Mlimani City (Dar es Salaam) Vs Rock City Mall (Mwanza)

Mmhh!wasukuma bwana hako kamji kenu ht mkononi hakajai kupata kamall kamoja bas hatuna raha loooh!
Pambaneni na rock city yenu
Mlimani city ya mzaramo,wewe kabila lako ni la mkoa gani?
Tujuze kwanza,halafu utuambie Kuna Mall gani huko ya kutisha?
Mimi kwetu Mbeya,hatuna Mall yoyote ya maana.
 
Rock Citya Mall si ya kufananisha na Mliman City, Labda uifananishe na AIM Mall ile ya Arusha, tena inaweza zidiwa na AIM Mall na yenyewe ikija kuchangamka
 
Nimesoma makala hii. Sijaona chochote cha kuizidi Mlimani City Mall,na siyo eneo la mradi wote,kwanza kuweka kumbukumbu sawa.
Ama kuhusu gharama za mradi wa Mlimani City kwa wakati huo ilikua ni 117bn/-, ingawa hii siyo hoja inayotajwa hapa. Hoja ni jengo la Mall.
Parking ya pale Mlimani City ni magari 3000, hiyo achilia mbali kule Mlimani City Conference Hall na pale yalipokuwa makao ya ofisi za Vodacom.
Tukija kwenye finishing,Rock City Mall ni Asian Culture Exterior Finishing,wakati Mlimani City ni Western Culture. Architects wanajua namaanisha nini.
Ukibahatika kwenda miji ya Asia kama Shanghai,Beijing,Seoul,Hongkong na Tokyo naksi za majengo yake ni kali sana kuliko Paris,Berlin,London,New York et al hiyo kwa sababu Waasia huwa na finishing za kumeremeta kama vile Waarab Wahindi nk.
Tuje kwenye ubora,Nguzo zote na roof structure yote ya Mlimani City ni Structural Steel Work,ambapo zilijengwa na Kampuni ya Kitaliano iitwayo CSI Engineering.
Technolojia ikiyotumika kuweka zege ni kwa kutumia paver maalum iitwayo Bidwell. Kama hiyo haitoshi,zile bati zimeezekwa kwa Technolojia kutoka Afrika ya Kusini ambapo kiwanda cha muda kililetwa pale na rollers kukunjuliwa na kuezekwa bila Misumari, na ikiwa na Span ya upana wa Mita 70,ilitakiwa Lattice Roof Truss ili kuweza kubeba bati hizo special.



Kwa kumalizia tu, sijui ukubwa wa JENGO(siyo Kiwanja chote na future development) ila naamini kwa ukubwa Rock City Mall haiwez kuizid Mlimani City Mall. Parking Lot ya Mlimani City ni kubwa na inabeba magari mengi kuliko Parking ya Rock City Mall.
Yote kwa yote,hongera Mwanza kwa kuendelea kupiga hatua.
117 bn tshs!!! Acha uwongo ww
 
Rock Citya Mall si ya kufananisha na Mliman City, Labda uifananishe na AIM Mall ile ya Arusha, tena inaweza zidiwa na AIM Mall na yenyewe ikija kuchangamka
Nimepita rock city mall wiki mbili zilizopita. Ni kubwa ukilinganisha na Mlimani city. Lakini ukiondoa ukubwa haiwezi kuisogelea Mlimani city kwa kitu kingine chochote
 
Acha ushamba wa kisukuma na unaonekana bado uko huko kijijini na huijui Dar. Wazaramo tofauti na nyie wa vijijini/mikoani, MTU mmoja akiwa tajiri kabila zima linamuabidia na kumuonea fahari. Huku mjini kila mtu hata akiwa tajiri ni yeye na familia yake ndio maana hausikii upuuzi wa kutaja na kuorodhesha majina ya mnaoona matajiri(maskini tu). MTU akijenga nyumba ya bati kama hao wa ulongoni huko kwenu ni mnamuhesabu tajiri!
In fact anayeishi na kumiliki nyumba Tandale,Mbondole na maeneo mengine ya Dar ambaye ni wa kawaida kwa Dar lakini huko mikoani ni tajiri. By the way Dar hakuna nyumba za makuti tofauti na Mwanza ukitoka katikati ya mji ukifika Kisesa unaanza kuona umaskini wa wasukuma kwenye vijumba vya udongo vilivyoezekwa na nyasi na vidirisha vidogo labda Dar umeona zile Pub na Bar ukafikiri ni nyumba.
Kisesa ni ndani ya jiji kwan?
 
Nimepita rock city mall wiki mbili zilizopita. Ni kubwa ukilinganisha na Mlimani city. Lakini ukiondoa ukubwa haiwezi kuisogelea Mlimani city kwa kitu kingine chochote
Nimepita mlimani siku si nyingi... Na kilichoizidi ni uchangamfu tu.
 
117 bn tshs!!! Acha uwongo ww
Hoja siyo ukubwa wa ki MSTATIRI AU MRABA, Hoja ni structure au ramani yake na mwonekano katika uzuri wa mjengo. Unaweza jenga nyumba ya vyumba 7 kama darasa , lakini akatokea mwingine akajenga vyumba 3 akakupoteza kabisaa katika appearance. Hivyo Rock city mall ni nzuri kuliko Mlimani city.
 
Kwa uzuri
1.Aura Mall Dar
2..Mkuki House Mall Dar
3.Aim Mall Arusha
4.Mlimani City Dar
5.Quality Centre Dar
6.Rock City Mall Mwanza

Kwa ukubwa
1.Rock City Mall 50k sqm
2.Mlimani 30k sqm
3.Quality Centre 30k sqm
4.Mkuki House Mall 28k sqm
5.City Mall 20k sqm
6 Aim Mall Arusha 15k sqm
7.
wa subiri na tumalize busisi /Kigongo ferry bridge... watakaa sana hao na dar yao.
 
Tukiichukua rock city tukaiweka Dar pale opposite na Mlimani city nadhani,mlimani cty itafaa kuwa kama store ya Rock city...Huko ndio kulinganisha sasa!
 
1.Thamani ya jengo Rock city Mall inathamani kuliko mlimani city.
2.Ukubwa Rockicity Mall ni kubwa kuliko Mlimani city. ,3.Ubora, uzuri na mwonekano Rock city mall ni nzuri kuliko mliman city.
4. Uchangamfu was biashara mlina city kumechangamka kuliko rock city mall

Tuache utani.. Unless mtu hujawahi kufanya manunuzi kwenye hizo malls mbili. Rock City Mall ipo so limited.. Mfano: Mtu unahangaika mall nzima kutafuta nguo na viatu vya watoto, halafu wauzaji wa humo wanakuelekeza uende Salma Cone utapata nguo nzuri.
Shiiit!!!
 
Back
Top Bottom