Mlevi, mzee wa kupiga hesabu baada ya matumizi

Pombe pombe pombe nakuita Mara 3 nilikaa miaka 4 bila kunywa pongwe siku moja jion Niko na kabaiskel nafanya mazoez nakunja Kona ya Kwanza kabar haka hapa maraaaaa paaap nasikia " classmate am happy to see you ,,,you are warmly welcome " najuta kuifuatisha hii kauli.


Ile nakaaa katika kiti tu Safar 8 mezan paaaap hapo nikajua Safar moja huanzisha nyingne sijui nilifika vip Atm na nilichokuwa nataka enda kufanya sikwenda nikajikuta naamka home miguu Ina matope kabaiskel kangu kamepinda Sterling yake saa Saba mchana wife kashika tama jicho kalitoa balaaaaa nikajua Leo nafwaaaaaa

Siku nakuja pewa taarifa kumbe maofisa wa polisi wakiwa Doria waliniona na wakawasiliana na wife kupitia simu yangu mpaka wakafika kwangu

NB: PENDEN KUNYWA MAENEO YA NYUMBANI MNAPOKAA,

MSIWEKE SIMU ZENU PASSWORD HASA UKIWA MAENEO YA NJE YA NYUMBANI

Vita kubwa tunayo ishindwa Ni Vita ya nafs na vile tunavyokutana navyo
 
Daah nami nitoe changu siku tuko pande fulani niko mwenyewe napiga maji mfukoni nina 2k nikasema napiga ugarii kitimoto kisha nashushia serengeti lite za ten jumla 14 buku la bado itimie 15, wee nafika bia ya tano jamaa angu akaniita jina langu la utanii alinipigia simu, wee tajiri mtoto uku wapiii aisee ukiniita hilo jina naweza kukuhonga hadi bandama bwana wee nikamwambia njoo Gwambina tulitoka saa 11 alfajiri baridi kinoma kufika home pombe imekata nimebakiwa na 69 na hiyo hela ilitakiwa nimpatie wife alikuwa anaenda safari kikazii aisee bado siku nyingine nikaanguka kuteguka mkono wa kulia na mguu nikajikuta niko chini ya karafati nimetulia kabisaa
 
Hata kama hakuna access ya kutoa hela mlevi hakosagi mbinu ya kupata hela ya kunywa kama ameishiwa atapambana hadi apate ya kukidhi haja yake.
Huu ni ukweli, Kuna kipindi nilikaa chini kucheki vile vikaratas wanatoaga mawakala wa CRDB ukitoa pesa aisee zaidi ya 4M ndani ya wiki jamani na wakati huo Natakiwa kwenda likizo. Ilikuwa ikifika muda nimeishiwa bar namuita boda anipeleke ATM yoyote hata Kama ipo KM 30 lazima tufike kulalake.
 
Hakuna siku nzuri kama siku nikiwa natoka kazini huku nikijua kesho yake sintoingia (off), koo huwa inanikereketa sababu ya kiu ya pombe huwa natamani nipae ili niwahi kufika mjini nianze kuzigwida.

Mara tu nifikapo town hatua ya kwanza huwa ni kwenye ATM kuvuta mpunga, nikiwa na salio kwenye account furaha yangu huwa maradufu. Naweka kadi kwenye ATM kwa madaha ikifikia kuchagua lugha nachagua ngeli (kizungu), naweka namba za siri kisha nabofya kitufe cha kiwango cha juu (kwa kadi yangu ni mia4) mara mbili. Hakuna mlio mzuri kama ule wa ATM ikihesabu hela ule mlio wa “Trrrrrrrr….!” acha kabisa! Wakati nasubiri muamala mkono mmoja upo kiunoni na mwingine ukichezea uchebe kidevuni mara ‘kratcha ka!’ kijimlango cha ATM kinafunguka mzigo huu hapa, navuta mpunga wangu nakunja mara mbili na kuweka mfukoni sinaga hobby ya wallet niliwahi kununua moja nikaitumia kama mara mbili tu nikaona inaongeza ujazo wa mfuko nikaitupilia mbali. Nasikia kuna watu huwa wanaweka mabox kwenye wallet zao kutunisha mifuko! Dah! Watu tunatofautiana sana. Wakati natoa laki nane nilikuwa na akili zangu timamu nikipiga hesabu za maana sana kichwani, mimi pekeangu siwezi kunywa hela yote hiyo ila huwa napenda kuwa na akiba ili kujiamini na niweze kuamka na hela ya kutosha siku inayofuata najipa moyo nitajitahidi nisichezee hela kwa mambo yasiyo ya lazima.

Ikiwa mapema huwa nachagua bar zilizotulia au hotel huwa napenda ukimya au mziki wa taratibu na wawepo wahudumu warembo kama sio wote basi hata wawili watatu. Nachagua meza ya kona sehemu ambayo nitaweza kuona watu vizuri kuliko wao kuniona mimi (walengwa hapa ni madem, mwanaume nitake kuwaona iweje wakati sina mpango wa kuhitaji ofa ya mtu!). Basi naagiza Heineken baridi kama jua ni kali au ya moto kama hali ya hewa ni ya kawaida. Naanza kugonga vitu huku nikiperuzi mitandao ya kijamii.

Baada ya bia ya 4 au 5 naagiza nyama choma nusu ya kuku, mbuzi au ng’ombe. Kitimoto situmiagi nilikulaga zamani nikaacha kwasababu za kiimani na kiafya “Mbona pombe unakunywa!?” jibu langu: nguruwe ina mbadala wa nyama nyingine ila pombe haina mbadala :p.

Baada ya bia ya 8 hivi huku giza likiwa limeingia rrraha inaanza kunijia. Najisikia amani moyoni natafakari maisha ninayoishi na kuona ni maisha ya furaha sana siwazi wanaonizidi kipato naangalia ninaowazidi kipato. Nazungusha macho meza mbili tatu naona watu wamejaza bia mezani kama mafungu ya nyanya gengeni natabasamu, mimi na rafiki zangu tabia hii huwa tunaita ushamba huwa ni tabia ya kabila fulani hivi au wale jamaa wa machimboni. Nikiangalia bia walizojaza ni za buku jero lakini sifa kibao. Najiona fahari mimi kunywa bia ya bei zaidi yao, wanywaji wengi hii huwa tunaisema moyoni maana ukisema hadharani utaonekana mshamba au limbukeni. Muda huo nasikiliza nyimbo huku nikinyanyua kiatu na kupiga chini taratibu kufuatisha beat za mziki, ikiwa ni mziki wa old school huwa napata raha zaidi maana nilikuwa teenager miaka ya 90’s kipindi hicho tunatumia tape.

Wakati huu ndio naanza kujiulizisha kwa muhudumu “mbona umekaa mbali na mteja wako?” (mteja nikimaanisha mimi) maranyingi wahudumu wakiona dalili za mfuko wa mteja wanaemuhudumia kuwa vizuri huwa hawapotezi hii nafasi hatakama ana wateja wengi atahudumia huku akija kukaa na wewe (hii inategemea na masharti ya eneo husika kuna baadhi ya hotel hawaruhusu muhudumu kukaa na mteja au kunywa muda wa kazi). Basi muhudumu akikaa namwambia ajihudumie kinywaji, tatizo hawa wahudumu (wengi wao) akishakuona unakunywa bia ya bei kidogo basi na yeye hatoagiza bia za kawaida hatakama anakunywaga Balimi.

Mzuka ukianza kunikolea huwa lazima nicheki na mmoja wa rafiki zangu mlevi mwenzangu ajumuike nami akisema hayuko vizuri namtoa wasiwasi asiogope aje, kama ataniambia yupo maeneo fulani ambayo ni mazuri kwangu basi nitamfata mimi. Nikiondoka muhudumu anaachwa kama alivyo bila kujali amekunywa bia zangu ngapi, mtindo wa kupita na ma bar maid nimepunguza sana(sijaacha lakini).

Pombe ikishakolea zaidi na usiku ukishakuwa mnene, sehemu iliyotulia huwa naona si dili tena akili yote huamia ushenzini (katikati ya mji kwenye bar kubwa zenye vibe na madem wengi) nikifika hapo si nshalewa vibe lake huwa so la mchezo madem ya mjini utayasikia tu sauti zikitoka huku na kule “Mtata!... Mtata!”

Mara muhudumu anakuja ananiambia kaka unaitwa na dada pale kwenye meza ile, naongozana na muhudumu nikipita katikati ya wateja kibao bila kujali (japokuwa mimi ni mtu wa aibu nikiwa sijalewa) huku mziki mkubwa ukipigwa na chombeza za DJ (wazee wa ushenzini mnajua mbwembwe za maDJ hawa) mimi huyo hadi kwenye meza niliyoitwa, nikifika hapo nasalimia huku nikizungusha jicho kuangalia vitu kadhaa; nimeitwa na nani, nshawahi kupita nae au bado kama ni mshkaji tu na sina mpango nae nacheki alio nao kama kuna chombo, nikiona sio dili namwambia muhudumu awape moja moja kisha nasepa.

Kumbuka mia8 bado yote kabisa kwahiyo bado najiamini mfukoni nna chochote hivyo sihofii. Mshkaji akiniomba bia nampa, wakati huo muhudumu anayenihudumia ana desperado mkononi bili juu yangu na nikilipia bili ikibaki buku anajikausha hairudishi nikitaka kulipa bili nachomoa teni teni tu nikipewa change naweka mfuko mwingine situmii hizi change kulipia.

Unafika muda naona sasa nitafute chombo ya kulala nayo, mara wanaingia watoto wakali wawili wanakuja kukaa meza ya jirani yangu, kila nikipiga funda jicho kwao huku nikipiga hesabu na kufanya chaguzi langu kabisa. Namtuma muhudumu anamwita mmoja namkaribisha nikimwambia wajumuike nami wakati huo wameshaagiza Savana moja moja wanakuja kukaa nami na vinywaji vyao mmoja akiwa karibu yangu. Baada ya kufahamiana na story mbili tatu muhudumu anasogea kutusikiliza ili atuongeze vinywaji, huku wakiangaliana wakiwa kama watu wenye jambo fulani moyoni yule chaguo langu anavunja ukimya ananiambia “tusikuchoshe kununua Savana bora utuchukulie Scotch Whisky maana sisi tunapenda pombe kali” mwenzake anaitikia kwa kichwa kusapoti huku wakijichekesha. Namwambia “hakuna shida muhudumu waletee scotch whisky”. Kabla muhudumu hajaondoka mwenzake anasisitiza “Monkey Shoulder ee…” niliona kama wananivuruga mara skochi mara nyani . Ukweli mimi si mtaalamu wa pombe kali labda Gordons au Konyagi .

muhudumu aliwaelewa mzigo ukaletwa mezani na glass mbili za whiskey wenyewe waliita whiskey tumbler hili nalo nilikuwa silijui (msinicheke nshawaambia mi si mzoefu wa pombe kali) na kitunzio cha ice wakaanza kugonga vitu. Hawa madem ni magumegume ya mjini (baadae nilikuja kugundua huyu wangu ndio alikuwa ametoka kumaliza chou kikuu nchi jirani) maneno mawili kizungu achana na wale wa uswazi muda wote story za madera, vigodoro na vituko vya michambo, japokuwa mimi si msomi ila hizi st Kayumba nilipita pita jumlisha udukuzi wa watoto wa mjini. Muda si mrefu nikaita mtu wa jikoni kutusikiliza nikiwaachia uhuru wao waamue tunakula nini. Hata sitaki kuwachosha kwa maneno mengi wenyewe mnajua madem wa mjini wanakulaga nini.

Tumepiga vitu vyetu pale tukatosheka, pamoja na kuwa madem wa mjini lakini hawa madada hawakuwa watu wa tamaa kuponza kichwa. Wenyewe ndio waliniambia tukalale wakati huo chombo yangu imeshaanza kuniita bae muda mwingi akiwa ameniegemea begani “bae tukiwa tunaenda kulala tumpeleke dada yangu mitaa ya Bomani kwanza” mtoto aliongea huku akinipapasa kifuani alikuwa amenizowea utadhani ni wapenzi wa zaidi ya mwaka, maisha haya bana raha sana “hakuna shida Mpenzi” huwa sina tabia ya kuwabishia watoto wazuri nikiwa na kitu mfukoni (kwa level yangu laki8 si hela ndogo)

Bili ikaja mezani ilikuwa kama mia tatu na point hivi (achana na zile bili za kwanza ilikuwa kila hatua kadhaa nalipa) chombo yangu ikachukua ile bili kama kuhakikisha akasema akiwa hana wasiwasi “ni sawa bae” nikamsapoti huku nikitoa mpunga nikampa muhudumu akalipie na jikoni huku tukinyanyuka tukaondoka japokuwa kulikuwa na vijisenti vya chenji sikuwa na muda wa kusubiri nikamwambia muhudumu “keep change”.

Baada ya kumuacha dadamtu kwake nikabaki na mtoto nikampeleka hotel nzuri japokuwa kawaida yangu ni lodge za 30 - 40 nikaenda hotel ambapo bei ya chumba cha chini ni 100,000. Kujihami na hili nikapita tena bank nikatoa laki mbili kisha tukaenda kulala.

Alfajiri pombe zikiwa zimeanza kupungua usingizi ukakata mawazo yakanijia nikavuta picha nilivyotumia hela jana, nikiwa nimelala chali nikageuka kumuangalia mtoto alikuwa amelala sura yake ya kitoto ikivutia zaidi, shuka ikiwa imefunika eneo dogo tu la makalio yake na kuacha eneo kubwa likiwa wazi nikajipa moyo na kujisemea moyoni “ukweli nimekula chombo ya maana sana” nilijisemea huku nikitabasamu. Hapo hapo ukuni ukastuka nikamgeukia mtoto nikapeleka mkono nikipapasa…… Hebu tuache hizi mambo lengo langu si kustusha ukuni wa msomaji hapa mnajua kilichotokea (kwakifupi nilikula mzigo tena).

Asubuhi mtoto hakuniomba hela ila haraka zangu na kujifanya niko vizuri nikakata laki nikampa. Hapa kwenye kuhonga wanaune huwa tuna tabia moja, huwa tunatoa kulingana na level ya dem na hali ya mfuko kwa wakati huo na asije mwanaume kukwambia kuwa hawezi kumpa mwanamke 50 kwa usiku mmoja nasisitiza hii huwa inategemea una nini mfukoni kwa wakati huo. Kuna wanaume wanahonga hadi milioni kwa gumegume (achana na dem wako unayemmiliki) maranyingi wanawake wanaofaidika na bahati hizi ni wale ambao hawana style za kuuza maana akishasema kulala 20 hatakama nna milioni siwezi kumpa zaidi sana naweza kumuongeza 10 ya nauli. Alafu kitu kingine wanaume huwa hatutoi siri ya jinsi tunavyohonga labda tukutane wanaume wenye tabia zinazofanana.

Mawazo huja zaidi binti akishaondoka pombe zikishakata, hapa ndio HESABU BAADA YA MATUMIZI huanza naamka nawaza nimetumia sh ngapi kwa usiku mmoja? Natoa suruali yangu na kuanza kutoa pesa kila mfuko, zinatoka buku buku, buku mbili, buku tano na buku teni chache tu zilizojikunjakunja kwakifupi jumla yake haifiki hata laki naanza kujiuliza “nimetumia laki9 jana!! Au niliibiwa hela?”. Naanza kupiga hesabu juu juu “nilipotoka kazini nilivuta mia8 ATM ya madini nikaenda MJ hotel, pale nilitumia chini ya laki” hesabu haziendi naamua kuweka hesabu ya juu basi nilitumia 80 nikaenda kuonana na P mitaa ya kati sikukaa sana inawezekana nilitumia 50 kwahiyo ushenzini nikifika pale nikiwa kama na 600 na sehem mfukoni, ziliishaje pale!? Wakati tunaondoka nilienda tena kutoa mia mbili ATM ya stand alafu asubuhi nimeamka na chenji tu . Naanza kuwaza hii laki tisa ningeongeza nguvu kwenye kamjengo kangu pale machakani si ningekuwa nimepiga hatua au basi ningekunywa hata laki mbili tu.

Kulingana na kipato changu kutumbua laki9 kwa siku au kwa wiki kwa starehe tu ni hatari sana, nimejua kosa langu sipangi bajeti kabla ya matumizi kulingana na kipato changu ila napiga hesabu baada ya kutumia . Hii haijanitokea kwa siku moja maranyingi nakunywa usiku nikiwa na furaha asubuhi naamka kupiga hesabu nilichotumia na kuwaza hadi kupelekea depression na hii sio kwangu tu nimeona kwa ma legendary wengi tu wazee wa kupiga hesabu asubuhi ndiomana na share nanyi kuwakumbusha.

Leo naandika uzi huu ni mwezi wa5 sijagusa pombe sijachezea hela nafanya mambo mengine, nimeona kabisa hela ilikuwa inatorokea wapi. Rafiki yangu mmoja ananiambia pombe haimalizi hela maana kwa wastani naweza kutumia si zaidi ya 50 tu kwa wakati nikanywa kawaida nikatosheka kwa bia zangu za elfu tatu tatu (achana na mapombe ya bei ya wale madem wa jana) lakini jibu langu ni hili; ni kweli hamsini inanitosha nikiwa naenda kunywa kabla na kulewa ( kabla ya rrraha kuanza) lakini nikishalewa mipango yote huvurugika

Sijaacha pombe nimepumzika tu sababu gambe hunipa raha sana ila najipanga nikirudi nisiwe mzee wa kupiga hesabu baada ya matumizi.

Nawakilisha
Sijaacha mstari.

Ila wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika.

Bata lazima aisee.
 
Mulemule mzee dahila aftermath hua simanzi sana, mi huwa natumia wiki nzima kurikava!

Unakuta ijumaa nina 200k,jmos nakurupuka na 25k na madusko dahh..ila raha sana
 
Daah huu uzi naosoma nikimwagilia moyo, ni full burdani yani!
Soon nabadilisha kiwanja, lakini lazima nipitie ATM nivute kama 300k hivi, muda kidogo kabla nilivuta 200k naona haitoshi!
 

Similar Discussions

91 Reactions
Reply
Back
Top Bottom