Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Kama kweli gharama ndio chanzo cha mkwamo wa kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya, basi naishauri iwaombe wabunge wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wasitishwe sitting allowance zao kwa idadi ya vikao fulani na hela zitakazookolewa zielekezwe kugharimia upatikana wa katiba mpya.
Serikali itamke wazi ni fedha kiasi gani zinahitajika na Bunge liweze kujua ni jumla ya vikao vingapi vitahijika ili kukusanya kiwango kinachotakiwa.
Hata Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi nao kama wana posho ya aina hii(sitting allowance) nao wahusishwe katika mpango huu.
Au ikiwezekana serikali ianzishe tozo maalumu ya muda, kwa kupeleka mswada Bungeni kwa hati ya dharura, kwenye aina fulani za vinywaji kama Juice,pombe,maji ya kunywa,n.k na hela itakayokusanywa ielekelezwa kugharamia mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya.
Naamini mpaka sasa kila mtanzania ameshaona umuhimu wa katiba mpya hivyo tutakuwa tayari kuumia kwa muda ili mradi tupate hiyo katiba.
Serikali inaweza pia kutengeneza t-shirt zenye ujumbe kuhusu katiba mpya na wananchi watazinunua tu tena kwa wingi tu.
Ikiwezekana baadhi ya t-shirt hizo ziwe na picha ya viongozi wa vyama vya siasa na wanasiasa wengine maarufu hapa nchini na kuwacha wananchi wanunue t-shirt yenye picha ya kiongozi au mwanasiasa anaempenda lengo likiwa ni kukusanya fedha.
T-shirt zingine zinaweza kuwa na picha ya mzee Warioba au picha ya wajumbe wengine wa Tume ya mzee Warioba au zenye picha ya pamoja ya wajumbe wote wa Tume na hata t-shirt zenye picha ya mzee Kikwete alieridhia kuanzishwa kwa mchakato huu lakini muhimu t-shirt zote hizi ziwe na ujumbe kuhusu katiba mpya.
Wabunge,hasa wa upinzani,mnaweza nanyi kupeleka hoja binafsi Bungeni kiu ya jambo hili na si kusubiri serikali tu.
Tusidanganyane nchi kwa sasa hakuna gharama kubwa tunayolipa kama Taifa kwa kutokuwa na katiba mpya.
Tusiridhike na haya majibu hapa chini yaliyoyolewa na serikali leo bali tuchukua hatua kadri tunavyoweza
Rejea hapa;
Serikali: Mchakato wa Katiba Mpya una gharama kubwa! Kipaumbele cha Serikali ni kutoa huduma za jamii kwa Watanzania