mlemavu anney et anahatarisha amani ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mlemavu anney et anahatarisha amani ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kasyabone tall, Sep 18, 2009.

 1. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  UPELELEZI wa kesi inayomkabili mlemavu Anney Anney (58), ya kumkashifu Rais Jakaya Kikwete, umekamika na itaanza kusikilizwa kwa mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali, Septemba 30.
  Kesi hiyo ipo kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, chini ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wilayani hapo, Mrakibu wa Polisi, Naima Mwanga.
  Akiwasilisha ombi la kutaka kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi, Naima, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo aliiomba mahakama kupanga tarehe ya kuanza kusikilizwa.
  Hakimu Maweda alikubali ombi la mwendesha mashitaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 30 wakati mtuhumiwa ataendelea kubaki rumande kwa kukosa dhamana.
  Mshitakiwa huyo mkazi wa Arusha, anadaiwa kumkashifu Rais Kikwete, Julai 23, mwaka huu kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, kwa kuandika ujumbe kwenye bango, hali ambayo ingeweza kuhatarisha amani ya nchi.
  Mtu huyu alikuwa akitumia uhuru wake wa kufikisha ujumbe kwa rais, sijui kama rais analijua hili au ndio wapambe wamelivalia njuga kujipendekeza kwa rais. Mbona wale vijana walioandama na mabango ya kusema serikali ya kishikaji hawakuchukuliwa hatua? au kwa sababu ni wasomi wanajua sheria. tunaomba mashirika ya kutetea haki za binadamu tumtetee mlemavu huyu. eti anahatarisha amani ya nchi, mbona wengi wanatoa kauli za kuhatarisha amani ya nchi hawashitakiwi?, au sheria inachukua mkondo wake kwa mlemavu tu. hivi kipimo gani kinachotumiwa kupima kuhatarisha amani ya nchi au mtu yeyote asipopendezwa na ujumbe anapakazia kuatarisha amani ya nchi?
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Naona network haishiki vizuri hapa! Huo ujumbe kwenye bango ulikuwa unasemaji wakuu? aliandamana peke yake?
   
 3. S

  Simoni Member

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani huyu Bwana Anney mimi namfahamu vizuri. Majina yake kamili ni LEOPOLD ANNEY. Nimeshangaa kusoma kwenye magazeti eti huyu ni raia wa Iraq. Huyu kabila lake ni muiraqw (inatamkwa muiraku) ambao kwa jina lingine wanaitwa wambulu. Ni mzaliwa wa Karatu.

  Kama walivyo wenyeji wengi wa Karatu anapenda sana masuala ya siasa na ni mshabiki mkubwa san asana wa Dr Slaa na CHADEMA. Na Slaa analifahamu hilo, kwa nini haendi kumwekea dhamana yeye mwenyewe Slaa atajua. Bw. Anney ni mlemavu-kiwete ambaye hutumia baiskeli ya miguu mitatu. Mpiga maji mzuri sana. Sijui alikujaje pale Ikulu otherwise makazi yake yapo Arusha na hupendelea kukamata kinywaji pale Bar ya Mawenzi mjini kati.

  Sifa yake huyu bwana ni mbishi sana na haambiliki. Ndiyo maana character yake hii ikamfikisha mpaka milango ya Ikulu na mabango yake. Hata pale Arusha hupendelea sana kushabikia kesi na kujifanya anajua. Kiburi hiki sasa alifikiri kitampa fursa ya kurusha matusi yake.

   
Loading...