Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Mkuu wa wilaya ya Mwanga Bw.Shayibu Ndemanga amesema, kuanzia sasa hatapeleka taarifa za kila wiki kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mpaka ajiridhishe baada ya kugundua amekuwa akipelekewa taarifa ambazo sio sahihi kwa miaka mitano iliyopita na kuidanganya Ikulu katika mipango ya maendeleo.
Bw.Ndeamanga ametoa tamko hilo wakati alipokutana na watendaji wa ngazi zote za Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga baada ya kumalizika kwa uhakiki wa watumishi hewa ambapo aligundua udanganyifu mkubwa katika kila sekta uliokuwa ukifanywa na halmashauri ya wilaya hiyo.
Amesema, inasikitisha kuona hata idadi ya mifugo wakiwemo Ng'ombe, Mbuzi na Kuku kwa miaka mitano hawaongezeki hata kupungua na sekta zingine vivyo hivyo takwimu zimekuwa hazilingani na hali halisi na kuonyesha wakuu hao wa idara wamekuwa wakikopi na kupesti taarifa zilizopita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw.Jamhuri William amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuwaonya watendaji wa chini yake kuwa makini kuanzia sasa na atakayekwenda kinyume atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Afisa Mtendaji wa Kata ya Msangeni Bi.Fabiana Msofe amesema, hali hiyo imetokana na tabia ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa mazoea na kujisahau kama wao ni watumishi wa umma.
Chanzo: ITV