Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bi. Khadija awaweka ndani Wakuu wa Shule kwa kuchelewa kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa

MPARE KIBOGOYO

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
404
258
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga amewakamata na kuwaweka ndani wakuu wa shule 3 za sekondari kwa kuchelewa kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa. Wamewekwa ndani kuanzia tarehe 8/11/2021.

====

UPDATES:

====

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi.Khadija N. Ali, amekanusha taarifa hii kuhusu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Bi. Mwantum Mgonja kuwaweka ndani Walimu wakuu wanaozembea katika kusimamia Ujenzi wa madarasa.

Amesema yeye ndiye aliyeagiza walimu hao kukamatwa na sio Mkurugenzi
 
Safi. Kuchekeana kwenye miradi utavuna mabua.

Kufikia tar 15 dec nataka nchi nzima yaoteshwe madarasa.

Tar 16 mkeka wa rc, dc na wakurugenz utasomwa live TBC.
 
Hao walimu wamemwambia wana shida ya madarasa kwa sasa, kwa nini wasifanye kwa ratiba yao waliyojiwekea au ndo haraka ya kupiga zile 1.3t
 
Eeh mseme kwa nguvu jamani mkatuangushia zigo hilo.
Wanaonewa hao walimu,kwani wao ndio wameshika tends ya ujenzi.
Mwl amesomea ujenzi?
Watendaji wa kata na vijiji ndio wajibu wao
 
Wameonewa,hii nchi mtumishi anaenyanyaswa sana ni mwalimu.

Pesa ya ujenzi imetoka wiki 1 imepita,alafu watawala wanataka madarasa yakamilike ndani ya wiki 3.

Sasa hawa walimu walikosa muda wa kufunya maandalizi maana ujenzi wenyewe unakwenda kwa haraka sana,wawape muda walomu

Pesa zenyewe ni za misaada ya corona alafu mnakuja kuwanyanyasa walimu wetu.

Walimu wenyewe wala serikali haiwajali mishahara yao haijaongezwa kwa miaka 5 sasa,watu wanaishi na stress alafu mnawaweka ndani kwa mambo ya kijinga.
 
Back
Top Bottom