Mkuu wa Wilaya ya Temeke, chunguza kampuni ya Wachina inayojenga Mtaro Mkubwa wa Maji ya mvua

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,767
2,000
Nimekuona ukipambana na Wachina wanaojenga barabara ya Mwendokasi huko Mbagala , sasa Wachina wale wa Mwendokasi wana nafuu mno kuliko hawa wanaojenga mtaro wa maji ya mvua kuanzia kule kwenye kiwanda cha bia cha Serengeti, haifahamiki walipataje kazi kubwa hivi kwa viwango vyao duni walivyoonyesha (nitachunguza)

Wachina hawa kiukweli hawaiwezi kazi waliyopewa, hebu jaribu kupita kila mahali walikopitisha mtaro wao kuanzia Chang'ombe , TCC Club, njoo kwenye Maghorofa ya nyuma ya Takukuru Temeke, njoo Keko, pita ndani ya gereza la keko, nenda hadi Keko Mwanga ujionee hasara waliyoisababisha ikiwemo vifo, usimtume mtu nenda mwenyewe ujionee, hii kampuni imesababisha nyumba za watu kubomoka kwa ujinga wao wa kuchimba mashimo makubwa na kuyatelekeza, spidi yao hata konokono ana nafuu , urefu wa mita 100 wanajenga kwa miezi 4, hivi ndivyo mlivyowaelekeza?

Hivi sasa barabara ya kwenda Gereza la Keko imefungwa kwa zaidi ya wiki 1 kutokana na kuchimba shimo kubwa ambalo wamelitelekeza, Wafungwa na Mahabusu sasa wanapitishwa vichochoroni kwa vile wachina wanalindwa, huoni hii hatari? Nimejionea mwenyewe baada ya kutaabika kufika gerezani kumuona mahabusu ndugu yangu ambaye nilitaarifiwa kwamba anaumwa.

Hatari iliyo kwenye mradi huu ni kubwa kuliko maelezo yangu, hebu DC nenda kajionee mwenyewe.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
 

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,021
2,000
Umeandika kwa hisia Sana mkuu.hongera kwa kuiona hiyo adha. Naamini DC ameiona, lakini pia tunasubiri mrejesho wa ufuatiliaji wako juu ya hawa wachina. Naamini ndiyo tuta coment vizuri, pole pia kwa kuuguliwa na mahabusu wako mkuu. Sio mbaya ukituambia nn tena kilimsibu ndg yako mpaka amefika ngomeni?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom