Mlevi mmoja aapa kumpigia kampeni Lissu kwenye vilabu vyote vya pombe za kienyeji DSM nzima

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
2,878
2,000
Alikua akitembea huku akipepesuka njia nzima mida ya saa tatu usiku.

Alikua akiongea peke yake muda mwingi,lakini kila aliyekutana nae alimshirikisha furaha yake bila kujali anamshirikisha Nani.

Alipokutana na Mimi,simjui hanijui,sikumpuuza Kama wengine walivyokua wakimpuuza.

Maneneo aliyokua akiyarudiarudia kwa furaha ya kilevi, Ni haya.

"Aaah nitampigia kampeni Dar es salaam yote".

Nikamuuliza Nani?

Akajibu" tayari wameshampitisha nakwambia"

Nikamuuliza Tena wamempitisha Nani?
Akanijibu kwa kunifokea" si Lissu!"

Nikamuuliza,wewe utamchagua Lissu?akajibu,"Tayari nimeisha Anza kumpigia kampeni kwenye vilabu viwili na ninaenda kwingine,nitafanya hivi Dar es salaam yote."

Na huko nilikotoka wamenielewa na wamekubali kumpigia,na huko nakoenda watanikubalia tu kwa sababu wananijua Sana,najulikan a Sana.

Kwa Nini unajulikana?
Akaanza kufunguka.

Kaka yangu amekufa.
Kabla hajafa alikua na nyumba nzuri tu Kimara.
nyumba yake ya Kimara ilibomolewa hakulipwa,

Familia ikakosa mahala pa kuishi.

Akarudi nyumbani mke na watoto akaacha kwangu,Mimi nimepanga chumba kimoja cha kuishi na ninafanya kazi ya kutembeza mitumba.

Kaka alikua mfanyabiashara wa korosho,akanyang'anywa korosho zake huko Mtwara kwa sababu hakua na shamba.

Kaka yangu akachanganyikiwa kabisa,akaugua "stroku" Hadi mauti yakamkuta.

Mke wake yaani Shemeji yangu yeye naye aliachishwa kazi kwa sababu eti walimwambia Hana Cheti,wakati aliajiliwa na serikali hiyihiyo,Sasa Kama Hana cheti walimwajilije? Aliuza mlevi.

Baada ya kuachishwa kazi na mme wake kunyang'anywa korosho na kwa kuwa nyumba Yao ilibomolewa bila kulipwa, na yeye kufukuzwa kazi Shemeji yangu nae akaanza kuumwa "Stroku"na yeye kafa.

Sasa nimebaki Mimi na watoto wao wanne,wawili wameacha kusoma chuo,wawili nawasomesha mimi ila Shule waliokua wanasomeshwa na wazazi wao niliwatoa.

Maisha yangu yamekua magumu,Sasa nimeamua kulewa tu. Sina kazi,nilisomea ufundi wa mashine ( fitter Turner). Nimemaliza chuo 2014 nimetafuta kazi miaka mitano sijapata.nimeamua kutembeza mitumba na kulewa tu.nina mke na watoto wawili wangu na wa Kaka wanne,jumla Nina watoto sita.

Nitamchagua Lissu na nitampigia kampeni vilabu vyote Dar es salaam.
Vilabu vyote nilivyopitia kabla hajapitishwa na baada ya kupitishwa wanamkubali Lissu.
Nilimtia moyo nikampa Sha 10,000=,nikaondoka yangu
Hiyo ndio hali halisi huko mitaani.
 

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
2,878
2,000
Kweli Lissu ni wakuljnganishwa na walevi wasiojitambua kama huyo.
Hujasoma ukaelewa,huyo jamaa kaamua kulewa sababu ya changamoto alizopitia Tena za kusababishiwa.
Kapoteza Kaka kwa kunyang'anywa mahala pa kuishi (kubomolewa nyumba bila malipo) na kadhulumiwa korosho zake.
Kamaliza chuo Hana ajira,
Shemeji yake kafa kwa kuambiwa Hana cheti,

Yeye kaapa kumpigia Lisu kampeni kwa wanyonge wenzie.

Huko vilabuni pia Kuna wapiga Kura hata Magufuli anahitaji kura zao.
 

UCD

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
7,286
2,000
Hujasoma ukaelewa,huyo jamaa kaamua kulewa sababu ya changamoto alizopitia Tena za kusababishiwa.
Kapoteza Kaka kwa kunyang'anywa mahala pa kuishi (kubomolewa nyumba bila malipo) na kadhulumiwa korosho zake.
Kamaliza chuo Hana ajira,
Shemeji yake kafa kwa kuambiwa Hana cheti,

Yeye kaapa kumpigia Lisu kampeni kwa wanyonge wenzie.

Huko vilabuni pia Kuna wapiga Kura hata Magufuli anahitaji kura zao.
Huyo hajitambui kama wewe!
 

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
2,878
2,000
Kwa uongo tu mpo vizuri.
Thibitisha kua Ni uongo.
Sio kila mlevi ji mjinga.
Wengine wanansababu za kulewa tofauti Ni Aina za pombe tu.
Kuna wanaonywea pombe kwenye mahoteli,

Kuna wanaonywea pombe kwenye ma bar,
Kuna wanaonywea pombe majumbani,na

Kuna wanaonywea pombe kwe vilabu.
Hawa wote Ni Watanzania na wengi wamejiandikisha.
Subiri mziki wao.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,754
2,000
Threads zingine si tu kwamba zinakera na za Kipumbavu, lakini pia zinashusha sana Hadhi ya Mtandao huu pendwa wa JamiiForums. Tujitathmini.
 

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
2,878
2,000
Acha gahawa mzee.

Andika uhalisia.
Ulitaka kujua nguvu ya mlevi mwaga pombe yake.

Kwenye vilabu Kuna TV,
Wanaangalia Man U Kama unavyoangalia wewe huko huku ukiwa umekaa kwenye sofa.
Wanafuatilia Kila kitu,taarifa za habari zote walevi wanafuatilia,Sasa utawatisha Nini.
Subiri Kipyenga kipulizwe oktoba ili ujue Kama mlevi Ni chizi au mzima.
 

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
2,350
2,000
Ulitaka kujua nguvu ya mlevi mwaga pombe yake.

Kwenye vilabu Kuna TV,
Wanaangalia Man U Kama unavyoangalia wewe huko huku ukiwa umekaa kwenye sofa.
Wanafuatilia Kila kitu,taarifa za habari zote walevi wanafuatilia,Sasa utawatisha Nini.
Subiri Kipyenga kipulizwe oktoba ili ujue Kama mlevi Ni chizi au mzima.
Umeadika uongo mkuu.

Hio scenario haiko sawa. Ungeipanga vizuri ungeeleweka.
 

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
2,878
2,000
Threads zingine si tu kwamba zinakera na za Kipumbavu, lakini pia zinashusha sana Hadhi ya Mtandao huu pendwa wa JamiiForums. Tujitathmini.
Kuna TV moja ilikua inarusha kipindi fulani kinaitwa mtaa kwa mtaa,(USWAZI)huko pia tuliona watu Kama huyu mlevi niliyekutana nae.
Nisamehe kama habari hii haijakupendeza,lakini Hawa wa hivyo wako wengi Sana huku mitaani hasa uswahilini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom