Mkuu wetu wa nchi anajitahidi sana kutafuta lakini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wetu wa nchi anajitahidi sana kutafuta lakini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Jun 2, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli Mkuu wetu wa nchi anajitahidi sana kutafuta wawekezaji toka nchi mbalimbali kuja kuwezeza Nchini Tanzania. haieleweki kikwazo nini. AKiwa nchini Brazil, mwezi Aprili, 2012 Mhe. Rais alitembelea na kuongea na Chama Cha wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchi hiyo,na kama kawaida walieleza maeneo ya vivutio lukuki vya uwekezaji, lakini ya furahisha ni hii ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza ndege na kuwaomba walisaidie shirika la ndege la Tanzania (ATC) kupata ndege mpya....(khaaa, mkuuu!!!, kivipi?)

  Hivi kwa nini tanzania panafaa kwa uwekizaji?

  (i) Kuna amani na utulivu

  (ii) kuna watu zaidi ya 40milioni

  (iii) Tanzania mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na bado majadiliano bado yanaendelea kuyafikia masoko ya kimataifa ikiwamo Marekani na nchi za Ulaya ambako tunapeleka kila kitu tunachozalisha isipokuwa Silaha.
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ukiona baba amefikia kuzunguka kijijini na kuwanadi mabinti zake kuwa ni wazuri wakarimu na hata wanajua mapenzi kwa hiyo vijana waje kuoa ujue kuna shida na si ndogo.
  dunia ni kijiji ukiweka mazingira mazuri hakuna haja ya kwenda ulaya kwa mabilioni ili kuwatangazia waje kuiba mali za uma.
  kila siku watanzania wanakimbilia china ni lini rais wa china alizunguka ulimwenguni kuwaambia waende china kununua bidhaa zao?
  hapa tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.
  mwalimu walimjia kwenye madini na kutaka kumpa15% akakataa leo mmeenda kuwaita wanawapa 3%
  hiyo akili matope?
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hata wao wanajiuliza hizo fursa anazotuambia kwa nini wananchi wake hawazitumii?
   
 4. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kamati ya akina Zitto walipambana wakapata hapo ka 1% zaidi kakawa 4%. mikataba imekaa kama green mamba, ukigusa tu unapigwa neuro toxic unahesabiwa dakika na unasahau kuamka milele!
  Ipo kazi hapa!
  hata demu ukimbembeleza sana lazima kuwe na 'attached strings". masharti kibao na lazima akupige changa la macho.
  both parties should have a win win situation, otherwise temena nayo. in JK situation, it is a win lose situation, and he thinks in terms of how many investors are in rather than what we get from our resources that are exploited.
  inasikitisha!
   
 5. n

  ndagabwene Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nafikiri kuna kila sababu ya kufanya mabadiliko katika secta ya uwekezaji na hata sheria zinazosimamia.mi sioni kama uwekezaji tatizo sana kwani kama rasilimali tunazo halafu tunashindwa kuzitumia kwa manufaa wa wenyenchi ni bora tuwape watu(wawekezaji)waziendeshe kwa kutulipa.tatizo kubwa sana katika nchi zetu za kiafrika hakuna uongozi bora na ndio mana wawekezaji wengi wanatuibia tunabaki tunawaangalia hakuna cha kuwafanya kutokana na sheria zetu za kikenge.
  kunasababu gani ya kuuziwa ndege ambazo zimetumika?kwani uwezo wa kununua mpya hatuna?mbona wenzetu wakenya wanaweza na rasilimali tumewazidi..............anyway someni waungwana kisha tafakarini kwani nikiwagusia wakenya naumia sana na kukosa uzalendo-wanachokifanya sasa hivi kwenye nchi hii na tunajivunia eti kuwa kwenye shirikisho la afrika mashariki wakati bado tunalaa tena usingizi kwelikweli-wasomaji wa gazeti la "Afrika mashariki"linalotoka kila jumamosi na kusambazwa jpili mtakubaliana nami(someni hili gazeti linalohusu habari za afrika mashariki kiuchumi,siasa,utamaduni na michezo).kama hatubadiliki kimtazamo,itikadi na kujishughulisha zaidi na shughuri za maendeleo-we will never change for the next 50 years and be slaves in our own land-working for our lovely neighbours.
   
 6. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,530
  Likes Received: 10,442
  Trophy Points: 280
  duh.! Inauma sana Mwalimu alikataa 15% sisi tumekubali 3%...mda mwingine ni bora ubaki gizani usijue nchi inavyoliwa na wenye meno tena kwa kubembelezwa na watawala wetu.!
   
 7. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima yako mkuu..we ni jembe
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana mwalimu alikuwa mzalendo namba1 ndio maana wakala njama za kummaliza!

  Then huyu cha nazi anahangaika tu..hajui hata afanye nini! Kwani wawekezaji ndio watakao shusha mfumuko wa bei? Na kuondoa shida zetu?
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Well said mkuu wala hujakosea hata nukta na hapo ndipo inatudhihirishia anasafiri kwakuwa anapenda sana kusafiri!
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwavile zipo mdomoni mwake tu na siyo in real sense
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Alafu watakuambia huyu mtu mwenye fikra kama hizo amesoma uchumi ninachojiuliza ni uchumi cheti ama uchumi maarifa!?
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nadhani tatizo ni la watz wote na siyo viongozi wake pekee, ukitaka kuamini je ni kwanini watz hawachoshwi na hali ya mambo ilivyo na kuikata kwa nguvu serikali iliyoboronga na kushindwa kuiongoza nchi badala ya chama tawala kukaa na kuangali ugumu wa maisha unaowakabili watz waliowapa dhamana badala yake ccm wameamua kukaa vikao wakijadili jinsi ya kuwaadhibu wabunge wa ccm walioonyesha uzalendo wa kumwajibisha waziri mkuu ambalo ni suala lilikuwa na maslahi kwa Taifa linalopoteza mwelekeo kwakuibiwa kila kukicha. Je hiki chama na serikali yake wana malengo gani na nchi yetu?
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndo tatizo la kuweka maslahi mbele!
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa anasafiri kwa kuwa anapenda kusafiri na sio kwenda kuwatafuta wawekezaji kwani watu wenye fedha zao wanapotafuta mahala pa kuwekeza sio lazima kuwabembeleza kwani wao wenyewe wanajua wapi wakiwekeza watapata faida; unapokwenda kuwabembeleza ndio hapo wanapokuwekea mashartu ya kukupa mrahaba wa 3% ambao haukusaidii kuwapa wananchi wako maisha bora!!Weka mazingira mazuri ya kuwekeza kwa wananchi wako ambao wanaweza kutafuta mitaji ama sivyo weke sheria ya kuwa wawekezaji lazima wawe wabia na wananchi na hapo nchi itafaidika badala ya kunyonywa!!
   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Amepita mpaka kwa wawekezaji wa kilimo cha nyanya...kule Iringa nyanya zinaoza kwa kukosa soko la uhakika, eti leo Mr. President anaenda kutafuta wawekezaji wa nyanya toka Brazil
   
Loading...