naye anakwambia baada ya bunge atakuja jimboni kwako ili kukuridhisha wewe Spika na kuniridhisha mimi mbunge, Mh Spika naomba bunge lituelekeze namna nyingine ya kuweza kuwabana hawa watu ili waweze kuwajibika kutokana na wajibu yao ya uongo" alisisitiza Mlinga
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,329
2,000
Ndio kwanza wabunge wa ccm wanaanza kuamka!!! Mawaziri wanajua wabunge wa ccm ni viazi, hivyo huwa wanawapa majibu wayatakayo. Na wabunge wa ccm huwa wanajigeuza mawaziri hapo unategemea waziri ataacha kutoa majibu ya kuchomekea?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom