Mkuu wa Wilayam Bukombe, azuia maandamano ya Walimu

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Amani Mwenegoha amezuia maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Walimu wilayani hapa ambayo yalipangwa kufanyika leo alisema ni batili na hayana msingi wowote.

DC ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya amesema hoja zote 17 ambazo waliziorodhesha zilishajibiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kupitia barua yenye Kumb. Na. A.30/3/84 ya tarehe Mei 16, mwaka huu.

Mkuu wa wilaya amekitaka chama hicho kama hakikuridhishwa na majibu hayo wakutane tena na mkurugenzi kuzungumzia masuala hayo badala ya kufanya maandamano.

Amesema maandamano hayo yataathiri shughuli za mitihani ya “Mock” kwa kidato cha nne inayoendelea kati ya Mei 10 na Mei 20 mwaka huu na ile ya “STEP” chini ya BRN kwa shule za sekondari iliyoanza Mei 16 na kukamilika Mei 20, mwaka huu.

Alisema kamati ya ulinzi na usalama ipo imara kudhibiti maandamano hayo na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika Wilaya ya Bukombe.
 
Back
Top Bottom