Mlima Kilimanjaro kuendelea kutangazwa upo Kenya nani alaumiwe? Nini kifanyike?

Nani wakulaumiwa?

  • Serikali

    Votes: 6 46.2%
  • Watanzania

    Votes: 2 15.4%
  • Bodi ya utalii

    Votes: 5 38.5%
  • Serikali ya Kenya

    Votes: 0 0.0%
  • Raia wa Kenya

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    13
  • Poll closed .

Tz boy 4tino

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,598
1,816
Mlima Kilimanjaro kuendelea kutangazwa upo Kenya na serikali ya Kenya/raia wa Kenya, Nani alaumiwe? Nini kifanyike?

Je ni uzembe wa wahusika kutotangaza vivutio vyetu?

Ni uzembe wa viongozi wetu kutolichukulia hili swala kwa uzito unaostahili?

VIONGOZI WETU KUKOSA UZALENDO NA RASILIMALI ZA TAIFA?
Nini kifanyike ?.

Serikali iichukulie hatua kali serikali Kenya ?..

Serikali iuunde kamati maalumu kuzishtaki website/taasisi zote zinazotoa taarifa za uongo kuhusu mlima wetu ? ..

Tuwaache Wakenya waendelee kufaidi matunda ya mlima Kilimanjaro?.

Je na sisi Watanzania tuanze kampeni ya kutangaza vivutio vya Kenya vipo nchini kwetu ?.

Tuwaache Wakenya waendelee onekana wapuuzi na wajinga kwa kudanganya watu 21st century ambapo Dunia imekuwa kama kijiji na kila taarifa legitimate zaweza patikana mtandaoni, Watalii wengi huandaa safari zao kuputia mitandaoni ?.
N.B: kuna travelin agency nyingi Nairobi zilizo na website zao zijulukanazo kimataifa na huchukua watalii na kupeleka kwenda kupanda mlima Kilimanjaro..

Tufunge mpaka eneo linapakana na mlima Kilimanjaro kudhibiti watalii kutokea Kenya na kuingia moja moja mlima Kilimanjaro pamoja na kuweka ulinzi mkali?..

REJEA , HISTORIA ;

Mlima Kilimanjaro umekuwepo nchini Tanzania tangu ukoloni wa mjerumani.
Kuna imani ya kwamba mlima huo ulikuwa Kenya na malkia Elizabeth wa Uingereza aliukabidhi kwa Wilhem aliyekuwa Prince wa Germany OestAfrika (Tanganyika, Rwanda, Burundi ) hilo sio kweli.
Mlima Kilimanjaro haujawahi kuwa Kenya bali hizo ni propaganda za baadhi ya watu wa Kenya kuhalalisha wizi wao.
Hadi kipindi hicho kulikuwa hamna nchi inayoitwa Tanganyika wala Kenya kulikuwa na makabila tu na jamii za kifalme tu, kutbitisha hilo tazama Wachagga/Wapare na watu wa upande wa pili wa Kenya hawafanani hata kidogo(muonekano, tabia). MLIMA KILIMANJARO HAUJAWAHI KUWA KENYA.

MUHIMU ;
~Ushindani wa kibiashara kativya Kenya na Tanzania upo kwa muda mrefu na Duniani kote lakini upotoshaji wa taarifa hilo swala ni harikubaliki kabisa (politically incorrect )
~Hakuna vivutio vya Kenya vinavyoifaidisha Tanzania mmoja kwa mmoja.
~Ni miezi kadhaa tu iliyopita serikali ya Kenya ilikataa gesi ya Tanzania kwa sababu wanaona Tanzania inafaidika kuuza mitungi pamoja na gesi. Hivyo wao wanataka tuwauzie gesi kupitia Mombasa ili wapate faida ya kuuza gesi yetu kwa kupitia mitungi yao. (Tugawane faida , na tusipate faida total benefit na rasilimali yetu) kwa nini leo watu haohao tunagawana nao faida ya mlima Kilimanjaro ?????.... still scratching my head.

Cc, Watanzania Wazalendo Community

Naomba unisaidie ku share (Kwa Mtanzania yeyote Mzalendo)..
 

Attachments

  • Screenshot_20170905-140515.png
    Screenshot_20170905-140515.png
    320 KB · Views: 72
  • Screenshot_20170905-140135.png
    Screenshot_20170905-140135.png
    96.4 KB · Views: 66
  • Screenshot_20170905-135930.png
    Screenshot_20170905-135930.png
    137.4 KB · Views: 72
  • Screenshot_20170905-135920.png
    Screenshot_20170905-135920.png
    68.3 KB · Views: 64
  • Screenshot_20170905-135842.png
    Screenshot_20170905-135842.png
    190.3 KB · Views: 80
  • Screenshot_20170905-135831.png
    Screenshot_20170905-135831.png
    97.2 KB · Views: 66
  • Screenshot_20170905-134946.png
    Screenshot_20170905-134946.png
    93.6 KB · Views: 70
  • Screenshot_20170905-134216.png
    Screenshot_20170905-134216.png
    210.4 KB · Views: 68
  • Screenshot_20170905-134149.png
    Screenshot_20170905-134149.png
    46.6 KB · Views: 65
Mimi nadhani cha kufanya hapo ni kuuhamishia tu huko huko wanakoutangaza kuwa wao.
 
Kama hivyo tubadili jina la nchi liwe 'KILIMANJARO' badala ya Tanzania. Halafu hutasikia tena hizo porojo ulizosema.

Kenya wana mlima unaitwa Mt. KENYA na ndio jina la nchi yao.

Ukiwa sehemu za Kenya unaweza kuuona Mt. Kilimanjaro na ukaupanda kwa upande huo kwa kuvuka mpaka. Huenda hii ndiyo kigezo chao cha kusema "njoni muuone na kupanda Kilimanjaro hapa Kenya"
Ni kama vile Congo wakisema ziwa Tanganyika liko kwao utabisha? Si wenyewe mmesema Tanganyika haipo?
Baadhi ya watalii wanachotaka ni kufika Kilimanjaro hawajuwi au hawataki kujihusisha na mambo (local) yasiyowahusu.
 
Mkuu labda mimi sijui kusoma kizungu vizuri,ila kwenye ivyo vibandiko naona hawajataja moja kwa moja kwamba huko Kenya.Ila wanaonyesha kuna side umepakana na Kenya.Na pia vingine vinaonyesha kabisa huko Tanzania e.g Moshi.Cha muhimu ni Serikali yetu ianze rasmi kuutanzgaza maana wenzetu ni wajanja zaidi.
 
Usipotoshe watu. Labda umeshindwa kutafsiri lugha. Mtangazaji kasema 'Njia ya rongai ndio pekee unayoweza kuupanda mlima kilimanjaro kutoka kaskazini kwa upande wa kenya.' Hakuna mahali amesema mlima uko kenya. Kwa taarifa yako dunia nzima sasa huwezi kudanganya mlima uko Kenya. Pamoja na hilo asili mia kubwa ya watalii wanaokuja Tanzania huingilia Kenya na hii ni kutokana na ndege nyingi za kimataifa kutua Nairobi zaidi. Sasa hii ni changamoto kwa serikali yetu na ilifanyie kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu labda mimi sijui kusoma kizungu vizuri,ila kwenye ivyo vibandiko naona hawajataja moja kwa moja kwamba huko Kenya.Ila wanaonyesha kuna side umepakana na Kenya.Na pia vingine vinaonyesha kabisa huko Tanzania e.g Moshi.Cha muhimu ni Serikali yetu ianze rasmi kuutanzgaza maana wenzetu ni wajanja zaidi.


Angalia vizuri kuna sehemu wamesema hadi mkoa wa kilimanjaro upo Kenya...
 

Attachments

  • 20170905_190223.png
    20170905_190223.png
    211.3 KB · Views: 58
  • 20170905_190140.png
    20170905_190140.png
    164.1 KB · Views: 57

Hujanielewa mlima upo Tanzania asilimia 100 na mpaka ni zaidi ya km 20 but unaweza kupanda ukutokea Kenya kwani eneo la mlima ni kubwa
 
Hujanielewa mlima upo Tanzania asilimia 100 na mpaka ni zaidi ya km 20 but unaweza kupanda ukutokea Kenya kwani eneo la mlima ni kubwa
nimekuelewa mkuu hila nadhani njia za kuingilia mlima huo ziwe upande wa Tanzania tu na sehem za kenya ulinzi uwekwe
 
Back
Top Bottom