Mlinda amani wa UN raia wa Tanzania ameuawa nchini Congo na mwingine ajeruhiwa, JWTZ imetoa taarifa rasmi ya kifo hicho

View attachment 591398
Tume ya Umoja wa Mataifa-UN nchini Congo inasema mlinda amani mmoja ameuwawa kufuatia mapigano katika eneo la Beni kwenye jimbo la Kivu kaskazini nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP tume hiyo ilisema Jumatatu kwamba mlinda amani huyo raia wa Tanzania alipigwa risasi wakati wa shambulizi la Jumapili lililofanywa na washukiwa waasi wa kundi la Allied Democratic Forces kwenye eneo la vikosi vya jeshi.

Ilisema eneo la jeshi lilikuwa kiasi cha mita 500 kutoka kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa. Tume ya Umoja wa Umoja ilisema mlinda amani mwingine raia wa Tanzania alijeruhiwa katika mapigano na amehamishiwa kwenye hospitali ya Umoja wa Mataifa huko Goma.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alilaani mauaji hayo na aliisihi serikali ya Congo kuchunguza tukio hilo na kuwafikisha waliohusika mbele ya sharia. Katika taarifa yake aliyataka makundi yote yenye silaha nchini Congo kusitisha ghasia

CHANZO: VOA
Huyo kamanda wetu aliyefariki anaitwa nani, na pia majuruhi
 
Isije kuwa ni matokeo ya Albadir

Acha uzushi. Ingekuwa si ya amani ungekuwa unaandika madudu yako hapo kwa amani. Hebu tembelea Kongo ndio utaelewa maana ya amani!
Huyo anaandika hivyo kwasababu hajulikani kama Lissu,angekua anajulikana kama Lissu premio ingemfuata na hapo angedhibitisha kua Tz kuna amani au laa,nikwambie kitu ndugu yangu,huyo askari kapigwa risasi chini ya thelathini huko Congo,huku Lissu anamiminiwa risasi 30+.
 
RIP kamanda ila nashauri waliobaki warudishwe tu nyumbani kwani hata huku hali ni tete tunahitaji usalama zaidi
 
Acha kuwashwa tena kwenye marinda, aliekuambia huku hali ni tete nani? Unayataka ya Congo yaje hapa? Uliza sisi tulioenda kule kuku wewe.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Naamini kuna watu baadhi wanamjua humu, wengine ni ndugu yao, classmate wao, jirani yao na pia urafiki tu wa kawaida. Kwa ufupi ni kijana ambae alizaliwa Musoma mzazi wake mmoja kama sikosei alikua anaishi Dodoma. Jina halisi la kijana huyo anaitwa Mussa Jumanne, alikua fundi nzuri, dereva nzuri wa magari makubwa na madogo. Picha ningeweka hapa lakini kutokana na mtandao wa eneo nilililopo inagoma. Kupata picha yake njoo pm nikupe namba ili uangalie dp ya jamaa.
 
Back
Top Bottom