Mkuu wa Wilaya ya Ubungo aagiza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akamatwe na polisi popote alipo

View attachment 527204
Naangalia hapa AZAM TV,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh Kisare Makori,anasema ameamua kumkamata Meya wa Halmashauri ya Ubungo na kuagiza Polisi wamuweke ndani sababu amekiuka taratibu za kazi kwa kuwaleta wanachama wa CHADEMA wa kanda ya Pwani na kuwatembeza katika miradi ya maendeleo ya halmashauri.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ubungo,anasema kwa sheria na taratibu,wenye mamlaka ya kukagua miradi ya maendeleo ni wajumbe wa kamati ya Maendeleo wa Halmashauri chini ya Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri.Hivyo kitendo cha Meya kutembelea miradi ya maendeleo bila madiwani wa kamati husika ni kuvunja sheria,na dawa yake ni kukaa ndani na kufunguliwa mashtaka.

Ameagiza Sumaye na viongozi wengine wa CHADEMA kanda ya Pwani walioambatana na Meya,nao wasakwe na jeshi la Polisi na kutiwa ndani popote pale walipo,ili waweze kujibu ni kwanini walikuja kutembelea miradi ya maendeleo bila idhini ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo.

Mkuu wa Wilaya anasema kitendo cha Meya kutumia ukumbi na majengo ya halmashauri kukutana na viongozi wa CHADEMA ni kinyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma,hivyo ameagiza Meya huyo kukaa ndani kwa masaa 48 kabla ya kufunguliwa mashtaka,huku akisisitiza Sumaye na viongozi wengine wasakwe.

My Take:Hivi hapa juzi kati,Mwenyekiti wa "Chama Dume" akifanyia mkutano wa Chama chake Ikulu?Na akasema sbb chama chake ndio kina dola,ni kawaida kufanyia mkutano huko?Kama Meya naye ni kiongozi wa Chama,kuna shida gani akifanya kama alivyofanya mkuu!!?
mimi nadhani chadema wenyewe wameyataka yote haya kwa maana wamewadekeza viongozi wa CCM kuufyata kwao bado kuna siku watahakikishwa wanaswekwa ndani kwa mwaka bila kuwaonyesha kwamba basi inatosha imekula kwao watadharilisha na vitoto visivyokuwa hata na tija kwa taifa hili
 
Kumbe tamko la Simbachawene kwa hawa ma DC lilikuwa halina maana yoyote.

Hii issue ilikuwa ifanywe na DAB lkn kwa kuwa yuko kwenye kifungo na adhabu kali ndo ametafutwa mburula mwingine
 
View attachment 527204
Naangalia hapa AZAM TV,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh Kisare Makori,anasema ameamua kumkamata Meya wa Halmashauri ya Ubungo na kuagiza Polisi wamuweke ndani sababu amekiuka taratibu za kazi kwa kuwaleta wanachama wa CHADEMA wa kanda ya Pwani na kuwatembeza katika miradi ya maendeleo ya halmashauri.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ubungo,anasema kwa sheria na taratibu,wenye mamlaka ya kukagua miradi ya maendeleo ni wajumbe wa kamati ya Maendeleo wa Halmashauri chini ya Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri.Hivyo kitendo cha Meya kutembelea miradi ya maendeleo bila madiwani wa kamati husika ni kuvunja sheria,na dawa yake ni kukaa ndani na kufunguliwa mashtaka.

Ameagiza Sumaye na viongozi wengine wa CHADEMA kanda ya Pwani walioambatana na Meya,nao wasakwe na jeshi la Polisi na kutiwa ndani popote pale walipo,ili waweze kujibu ni kwanini walikuja kutembelea miradi ya maendeleo bila idhini ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo.

Mkuu wa Wilaya anasema kitendo cha Meya kutumia ukumbi na majengo ya halmashauri kukutana na viongozi wa CHADEMA ni kinyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma,hivyo ameagiza Meya huyo kukaa ndani kwa masaa 48 kabla ya kufunguliwa mashtaka,huku akisisitiza Sumaye na viongozi wengine wasakwe.

My Take:Hivi hapa juzi kati,Mwenyekiti wa "Chama Dume" akifanyia mkutano wa Chama chake Ikulu?Na akasema sbb chama chake ndio kina dola,ni kawaida kufanyia mkutano huko?Kama Meya naye ni kiongozi wa Chama,kuna shida gani akifanya kama alivyofanya mkuu!!?
Last week Waziri Simbachawene aliwataka Dcs na RCS waachane na mambo ya show off. Sumaye analindwa na serikali sasa utasemaje akamatwe popote alipo?
 
Back
Top Bottom