Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amtandika makofi Mwenyekiti wa Mtaa

mzee wa giningi

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
519
336
DSC_0486.JPG

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri Amejikuta akimtandika makofi Mwenyekiti wa Mtaa wa Buguruni –Matalawe Emmanuel Ngelime mara baada ya kutokuwepo kwa maelewano baina ya viongozi hao wawili.

Mapema katika ziara ya kushtukiza ya mkuu huyo wa wilaya katika ofisi ya mtaa wa Buguruni Mjini Njombe kumeibuka hali ya Taharuki iliyomfanya mkuu wa wilaya kushindwa kuzuia hasira zake na kumtandika makofi mwenyekiti huyo.

Imebainika kuwa Mpaka sasa Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Emmanuel Ngelime Anatumikia kifungo cha Nje cha Mwaka Mmoja kwa kosa la kujaribu kumbaka mwanamke mmoja mtaani kwake.
Mara Kadhaa Mkuu huyo wa wilaya amesikika akimtaka Mwenyekiti huyo kutojihusisha na maswala ya kazi kama kiongozi wa mtaa lakini Mwenyekiti Huyo amekuwa akikaidi kwa kuendelea kufanya kazi ili hali amekosa sifa ya kuwa Mwenyekiti.

Ziara ya mkuu wa wilaya imefuatia mara baada ya kupewa taarifa za kuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo amehukumiwa kwa kifungo cha mwaka mmoja kwa madai ya kutaka kumwingilia kingono mwanamke mmoja mtaani hapo bila ridhaa yake .

Hata hivyo tafsiri ya sheria imeweka wazi kuwa kiongozi yeyote wa serikali atakae hukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita basi kisheria atakuwa amepoteza uhalali wa kuwa kiongozi katika nafasi yoyote kwa mujibu wa sheria.
 
Ningeenda kuzungumza na mababu matokeo yangepatikana baada ya siku chache. Head of state mwenyewe alitoa second chamce kwa watu kulipa kodi walizo kwepa

Angewakusanya na kuwatandika makofi angekuwa ametatua tatizo?
 
DSC_0486.JPG

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri Amejikuta akimtandika makofi Mwenyekiti wa Mtaa wa Buguruni –Matalawe Emmanuel Ngelime mara baada ya kutokuwepo kwa maelewano baina ya viongozi hao wawili.

Mapema katika ziara ya kushtukiza ya mkuu huyo wa wilaya katika ofisi ya mtaa wa Buguruni Mjini Njombe kumeibuka hali ya Taharuki iliyomfanya mkuu wa wilaya kushindwa kuzuia hasira zake na kumtandika makofi mwenyekiti huyo.

Imebainika kuwa Mpaka sasa Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Emmanuel Ngelime Anatumikia kifungo cha Nje cha Mwaka Mmoja kwa kosa la kujaribu kumbaka mwanamke mmoja mtaani kwake.
Mara Kadhaa Mkuu huyo wa wilaya amesikika akimtaka Mwenyekiti huyo kutojihusisha na maswala ya kazi kama kiongozi wa mtaa lakini Mwenyekiti Huyo amekuwa akikaidi kwa kuendelea kufanya kazi ili hali amekosa sifa ya kuwa Mwenyekiti.

Ziara ya mkuu wa wilaya imefuatia mara baada ya kupewa taarifa za kuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo amehukumiwa kwa kifungo cha mwaka mmoja kwa madai ya kutaka kumwingilia kingono mwanamke mmoja mtaani hapo bila ridhaa yake .

Hata hivyo tafsiri ya sheria imeweka wazi kuwa kiongozi yeyote wa serikali atakae hukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita basi kisheria atakuwa amepoteza uharali wa kuwa kiongozi katika nafasi yoyote kwa mujibu wa sheria.
 
Nimeipenda.....enzi za kikwete kumpiga raia kule mlangali jukwaani Ludewa. MTU alikula kofi pwaaa! Mbele ya wananchi...sijui alikuwa ni mkurugenzi yule....2009.

Naona njombe hakajawatoka kale katukio....mnazidi kukaenzi....safi sana
 
Hawana suluhisho la kutatua kero za wananchi, ndio maana wanatumia hasira kulazimisha mambo.
 
Tell me this's all lies... NO; BIG LIE!!! Sitaki kuamini! Na kama ni kweli kwanini dume zima anakubali kupigwa?! Simply because ni DC; au?!
 
Back
Top Bottom