Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Albert Msando apongezwa kwa utendaji kazi

Dec 7, 2020
10
1
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mhe. Albert Msando amepongezwa kwa utendaji kazi wake kuwa kwa kipindi kifupi umeleta mabadiliko mazuri kiutawala na hasa katika kuwaletea maendeleo wananchi na wakazi wa wilaya ya Morogoro Mjini.

Hayo yamezungumzwa na Waheshimiwa Madiwani katika kikao Cha Baraza la Madiwani cha kawaida kilichofanyika leo November 18,2021 katika ukumbu wa chifu kingalu uliopo mjini Morogoro.

Kwa upande wake Mstahiki meya kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Paschal Kihanga,alimshukuru sana kwa utendaji kazi wake ambapo kwa kipindi kifupi tuu tangu alipoteuliwa na kuwasili hapa Morogoro ameweza kuonyesha dira na mwelekeo mzuri sana katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Wilaya na Hasa kwa Manispaa ya Morogoro.

Hivyo amemuomba kuendelea kutenda kazi bila kukata tamaa wala kuogopa kwa niaba ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo anakusudia kuwatumikia watanzania wote.

Na

Hon. John Joseph
luhungo Morogoro.

Screenshot_20211118-163054_Instagram.jpg
 
Wazo lake la Kuwapanga wamachinga kwa vitendo alipojenga vile vibanda pale pembeni ya soko kuu limeleta matokeo chanya, na ndiyo maana mikoa mingine wamemuiga. Hongera zake
 
Tajeni hayo maendeleo aliyofanya kwa mda mfupi.Anasifiwa kwa kuwa yupo kwenye kiti,DC kuwa mskini na sifa hizo watakupiga kwenye hela ha uviko
 
Tajeni hayo maendeleo aliyifanya kwa mda mfupi.Anasifiwa kwa kuwa yupo kwenye kiti,DC kuwa mskini na sifa hizo watakupiga kwenye hela ha uviko
Mimi nipo Morogoro mjini na hayo maendeleo wanayo sasifia Hawa Mataga siyaoni. Sijui huyu Mataga mleta post anakaa Morogoro ipi? Au Kuna Morogoro mbili?
 
Back
Top Bottom