Mkwamo Katiba Mpya: Kama tatizo ni gharama,serikali iwambo wabunge wakatwe sitting allowance zao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,987
144,318
Kama kweli gharama ndio chanzo cha mkwamo wa kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya, basi naishauri iwaombe wabunge wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wasitishwe sitting allowance zao kwa idadi ya vikao fulani na hela zitakazookolewa zielekezwe kugharimia upatikana wa katiba mpya.

Serikali itamke wazi ni fedha kiasi gani zinahitajika na Bunge liweze kujua ni jumla ya vikao vingapi vitahijika ili kukusanya kiwango kinachotakiwa.

Hata Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi nao kama wana posho ya aina hii(sitting allowance) nao wahusishwe katika mpango huu.

Au ikiwezekana serikali ianzishe tozo maalumu ya muda, kwa kupeleka mswada Bungeni kwa hati ya dharura, kwenye aina fulani za vinywaji kama Juice,pombe,maji ya kunywa,n.k na hela itakayokusanywa ielekelezwa kugharamia mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya.

Naamini mpaka sasa kila mtanzania ameshaona umuhimu wa katiba mpya hivyo tutakuwa tayari kuumia kwa muda ili mradi tupate hiyo katiba.

Serikali inaweza pia kutengeneza t-shirt zenye ujumbe kuhusu katiba mpya na wananchi watazinunua tu tena kwa wingi tu.

Ikiwezekana baadhi ya t-shirt hizo ziwe na picha ya viongozi wa vyama vya siasa na wanasiasa wengine maarufu hapa nchini na kuwacha wananchi wanunue t-shirt yenye picha ya kiongozi au mwanasiasa anaempenda lengo likiwa ni kukusanya fedha.

T-shirt zingine zinaweza kuwa na picha ya mzee Warioba au picha ya wajumbe wengine wa Tume ya mzee Warioba au zenye picha ya pamoja ya wajumbe wote wa Tume na hata t-shirt zenye picha ya mzee Kikwete alieridhia kuanzishwa kwa mchakato huu lakini muhimu t-shirt zote hizi ziwe na ujumbe kuhusu katiba mpya.

Wabunge,hasa wa upinzani,mnaweza nanyi kupeleka hoja binafsi Bungeni kiu ya jambo hili na si kusubiri serikali tu.

Tusidanganyane nchi kwa sasa hakuna gharama kubwa tunayolipa kama Taifa kwa kutokuwa na katiba mpya.

Tusiridhike na haya majibu hapa chini yaliyoyolewa na serikali leo bali tuchukua hatua kadri tunavyoweza

Rejea hapa;
Serikali: Mchakato wa Katiba Mpya una gharama kubwa! Kipaumbele cha Serikali ni kutoa huduma za jamii kwa Watanzania
 
wa kwanza ni huyu muigizaji rais wa wanyonge akatae kabisa mshahara........
 
Tunaona katiba ni gharama lakini hatujui kuwa katiba ya sasa inazuia mawazo mazuri ya walio nje ya mfumo wa sasa ambayo yangesaidia kuongeza mapato na kupunguza gharama mara mia zaidi ya hizi za kutengeneza katiba bora.
Asante sana Mbunge kwa kuuliza hili swali maana kuanzia sasa msimamo wa serikali ya awamu ya tano juu ya katiba umejulikana rasmi na historia imerekodiwa!
 
Kama kweli gharama ndio chanzo cha mkwamo wa kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya, basi naishauri iwaombe wabunge wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wasitishwe sitting allowance zao kwa idadi ya vikao fulani na hela zitakazookolewa zielekezwe kugharimia upatikana wa katiba mpya.

Serikali itamke wazi ni fedha kiasi gani zinahitajika na Bunge liweze kujua ni jumla ya vikao vingapi vitahijika ili kukusanya kiwango kinachotakiwa.

Hata Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi nao kama wana posho ya aina hii(sitting allowance) nao wahusishwe katika mpango huu.

Au ikiwezekana serikali ianzishe tozo maalumu ya muda, kwa kupeleka mswada Bungeni kwa hati ya dharura, kwenye aina fulani za vinywaji kama Juice,pombe,maji ya kunywa,n.k na hela itakayokusanywa ielekelezwa kugharamia mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya.

Naamini mpaka sasa kila mtanzania ameshaona umuhimu wa katiba mpya hivyo tutakuwa tayari kuumia kwa muda ili mradi tupate hiyo katiba.

Wabunge,hasa wa upinzani,mnaweza nanyi kupeleka hoja binafsi Bungeni kiu ya jambo hili na si kusubiri serikali tu.

Tusidanganyane nchi kwa sasa hakuna gharama kubwa tunayolipa kama Taifa kwa kutokuwa na katiba mpya.

Tusiridhike na haya majibu hapa chini yaliyoyolewa na serikali leo bali tuchukua hatua kadri tunavyoweza

Rejea hapa;
Serikali: Mchakato wa Katiba Mpya una gharama kubwa! Kipaumbele cha Serikali ni kutoa huduma za jamii kwa Watanzania
Hela walizotumia zilikuwa nyingi sana. Kwanini wasizirudishe ili tuanzie hapo?
 
Mwananchi alievunjiwa nyumba huku akiwa na zuio la mahakama hii kwake haiwezi kuwa gharama ila wewe ambae labda mpaka sasa hujaguswa unaweza ukaona ni ghrama.

Zamu yako inakuja.
Unasumbuka bure mkuu Katiba Mpya si kipaumbele kwa sasa mkishinda uchaguzi ujao basi anzisheni huo mchakato wa katiba mpya!
 
Mwananchi alievunjiwa nyumba huku akiwa na zuio la mahakama hii kwake haiwezi kuwa gharama ila wewe ambae labda mpaka sasa hujaguswa unaweza ukaona ni ghrama.

Zamu yako inakuja.
Hata wakiingia CDM watavunja nyumba tu. Tusidanganyane hapa. Kuna sehemu hakuna uwezekano wa kuweka barabara hata ya baiskeli ila watu wamejenga sio mchezo. Utafanyaje?
 
Ninaomba katiba mpya iweke kipengele cha kunyonga kwa wanaokiuka katiba ktk nafasi za urais
 
Katika vitu visivyotakiwa na viongozi waandamizi wa ccm ni katiba mpya. Hivyo zitatolewa sababu nyingi kuhakikisha hilo halitimii. Suala hili nalifananisha na suala la bunge live, zilitolewa sababu za gharama, wakajitokeza watu wakasema watalipia wakabadili kibao eti watu wafanye kazi. Lakini mwisho wa siku imefahamika ni hila tu kwani siku hizi mkulu hata akienda kufungua mradi wa milioni 2 anakuwa mubashara tena saa za kazi.
 
Tatizo la gharama ya kifedha haipo. Tatizo ni gharama ya kuwapa wananchi mamlaka yao ndani ya Katiba. Watawala hawatakubali hilo. It is very unfortunate. Wanasahau kuwa hayo "maendeleo" yanayoshughulikiwa sasa hayawezi kufanyika bila utawala bora. Na utawala bora hautakaa utokee bila Katiba bora.
 
Kumbuka bunge live ilikuwaje?Sababu iliyotolewa ilikuwa gharama za uendeshaji ni nyingi mno,lakini walipojitokeza watu na kusema kuwa watarusha wao kwa gharama zao wenyewe,heee! Sababu zikabadilika,na ikawa kuwa haitarushwa live kwasababu watanzania wataacha kufanya kazi na kuamua kufatilia bunge.NOTA BENE 1+1=11
 
wasilete sababu zao za kitoto, waseme gharama ni kiasi gani watu wapitishe mfuko....

tutaomba hata nchi jirani mbona tetemeko tuliombaa
 
Tatizo sio gharama, kama ni gharama watangaze waone wazungu wanaotutakia mema watakavyochangia, hivi mmelogwa na nani enyi watanzania mkakaa mkitegemea ccm Na serikali yake watakuleteeni katiba Mpya kote kwenye katiba Mpya watu waliziangaikia Na wengine wakaingia katika mashaka makubwa kwa ajili ya katiba sasa mkikaa Na maswali yenu ya hapo kwa hapo au ya nyongeza mkategemea katiba Mpya mtangoja sana, kwani katiba Mpya ni kupunguza mamlaka yao kwa 40% hapo bado uchaguzi, kwa hiyo hawawezi kukubali kwa hiali, mpaka Kazi ifanyike kweli,
 
maendeleo yanayokuja bila katiba ni sawa na kunywa ARV wakati huna virusi vya ukimwi

yaani hakuna kitu kama hicho duniani
 
Wananchi wapo tayari kuchanga km ni gharama,hii ishu ya katiba waliopo kwenye system wanaiona haina umuhimu wakati uwezo wanao Kwa sasa wakishakuwa nje ya system utasikia wanaiongelea kuishinikiza kama kuna baadhi yao walikuwa na nafasi hio kipindi hicho Leo wako nje ya system hawana nguvu wala Madaraka hapo ndo naposhangaa sasa walikuwa na nafasi ya kufanya mabadiliko hawakufanya wako nje ndo wanakumbuka.Ili suala La katiba mpya ni manufaa Kwa wote walio na Madaraka sasa na hata watakapokuwa nje madaraka japo wataelewa wakiwa nje.
 
Kumbuka bunge live ilikuwaje?Sababu iliyotolewa ilikuwa gharama za uendeshaji ni nyingi mno,lakini walipojitokeza watu na kusema kuwa watarusha wao kwa gharama zao wenyewe,heee! Sababu zikabadilika,na ikawa kuwa haitarushwa live kwasababu watanzania wataacha kufanya kazi na kuamua kufatilia bunge.NOTA BENE 1+1=11
Yes ila kwenye dhima au shughuli mbalimbali Mfano sherehe au uzinduzi vinarushwa live tena mda wa kazi ,Kwa bunge hapana ni mda wa Kazi watu wafanye Kazi ila mengine ruksa hawaangalii mda wa Kazi.
 
Back
Top Bottom