KXY
JF-Expert Member
- Dec 31, 2011
- 880
- 327
Katiba ya Zanzibar
28.(1) Kufuatana na Katiba hii mtu ataendelea kuwa Rais mpaka:
(a) Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais; au
(b) afariki wakati akiwa Rais; au
(c) hapo atapojiuzulu; au
(d) iwapo amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania; au
(e) kwa sababu yoyote nyengine ameacha kuwa
Kiongozi kwa mujibu wa vifungu vyengine vya Katiba
hii.
Nimeshangazwa sana na kipengele hiki cha katiba ya Zanzibar, hapa katiba haimlazimishi mtu kutoka madarakani. Angalia maneno afariki, atapojiuzulu, amechaguliwa, ameacha.
Kifungu cha pili
(2) Kufuatana na maelezo ya kijifungu (1) cha kifungu hiki,
Rais ataacha madaraka yake baada ya kumalizika miaka mitano
kuanzia tarehe, ambapo:
(a) kama yeye ni mtu ambaye ndiye mara ya kwanza
amechaguliwa kuwa Rais chini ya Katiba hii alipokula
kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais
Kifungu hiki kinatumika pale ambapo Rais mwingine anatakiwa aapishwe yani 1(a) hapo juu itatokea baada ya miaka mitano.
Mbaya zaidi katiba haizungumzii nini kifanyike endapo kiti cha Rais kuwa wazi baada ya ukomo wa madaraka(ina maana katiba hairuhusu hili kutokea)
33.(1) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kwa:
(a) kufariki; au
(b) kujiuzulu; au
(c) maradhi ya kimwili au kiakili; au
(d) sababu nyengine yoyote itakayomfanya Rais
kushindwa kutekeleza kazi za Rais,
watu wafuatao, kwa mujibu wa mpangilio, watashika nafasi hiyo:
(i) Makamo wa Pili wa Rais, au ikiwa hayupo;
(ii) Spika wa Baraza la Wawakilishi ambaye
anatoka katika chama anachotoka Rais na yeye
ikiwa hayupo;
(iii) Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Endapo katiba ya Jamhuri ingekua inafuatwa huko Zanzibar mambo yangekuwa rahisi. Inasema hv..
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kitakuwa ki wazi,
na uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
utafanyika ili kujaza nafasi hiyo kila mara litokeapo lolote kati ya
mambo yafuatayo.
(a) baada ya Baraza la Wawakilishi kuvunjwa;
........
Suala hili lingesimamiwa na vyombo vya kisheria na si vyama vya siasa.
Kila la heri wazanzibari!