Mlango wa ajabu katika jumba la ibada ambao hakuna mtu aliyefanikiwa kuufngua

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,982
2,915
Kuna jumba la ibada huko India lijulikanalo kama Padmanabhaswamy ambalo kuta zake za nje zimetengenezwa kwa dhahabu. Jumba hili liko sehemu ijulikanayo kama Thiruvananthapuram katika Mji wa Kerala. Jumba hilif ni kati ya vivutio ya utalii ambapo utembelewa na watalii wengi kila mwaka. Lakini katika jumba hili kuna mali yenye thamani kubwa sana ambayo ilikuwa imefichwa kwa muda mrefu kwa karne na karne.

Jumba la ibada la Padmanabhaswamy ni mojawapo kati ya nyumba za ibada 108 wa Hindu zinazotumika katika kumwabudu mungu wao ajulikanaye kama Vishnu.

Jumba hili linalindwa na familia yenye damu ya kifalme ijulikanayo kama familia ya Travancore. Uamuzi wa kuweka jumba hili mikononi mwa familia hii ulifanyika mwaka 1729. TJumba hili na kila kilichomo kilikuwa kinamilikiwa na Padmanabhaswamy pamoja na hii familia ya kifalme niliyotaja hapo juu.
Lakini kuna mambo yalitokea na familia hiyo ya kifalme ikanyanganywa haki ya kuendelea kutunza jumba hilo, uamuzi huo ulifanya na mahakama kuu ya India. Hili jambo lilipelekea kugundulika kwa siri kubwa iliyokuwa imejificha kwenye jumba hilo ambalo limejengwa miaka mingi hata kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.
Mwaka 2011, jamaa ajulikanaye kama Sunder Rajan alifungua shitaka kwenye mahakama kuu ya india akidai kwamba familia ya Transcore iliyokuwa inalinda jumba hilo ilikuwa inatumia vibaya mali zilizokuwa kwenye jumba hilo. Wakati shauri hilo likiendelea, mahakama iliunda jopo la watu saba ambao walipewa kazi ya kuingia ndani ya jumba hilo na kukagua mali zote zilizomo ikiwemo pia nakala zozote zitakazokuwa zimehifadhiwa humo.

Jopo l;a watu hao saba, waligundua kuwa ndani ya jumba hilo kulikuwa na vyumba vya siri sita ambavyo, walihisi vitakuwa vina mali. Milango ya kuingia kwenye vyumba hivyo imetengenezwa kwa chuma ila haina na sehemu ya kuweka fungua, wala kofuri, wala bawaba, wala vitasa wala klitu chochote ambacho kingekufanya upate namba ya kuwaza jinsi ya kuufungua hiyo mlango.

Baada ya kufanikiwa kufungua milango hiyo kwa kutumia vifaa vya kisasa na muda mrefu, waligundua kuna mali yenye thamani ya dolla bilioni 22. Msomaji hii ni karibu tilion za Kitanzania 70, budget yetu ya miaka mitatu. Mali hii inajumuisha midori, shanga, mikufu, shilingi za pesa ya zamani sana, mabakuli, vifuu vya nazi vya dhahabu, dhahabu iliyotengenezwa kwa mfano wa mayai, almasi kubwa kubwa n.k
Pia kulikuwa na almas kubwa kubwa ambazo nyingine zilifikia karati 110, nadhani kwa wanaojua vipimo vya madini haya watakuwa wanaelewa. Wataalamu wa mambo ya kale wanakisia kwamba kimdori kidogo cha Vinshu kutoka katika hazina hiyo kinaweza kuwa na thamani ya dola milioni 30, karibia bilion 65 za Kibongo ndugu msomaji.

Wakati wakifungua vyumba hivyo vya siri walivipatia majina kwa herufi kuanzia Chuma A mpaka F kutokana na vilivyokuwa vimepangana. Sasa kimbembe ni kufungua mlango wa chumba B ilishindikana baada ya milango ya vyumba vyote kuwa imefunguliwa kasoro hiki chumba ambacho mlango wake ni wa tofauti kabisa na vile vingine na nje ya mlango kumewekwa onyo kuwa kuna ulinzi wa mijoka mikubwa.
Katika nakala walizokuta mle ndani zikiwa zinaonyesha mali zilikohifadhiwa, vile vyumba vingine viliandikwa kuwa vina mali lakini hiki chumba B hakijaorodheshwa kama chumba ambacho kimehifadhiwa mali, jambo linaloleta maswali mbona ndicho chumba chenye ulinzi mkali kuliko vyote.

Chumba hiki kina milango mitatu, mlango wa kwanza lilikuwa geti la grill la kawaida nyuma ya hilo geti kulikuwa na mlango mkubwa wa mbao walipofungua mlango wa mbao ndipo wakakutana na lango kubwa la chuma lisilokuwa na sehemu au kitu chochote cha kuashiria jinsi ya kuufungua. Pia juu yake likiwa na urembo mfano wa mijoka miwili aina ya cobra ambapo hii uashiria onyo kwa yeyote atakaye jaribu kufungua na kuingia katika chumba hicho kuwa atakutana na adhabu kali sana.
Tofauti na milango yavyumba vingine walau ilikuwa na bolts huu wa hiki chumba ni chuma kitupu hauna hata bolt hata moja.

Wahindu wao wanaamini kwamba juhudi zozote zitakazo fanyika kwa kutumia utaalamu wowote na kufanikiwa kufungua mlango wa chumba hicho, otapelekea janga kubwa ambalo linaweza kuteketeza mji mzima au India nzima pamoja na dunia kwa ujumla.

Tetesi nyingi zinazowahusu watu saba waliojaribu kufungua huo mlango zinasema kwamba waliugua wakati wanajaribu kuufungua, na mmoja wapo akiwa katika juhudi za kuufungua mama yake alifariki.
Pia jamaa aliyefungua shauri ambalo lilipelekea mahakama kutoa kibari cha kufungua jumba hilo bwana Sunder Rajan alifariki jambo ambalo wahindu wanalihusisha kama onyo kwa mtu yoyote anayetaka kufungua chumba hicho.

Hadithi za kale zinadai kwamba Marthanda Varma kutoka kwenye familia ya kifalme ya Travancore ndiye aliye jenga hivyo vyumba sita. Kati ya hivyo vyumba sita, chumba B kiliwekewa zindiko lilijumuisha mamia ya wazee wa Kihindu kutoka sehemu mbalimbali

Hadithi hizi zinadai ni kiongozi wa juu kabisa wa Kihindu ambaye anajua chanting inayojulikana kama Garuda Mantra ndiye anayeweza kufungua chumba hicho. I

Hadithi zingine zinadai kwamba hicho chumba kimeungana na sakafu zinazoshikiria bahari hivyo kikifunguliwa kitaruhusu bahari kumeza ardhi.

Haya ndiyo maajabu ya kale na huko India kuna maajabu mengi mfano wa mnara wa chuma ambao upo umesimama kwa mamia ya miaka na haujawahi kupata kutu, japo umetengenezwa kwa chuma ambacho kina mjumuiko wa madini mengine jambo ambalo hufanya chuma kupata kutu lakini mnara huu umesimama bila kupata kutu hadi wanasayansi wamekosa majibu.
21.jpg
22.jpg
 
Jina la jumba ya ibada na sehem lilipo vimenishinda kusoma, inataka kufanana na hadithi za kutafta hazina ya mjerumani sema hii ya india iko extra mile.
 
Wazungu nahisi nao walikuepo kwenye kufungua hapo maana hawa jamaa siyo poa
 
Waafrika ni zaidi ya balaa ila hawafatilii hivi vitu kwa undani. wamebaki kurudishana nyuma kimaendeleo na kuwangiana
 
Back
Top Bottom