Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro, atoa Wiki 2 kwa RUWASA kumaliza matatizo ya maji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
MTATIRO AIPA RUWASA WIKI MBILI

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro, ameipa Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) wilayani Tunduru na mkoani Ruvuma kuhakikisha imeanza upembuzi yakinifu ili kuanzisha mradi wa maji katika kijiji cha Msinji wilayani humo.

Mtatiro ametoa maelekezo hayo katika mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambazo zimo wiki ya 3 kati ya wiki 5 zilizopangwa.

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Msinji alimweleza DC Mtatiro kuwa mradi wa maji uliotumia mamia ya milioni za serikali hauna tija kwa sababu maji yake ni ya chumvi kali kupita kiasi jambo lililopelekea wananchi waususe.

Mradi huo uliojengwa miaka mitano iliyopita umethibitishwa na wataalamu wa maji safi na salama muwa haufai na siyo salama kwa matumizi ya wanadamu.

DC Mtatiro ameshangazwa na kitendo cha kuwepo mradi mkubwa wa maji uliotumia fedha nyingi sana huku maji yake yakiwa hayafai!

Wananchi wa Msinji wamemshukuru DC Mtatiro na kumtaka aendelee kusimamia utatuzi wa kero zao kwa wakati.

Ziara za DC Tunduru wilayani kwake, kutembelea vijiji kwa vijiji zinatarajiwa kukamilika Mei 06, 2021.

Idd Mohamed,
Tunduru.
IMG-20210501-WA0018.jpg
IMG-20210501-WA0020.jpg
IMG-20210501-WA0019.jpg
 
Back
Top Bottom