Mkuu wa Wilaya ya Ubungo aagiza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akamatwe na polisi popote alipo

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669

Naangalia hapa AZAM TV,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh Kisare Makori,anasema ameamua kumkamata Meya wa Halmashauri ya Ubungo na kuagiza Polisi wamuweke ndani sababu amekiuka taratibu za kazi kwa kuwaleta wanachama wa CHADEMA wa kanda ya Pwani na kuwatembeza katika miradi ya maendeleo ya halmashauri.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ubungo,anasema kwa sheria na taratibu,wenye mamlaka ya kukagua miradi ya maendeleo ni wajumbe wa kamati ya Maendeleo wa Halmashauri chini ya Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri.Hivyo kitendo cha Meya kutembelea miradi ya maendeleo bila madiwani wa kamati husika ni kuvunja sheria,na dawa yake ni kukaa ndani na kufunguliwa mashtaka.

Ameagiza Sumaye na viongozi wengine wa CHADEMA kanda ya Pwani walioambatana na Meya,nao wasakwe na jeshi la Polisi na kutiwa ndani popote pale walipo,ili waweze kujibu ni kwanini walikuja kutembelea miradi ya maendeleo bila idhini ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo.

Mkuu wa Wilaya anasema kitendo cha Meya kutumia ukumbi na majengo ya halmashauri kukutana na viongozi wa CHADEMA ni kinyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma,hivyo ameagiza Meya huyo kukaa ndani kwa masaa 48 kabla ya kufunguliwa mashtaka,huku akisisitiza Sumaye na viongozi wengine wasakwe.

My Take:Hivi hapa juzi kati,Mwenyekiti wa "Chama Dume" akifanyia mkutano wa Chama chake Ikulu?Na akasema sbb chama chake ndio kina dola,ni kawaida kufanyia mkutano huko?Kama Meya naye ni kiongozi wa Chama,kuna shida gani akifanya kama alivyofanya mkuu!!?
 
Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    52.9 KB · Views: 139
View attachment 527204

Hivi hawa watu Magufuli kawatoa wapi? ni vijana lakini wana akili ya mwaka 47. Aibu kweli kweli.
 
"Maendeleo hayana chama". Siamini kama sasa ndio tumefika huku, hivi kweli mtu wa chama akitembelea mradi wa maendeleo ni kosa kweli? Kimantiki sijaona kosa liko wapi. Ifike sehemu viongozi wetu waongozwe na busara, na kuepuka kusababisha chuki zisizo na msingi wowote
 
Back
Top Bottom