Mlimani park | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlimani park

Discussion in 'Entertainment' started by misha, Dec 10, 2010.

 1. m

  misha Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ni miongoni mwa wasikilizaji na wafuatiliaji wa Mlimani pamoja na vikundi vingine vya muziki nchini,kwa bahati mbaya bado sijakisikia kibao cha Mlimani(TENDE HALUA HALUA) kilichopigwa 'full stop' na SMZ,kwa kutumia mashairi ya matusi-kwa siwezi kusemea sana hili, ingawaje ndugu Jimmy Chika ametamka kuwa mtunzi ni mtu anayejiheshimu-nifahamuvyo mashairi huwa na miguso tofauti tofauti, kuna wakati ujumbe wa mshairi unaweza ukachora picha tofauti kabisa na ile iliyokusudiwa na mtunzi na kuleta maana isiyo-kusudiwa, haya yamewakuta baadhi ya vinara wa mashairi nchini,Ustaadh Andanenga na UKUTA waliyaongelea haya. Kuna taarab ya East African melody-Tamba, kama sikosei imeimbwa na Sabah Salum, nimejaribu kuifuatilia maana yake kwa muda na kulinganisha na rafiki yangu tukapata maana tofauti kabisa! Mimi nikiwa na mtazamo kuwa ni mashwala ya 'ILMU au ELIMU', rafiki yangu anamtazamo kuwa ni mapenzi ya wapendanao kimahaba(mahaba kwa maana ya 'erotic').
  Kwangu mimi mwimbaji anatuacha solemba, anaongelea mambo mengi sana anayotaka kuyafanya katika mkesha na habibi wake,kikubwa anaanza kwa kutamka 'tukeshe tukitazamana' na mengine yanafuata kutoka kwenye mkesha wa kutazamana. kwangu mimi huku kutazamana siyo kwa kawaida ni kama ilivyo kuwa kwa Hayati Maulana Rumi na Shamsi, sijui wengine mnaonaje. Nitafurahi kusikia wanajamvi kuhusu walivyouelewa ujumbe wa Taarab ya 'Tamba' East African Melody-Sabah Salum.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. m

  misha Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana X-PASTER kwa kuweka kideo
   
Loading...