Mlima Kilimanjaro kama ulivyosanifiwa katika kitabu ''Rajabu Ibrahim Kirama Jemadari wa Vita kuwa Jemadari wa Uislam''

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,253
MLIMA KILIMANJARO KAMA ULIVYOSANIFIWA KATIKA KITABU ''RAJABU IBRAHIM KIRAMA JEMADARI WA VITA KUWA JEMADARI WA UISLAM''

''Mlima Kilimanjaro unaonekana muda wote; ikiwa hakuna mawingu; tokea Moshi.

Huu ni mfano wa alama ya kueleza kuwa chini ya mlima ndiyo nchi ya Wachagga.

Mlima Kilimanjaro kwa namna ya ajabu ulikuwa alama kwa marafiki na maadui kuwaelekeza kuwa chini ya mlima huu wenye theluji katika tropiki ndiko waliko Wachagga.

Wamishionari walipongia Uchaggani kutokea upande wa pili wa mlima au kutokea pwani lau kama walikuwa na watu wa kuwaongoza, macho yao daima yalikuwa yakitazama mbinguni kuutafuta Mlima Kilimanjaro na walipouona walijua kuwa safari yao imefikia mwisho.

Wachagga toka zama hizo walijihisi na kujiona ni taifa na ardhi yao yote ni nchi kamili.

Nchi yenye mipaka yake ya kueleweka.

Wenye lugha moja lau kama makabila yao ni mengi na yakiishi sehemu mbalimbali chini ya mlima.

Mlima Kilimanjaro uliwaongezea Wachagga mapenzi kwa nchi yao kwa ajili ya ule uzuri wake.

Mlima umesimama ukiinamia ardhi yote; hasa unapokuwa haujafunikwa na mawingu kwani kuna siku Wachagga huamka na wasiuone mlima.

Wachagga wanaamini bila Mlima Kilimanjaro hakuna Wachagga.

Na hakika kabisa unaweza mtu ukafikiria na kusema kuwa, Mlima Kilimanjaro ni nembo ya matumaini makubwa kwa ustawi wa Wachagga.

Mlima pia ni sawa na alama inayomuonesha rafiki au adui, walipo Wachagga.

Ikiwa una haja nao na unawatafuta iwe kwa kheri ama kwa shari.

Kwa anayekuja, kokote anapotokea: iwe kutoka pwani ya mbali za ardhi ya Wachagga; au nyuma ya mlima, kutokea Kenya, Mlima Kilimanjaro utaonekana umesimama hausogei pale ulipo.

Na kila unapoukaribia ndipo unapozidi kujidhihirisha ukubwa na uzuri wake.

Njia nzima kuelekea Machame ni ardhi yenye rutuba na migomba imepandwa kila mahali kulia na kushoto ya njia na sehemu nyingine imepandwa kahawa.

Mbele kidogo unapoingia Nkuu kijiji alichozaliwa Muro Mboyo baba yake Kirama Mboyo miaka ya 1800.

Hili ndilo lilikuwa jina lake kabla hajaingia Uislamu na kuitwa Rajabu Ibrahim Kirama.''
 
Wachagga toka zama hizo walijihisi na kujiona ni taifa na ardhi yao yote …
Picha
Screenshot_20201217-215847~2.jpg
Screenshot_20201217-220123.jpg
 
Shukran sana Shekh Mohamed Said.
Leo siku nzima nimekua nafatilia kama umeandika chochote kuhusu miaka 52 ya BAKWATA
Brada...
Kuna kipi cha kuandika kuhusu BAKWATA?

Nipe fikra nini unadhani Waislam wangependa kujua kuhusu BAKWATA?
 
MLIMA KILIMANJARO KAMA ULIVYOSANIFIWA KATIKA KITABU ''RAJABU IBRAHIM KIRAMA JEMADARI WA VITA KUWA JEMADARI WA UISLAM''

''Mlima Kilimanjaro unaonekana muda wote; ikiwa hakuna mawingu; tokea Moshi.

Huu ni mfano wa alama ya kueleza kuwa chini ya mlima ndiyo nchi ya Wachagga.

Mlima Kilimanjaro kwa namna ya ajabu ulikuwa alama kwa marafiki na maadui kuwaelekeza kuwa chini ya mlima huu wenye theluji katika tropiki ndiko waliko Wachagga.

Wamishionari walipongia Uchaggani kutokea upande wa pili wa mlima au kutokea pwani lau kama walikuwa na watu wa kuwaongoza, macho yao daima yalikuwa yakitazama mbinguni kuutafuta Mlima Kilimanjaro na walipouona walijua kuwa safari yao imefikia mwisho.

Wachagga toka zama hizo walijihisi na kujiona ni taifa na ardhi yao yote ni nchi kamili.

Nchi yenye mipaka yake ya kueleweka.

Wenye lugha moja lau kama makabila yao ni mengi na yakiishi sehemu mbalimbali chini ya mlima.

Mlima Kilimanjaro uliwaongezea Wachagga mapenzi kwa nchi yao kwa ajili ya ule uzuri wake.

Mlima umesimama ukiinamia ardhi yote; hasa unapokuwa haujafunikwa na mawingu kwani kuna siku Wachagga huamka na wasiuone mlima.

Wachagga wanaamini bila Mlima Kilimanjaro hakuna Wachagga.

Na hakika kabisa unaweza mtu ukafikiria na kusema kuwa, Mlima Kilimanjaro ni nembo ya matumaini makubwa kwa ustawi wa Wachagga.

Mlima pia ni sawa na alama inayomuonesha rafiki au adui, walipo Wachagga.

Ikiwa una haja nao na unawatafuta iwe kwa kheri ama kwa shari.

Kwa anayekuja, kokote anapotokea: iwe kutoka pwani ya mbali za ardhi ya Wachagga; au nyuma ya mlima, kutokea Kenya, Mlima Kilimanjaro utaonekana umesimama hausogei pale ulipo.

Na kila unapoukaribia ndipo unapozidi kujidhihirisha ukubwa na uzuri wake.

Njia nzima kuelekea Machame ni ardhi yenye rutuba na migomba imepandwa kila mahali kulia na kushoto ya njia na sehemu nyingine imepandwa kahawa.

Mbele kidogo unapoingia Nkuu kijiji alichozaliwa Muro Mboyo baba yake Kirama Mboyo miaka ya 1800.

Hili ndilo lilikuwa jina lake kabla hajaingia Uislamu na kuitwa Rajabu Ibrahim Kirama.''
Nilitaka kushangaa hii post haina lolote kuhusu Uislamu. Nimefarijika kukuta sentesi ya mwisho ina hiyo kitu
Post nzuri kaka, hongera
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom