Mlimani wapinga JK kuunda Tume ya Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlimani wapinga JK kuunda Tume ya Katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280
  Mlimani wapinga JK kuunda Tume ya Katiba


  na Tutindaga Mwakalonge


  [​IMG] VUGUVUGU la madai ya Katiba mpya limechukua sura mpya baada ya uongozi wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani (DARUSO) kumpa siku saba Rais Jakaya Kikwete awe amebadili msimamo wake wa kuunda Tume ya Katiba na atangaze kuliacha suala hilo mikononi mwa wananchi.
  Mwenyekiti wa wanaharakati wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Rich Mwita, alisema wanamtaka Rais Kikwete atangaze kuliacha suala la kuandikwa kwa Katiba mpya mikononi mwa wananchi ambao kupitia mwongozo utakaotolewa na Bunge ndio waamue aina ya Katiba inayotakiwa.
  “Tunataka rais achomoe wazo lake la kuunda tume. Hatutaki yeye atuundie tume ya Katiba, tunatoa siku saba atangaze kuliacha suala la Katiba mikononi mwa Bunge maana ndicho chombo cha wananchi. Tunataka mchakato mzima wa kuandikwa Katiba mpya ushirikishe jamii na si wanasheria au kamati itakayoundwa na Rais. Asipofanya hivyo tutashinikiza kwa maandamano na mgomo. Suala la Katiba linatugusa sana,” alisema Mwita.
  Sanjari na shinikizo hilo kwa rais, dai la pili la wanaharakati hao wa Daruso ni kutaka Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, pamoja na Mwanasheria Mkuu, Frederick Werema, kujiuzulu haraka iwezekanavyo kwani walitoa misimamo inayohujumu matakwa ya umma kuhusu Katiba huku kauli zao zikidaiwa kukinzana na kile alichokisema Rais Kikwete mwenyewe.
  Daruso pia imempa siku saba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, kuonana na wanafunzi chuoni hapo vinginevyo watafanya mgomo kushinikiza kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili.
  Waziri Mkuu wa Daruso, Makuli Paul, alisema wanataka Dk. Kawambwa afike chuoni hapo ili kutambua matatizo yanayowakabili wanafunzi hao ikiwa na kuendelea kupewa fedha kidogo ya kujikimu (boom) isiyolingana na gharama za maisha ambazo zimepanda.
  Alisema ukosefu wa madarasa pamoja na viti huwalazimu baadhi ya wanafunzi chuoni hapo kusimama nje ya madarasa wakati wa vipindi hali inayowafanya wazagae nje badala ya kupata mafunzo.
  “Kumekuwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya kulala (mabweni) chuoni hapo hivyo kusababisha baadhi ya wanafunzi kulala katika korido za vyumba. Hii inahatarisha afya zetu na hakuna jitihada zozote zilizofanywa na uongozi wa chuo…na yote haya yanatokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliodahiliwa,” alisema Paul.
  Daruso imemtaka waziri huyo kwa mamlaka aliyopewa kuwarudishia miradi mbalimbali iliyofutwa hapo awali wakati wa uongozi wa serikali iliyopita ambayo ilijulikana kama DUSO na kuifufua tena.
  Aliitaja miradi hiyo kuwa ni mgahawa ambao ulikuwa chini ya serikali ya wanafunzi, baa pamoja na steshenari, miradi ambayo iliwasaidia wanafunzi chuoni hapo.
  Aidha, alisema Daruso imemwandikia barua rasmi mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika pamoja na mkuu wa wilaya ili walipatie ufumbuzi tatizo la kutokea ajali katika barabara ya Mandela eneo la Mabibo Hostel kwani wanafunzi wamekuwa wakipoteza maisha yao mara kwa mara.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280
  Mwanzo wa mwisho wa JK na serikali yake ya kifisadi umeanza inapingwa kila upande kwa sababu haina uhalali wowote wa kutuongoza na hakuna mwenye imani nayo.......................
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,345
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  GOOD................kikwete na mafisadi bado wanaamini nchi ni yao na si ya wananchi....aibu kubwa sana!.............hatutaki tumne ya rais maana zingine kibao hazijasaidia.....tume ya rais ni ya rais tunataka mchakato wetu sisi wananchi ili tuwape mashrti ya kuongozwa na si tupewe mashrti na viongozi....zama za kuhodhi zimeisha....zama za rais asishitakiwe zimeisha kwa hiyo km kikwete alisema tumwache mkapa apumzike sisi hatutamwacha hakika kwani kajihusisha kwenye kashfa nyingi na rafiki zae lowasa na rostamu tutaunda sheria za kuwashitaki ili iwe fundisho
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Huo ndo uwezi harisi wa kikwete aliye tutapeli wananchi na tukampa kura kwa 80%. Lakini safari hii tumemkataa lakini kateuliwa na Tume ya taifa ya uchaguzi na kiutaratibu hatutakiwi kuhoji mahakamani
   
Loading...