Ml.Kili, Serengeti kuwa Kenya ni sababu za Kihistoria!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Najua hili swala litatoa wengi mapovu lkn potelea mbali nitalisema tu, kumekuwa na manun'guniko mengi sana kuhusu nchi ya Kenya na watu wake kutumia mambo ambayo yako nchini mwetu kujitangaza kwa mfano Ml. Kili wetu, au Mbuga ya Serengeti na inakwenda mbali zaidi hata Kiswahili Duniani kinajulikana kama ni Lugha ya Kenya, nilishawahi kwenda Ghana na huko nikaulizwa lugha yangu ni nini nikawaambia Kiswahili na wengi wakaniambia but Swahili is a language of Kenya nikajaribu kuwaelezea nikaleweka!

Sasa kwanini iko hivi? Sababu hasa ni za kihistoria na wala hazihusiani na Wakenya hivyo hamna haja ya kuwashambulia Wakenya, baada ya Wajerumani kushindwa vita walinyang'anywa nchi yetu na kupewa Waingereza ambao tayari walikuwa wanatawala Kenya na Uganda ambazo zilikuwa zinajulikana kama British East Afrika hivyo walivyopewa nchi yetu ambayo ilikuwa inaitwa Ujerumani ya Afrika Mashariki (detch ost Afrika) wakaibadilisha na kuiita Tanganyika jina lililotokana na Ziwa Tanganyika!

Sasa nchi ya Tanganyika ikaingizwa na kuwa sehemu ya British East Afrika chini ya Muingereza ambapo makao makuu ya British East Afrika yalikuwa Nairobi Kenya, yaani British East Afrika ilikuwa ni nchi moja chini ya mwamvuli wa British East Afrika hivyo basi Waingereza walitawala British East Afrika na kila kitu kilifanywa chini ya mwamvuli wa British East Afrika na hii ni kuanzia Utalii, Uchumi kama Viwanda, fedha, Usafiri n.k kwa mfano kwenye Utalii Waingereza walikuwa wanaitangaza British East Afrika kama one destination hivyo kama ni Ml.Kili ulikuwa uko British East Afrika, kama ni Serengeti ilikuwa iko British East Afrika kumbuka kwamba hapo mwanzo Wazungu wengi walikuwa wanafahamu kwamba Ml.Kili uko British East Afrika na British East Afrika ni Kenya na habari za Tanganyika kuingia zilikuwa hazijulikani!

Hivyo watalii ktk Ulaya na kwingineko walikuwa wakija kupanda Ml.Kili wanashukia Nairobi wanapita Loi tok tok wanapanda Ml.Kili baadaye wanarudi hivyo kwao wao Ml. Kili ulikuwa uko Britsh East Afrika!

Hivyo Uhuru ulivyopatikana tukaanzisha Jumuiya ya AM ambayo ilikuwa tu muendelezo wa British East Afrika hivyo hii Jumuiya ya Afrika Mashariki hatukuianzisha sisi bali ilkiwepo na ilianzishwa na Waingereza, hivyo kwa wageni nchi ya Tanganyika ni ngeni na hawaijui kwa maana Waingereza walikuwa wanalitangaza koloni lao la BEA ambapo baadae iliitwa Kenya hiyo ndiyo sababu ya watalii wengi wanafikiri kwamba haya mambo yote bado yako Kenya kwa sababu ni ukweli kwamba Waingereza walikuwa wanatangaza kama eneo moja na EA ulivyovunjika wengi bado wanadhania mabakia ya British East Afrika ni Kenya!

Hivyo kuwalaumu Wakenya ni kuwaonea kwa maana ukiangalia hakuna jipya kila tunachojaribu kufanya ni kwamba tunafufua tu kile kilichokuwepo tangu Ukoloni wa Waingereza kwa mfano single tourist VISA ilikuwepo tangu Mkoloni, single currency ilikuwepo tangu Mkoloni, single travel document ilikuwepo tangu Mkoloni, hata olduvai Gorge iligunduliwa na Dr.Leakey na ilijukana kwamba binadamu wa kwanza aliishi British East Afrika na siyo Tanganyika hivyo ndivyo Waingereza walivyotangaza!

Vile vile litawashangaza wengi lkn jina official la nchi yetu siyo TanZania bali ni EAT yaani East Afrika, Tanganyika/Tanzania hiyo ndiyo country code (EAT) na siyo TZ kama wengi tunavyodhania ina maana sisi Dunia inajua kwamba ni sehemu ya British East Afrika!

Hivyo sisi kama TZ tuna kazi ngumu sana ya kuweza kulibadilisha hilo kama hata kuna umuhimu na tuna uwezo wa kifedha wa kulifanya hilo ni swali gumu sana na kama ni la lazima kwetu , kwani cha muhimu ili mtalii apande Ml.Kili ni lazima aje kwetu!
 
Ukiwa CCM hata akili inageuka??Historia hiyo uliisoma wapi???

Duh kama hujui kitu uliza basi
 
Back
Top Bottom