Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Kuna mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Nasuro jirani na shule ya sekondari Islamic Kirinjiko ambapo mtu mmoja anayejiita mwekezaji aitwaye Isaya Malongoza alivamia kijiji hicho na kuzungusha uzio kuzunguka nyumba za wakaazi wa kijiji hicho ukubwa ekari 100 huku nyumba za wakazi wa kijiji hicho na maboma ya mifugo yao yakiwa ndani ya uzio huo.
Mwekezaji huyo pia ameharibu mazao ya wakazi wa kijiji hicho na kuwazuia kuendelea na shughuli za kilimo jambo ambalo limewaweka wakazi hao katika wakati mgumu.
mgogoro huo ambao unaonekana kulelewa na mkuu wa Wilaya same ulianza mwaka 2013 mpaka sasa haujapatiwa ufumbuzi pamoja na wakazi hao kuhusisha ofisi ya taasisi ya kuzuia Rushwa Wilaya ya Same.
Pamoja jitihada za Mkurugenzi wa Wilaya ya Same kutaka kutatua mgogoro huo lakini amekuwa akikwamishwa na Mkuu wa Wilaya.
Hivi sasa wakazi wa kijiji hicho wameandika barua kwa Mkuu wa mkoa ndugu Mecky Sadick lakini bado hawajajibiwa.
Wakazi hao sasa wanataka kumuona Waziri wa Ardhi ndugu William Lukuvi
Nitaambatanisha nakala za barua za mgogoro huu kwani niko huku kijijini sijapata Photo Copy.