lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,147
- 33,299
Alikua akitembea huku akipepesuka njia nzima mida ya saa tatu usiku.
Alikua akiongea peke yake muda mwingi,lakini kila aliyekutana nae alimshirikisha furaha yake bila kujali anamshirikisha Nani.
Alipokutana na Mimi,simjui hanijui,sikumpuuza Kama wengine walivyokua wakimpuuza.
Maneneo aliyokua akiyarudiarudia kwa furaha ya kilevi, Ni haya.
"Aaah nitampigia kampeni Dar es salaam yote".
Nikamuuliza Nani?
Akajibu" tayari wameshampitisha nakwambia"
Nikamuuliza Tena wamempitisha Nani?
Akanijibu kwa kunifokea" si Lissu!"
Nikamuuliza,wewe utamchagua Lissu?akajibu,"Tayari nimeisha Anza kumpigia kampeni kwenye vilabu viwili na ninaenda kwingine,nitafanya hivi Dar es salaam yote."
Na huko nilikotoka wamenielewa na wamekubali kumpigia,na huko nakoenda watanikubalia tu kwa sababu wananijua Sana,najulikan a Sana.
Kwa Nini unajulikana?
Akaanza kufunguka.
Kaka yangu amekufa.
Kabla hajafa alikua na nyumba nzuri tu Kimara.
nyumba yake ya Kimara ilibomolewa hakulipwa,
Familia ikakosa mahala pa kuishi.
Akarudi nyumbani mke na watoto akaacha kwangu,Mimi nimepanga chumba kimoja cha kuishi na ninafanya kazi ya kutembeza mitumba.
Kaka alikua mfanyabiashara wa korosho,akanyang'anywa korosho zake huko Mtwara kwa sababu hakua na shamba.
Kaka yangu akachanganyikiwa kabisa,akaugua "stroku" Hadi mauti yakamkuta.
Mke wake yaani Shemeji yangu yeye naye aliachishwa kazi kwa sababu eti walimwambia Hana Cheti,wakati aliajiliwa na serikali hiyihiyo,Sasa Kama Hana cheti walimwajilije? Aliuza mlevi.
Baada ya kuachishwa kazi na mme wake kunyang'anywa korosho na kwa kuwa nyumba Yao ilibomolewa bila kulipwa, na yeye kufukuzwa kazi Shemeji yangu nae akaanza kuumwa "Stroku"na yeye kafa.
Sasa nimebaki Mimi na watoto wao wanne,wawili wameacha kusoma chuo,wawili nawasomesha mimi ila Shule waliokua wanasomeshwa na wazazi wao niliwatoa.
Maisha yangu yamekua magumu,Sasa nimeamua kulewa tu. Sina kazi,nilisomea ufundi wa mashine ( fitter Turner). Nimemaliza chuo 2014 nimetafuta kazi miaka mitano sijapata.nimeamua kutembeza mitumba na kulewa tu.nina mke na watoto wawili wangu na wa Kaka wanne,jumla Nina watoto sita.
Nitamchagua Lissu na nitampigia kampeni vilabu vyote Dar es salaam.
Vilabu vyote nilivyopitia kabla hajapitishwa na baada ya kupitishwa wanamkubali Lissu.
Nilimtia moyo nikampa Sha 10,000=,nikaondoka yangu
Hiyo ndio hali halisi huko mitaani.