Mkwara wa UVCCM ni wa kufundishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkwara wa UVCCM ni wa kufundishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaijabutege, Jan 24, 2011.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Upeo wa kufikiri wa viongozi wa CCM ni mdogo sana. Niliduwazwa na mkwara-mbuzi wa UVCCM wa kuwafokea 'Baba Dhao' na kujidai ni matakwa yao. Kwanza nikafikiri kuwa vijana wa CCM ni makini na wanataka kukinusuru chama chao. Lakini baadaye nikatafakari na kugundua kuwa ule ulikuwa ni usanii uliofadhiliwa na uongozi wa juu ya CCM ili kufikisha ujumbe kwa wale ambao 'Baba Dhao' wanaogopa kuwambia moja kwa moja ili kuepusha mpasuko zaidi.

  Kesho yake nikawa ninaongea na rafiki yangu juu ya hisia zangu. Rafiki yangu huyo akaniambia ni kweli vijana hawakuwa na ubavu wa kusema waliyoyasema. Akanijuza kuwa mwanae alikuwa ni mmojawapo katika kikao hicho na kuwa ni CCM ngazi za juu iliyowatuma ili kuona kama wanaweza kuwavuta vijana kurudishe imani yao kwa CCM. Alitanabaisha kuwa mapenzi yaliyooneshwa na vijana kwa CHADEMA katika uchaguzi mkuu uliopita ndio ulioipa CCM woga; na hivyo kuiamuru UVCCM ihakikishe, kufa na kupona, inavuta vijana kukipenda chama hicho.

  Nionavyo, la kuvunda halina ubani. Kila mwenye akili ya uchambuzi aligundua kuwa UVCCM waliandikiwa na wakubwa wao waongee waliyoyaongea,

  Ivumayo haidumu!
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tusubiri tuone baba zao wanalipa zile hela then ndo tuanze kuwahoji kujua ni sehemu ipi wamesimamia.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  walifanya vizuri waendelee wanaweza kufanikiwa!
   
 4. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Maigizo hayatawafikisha mbali. Tembo hatajifichaje kwenye msitu wa matembele? Wameonekana.
   
 5. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  2010 na kuendelea....? hatundanganyiki?
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hatudanganyiki na hatununuliki. Maana CCM wakishindwa kukudanganya, wanakununua.
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  I agree with you 1,000,000%.
   
Loading...