Mkwawa hakujipiga risasi kama wajerumani walivyotusimulia, bali aliliwa na simba..

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Binafsi nimejipa utaratibu kuwa vitabu vinavyohusu uafrika na waafri sitavitilia mkazo sana vile vilivyoandikwa na wazungu bali vilivyoandikwa na Waafrika wenyewe! Mfano ukisoma historia ya Mkwawa iliyoandikwa na wazungu wanasema mkwawa alijiua kwakujipiga risasi,

Ukweli wa historia ya kiafrika wazungu waliona aibu kusema walimshindwa Mkwawa, Mkwawa hakujiua bali aliwatoroka wazungu na kuelekea Songea ambapo alifia milima ya Lukumbulu kwakuliwa na Simba baada ya kuugua akiwa milimani peke yake.

Ni rahisi sana Vijana wa leo kuwadharau wazee wanaokutana nao barabarani na kuwaona watu wasio na Elimu wakiaminishwa kuwa elimu ilianzia magharibi, Cha ajabu Ahmed Baba (1556-1627) karne ya 16 aliandika vitabu 60.Ni mingoni mwa wasomi wa Phd katika ufalme wa Mali.

Ni vizuri watu tuyasake maarifa kwakutumia maarifa, na kwakutokujua historia yetu Waafrika tumelidhika Bara letu la Afrika na yale machache tunayoyafahmu, tukidhani wazungu ndio wasomi wa mwanzo duniani kumbe wapo waliofanya mapinduzi makubwa katika Africa,ila wamefichwa na historia za kigeni zinazofundishwa mashuleni.

Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo mkubwa......Pamoja na kwamba 1927 Gavana Sir David Cameron kupiga marufuku mtu mweusi kukanyaga mjini (posta ya leo) hasa kwenye sherehe za wazungu ambazo zilikuwa maranyingi zinafanyikia ukumbi wao pale makao makuu ya NBC leo,

Gavana huyu aliwaundia chama cha kuratibu sherehe za weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu mateka wa vita vya kwanza vya dunia toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).

Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya)huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika pale ukumbi wa Anautoglo Mnazimmoja Dar es Salaam na Julius Nyerere akashinda kwa kishindi dhidi ya mpinzani wake Adulwahid Sykes. Mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU iliyokwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM ambacho kinalitafuna taifa leo..

Hili ndio chimbuko la AA, TAA, TANU na hii CCM.

Kwa undani zaidi soma kitabu cha ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, kwa ofa ya mwezi mtukufu

Ofa ni 50,000 tu, nunua kwa 0715865544 au 0755865544 kisha tuma majina yako na mahali ulipo. Nakulete bureeeee

FB_IMG_1557900517502.jpg
 
Waafrika hatukua na utaratibu wa kuandika vitabu hivyo tulirithishana historia kwa hadithi mfano mzuri ni wa kanda ya kaskazini machief na mamangi wanaenziwa hadi leo kwenye hadithi hivyo hakuna mzungu aliyeandika kitabu na kudanganya.
Natamani kujua wahehe wanasemaje juu ya huyu chifu isije ikawa hii ni chai kwani vijana wa ufipa ni kawaida yenu kutengeneza chai za aina mbalimbali kuwahadaa wananchi.
 
Leo nilikua kwenye ofisi flan..nilipaata wasaa wa kuona typewritter ya zamani sn nilituliza bongo yangu na kuangalia kwa makini jinsi gan binadamu Mungu alivyo mpa akili..nikichunguza naona waya nyingi lkn kila uki chapa ni waya mmoja unaenda gonga wino karatasi linasogea..
Ila mimi ni muumini waafrica kwa mwasisi Walter Rodney..lkn hawa white people they are smart..we africa thinking about Sex tu all the time..bongo zetu zina spendi kwenye kukata viunoo. Mara sijui Nandi ooh Gwajima ooh that is non sense..kizazi cha kina Chief Mkwawa chenyewe alinufaika kwa kuuza wafrica utumwani kwa waarabu katili.sisi tujitafakali sn wenzetu mda mwingi wanatumia bongo za kufikili ni jinsi gani watatengeneza machine ama mitambo ambayo ita saidia kuongeza kipato production kama kilimo uvuvi..
sasa mpaka sasa yote kumi mblack apate uongozi..just emergine toka tumepata uhuru kuna mapya...tunachukiana hatuaminiani..tabaka la wa babe na wanyonge lina achana saanaa
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom