Mkuu wa Wilaya ya Mkalama amemfukuza kazi Afisa Afya wa Wilaya kwa makosa ya Ubadhirifu

Hawa wakuu wa wilaya wote ni pumba tu; Zero kabisa, ametumia sheria ipi? Nawashangaa hawa watumishi wanaochapwa viboko, kuswekwa rumande na hawa majuha then wanakaa kimya. Ni uoga au? Mtaonewa mpaka lini?

Eti, mkuu wa wilaya anasema "mtu atakayeugua kipindupindu atamsweka rumande!" Kweli? Hivi wanafikiri kufagia barabara juzi na kuokota makopo ndio njia ya kuzuia cholera? Mimi huwa sipendi kuonewa hata kidogo.

Safi sana Kiongozi! Matanzania majinga sana!
 
WAtu kama hawa ndio wanaitia hasara taifa.

Unaamka unamchap mwalimu fimbo, Mara kesho unawalazimisha unawapeleka watu lupango kisa wamefungua maduka wewe ulitaka wafagie wilaya, mwingine anazua likizo za watu.

Hivi vyeo kama wanashindwa kuelewa job discriptions zao vifutwe tu. tubaki na wakurugenzi.

Utaratibu wa kumshughulikia mla rushwa uko wazi
 
mtu kaiba amefukuzwa kazi mnaanza kumponda kweli ELIMU ELIMU ELIMU inahitajika
 
Jibu swali
Mkuu wa wilaya ana mamlaka ya kumfukuza mtumishi kazi?
Usiniite mkuu kama una akili za kibwege

Hebu mwambie huyo mtu.Kila kitu lazima kifanyike kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria za nchi.
Siyo mteuliwa fulani kujitwika mamlaka yasiyo yake na kufanya dhulma tu.Mpira pasi ili ulete magoli murua.Angempa mwenye mamlaka yake muajiri wa huyo mtumishi atimize uondoaji shaka wa mtuhumiwa.
Ikitokea mtuhumiwa ameonewa itakuwaje?Ukila ya mbuzi si kweli utaota mapembe....labda ya kufikirika tu.
 
mtu kaiba amefukuzwa kazi mnaanza kumponda kweli ELIMU ELIMU ELIMU inahitajika

Tatizo ni moja,mwenye mandate hiyo sio DC maana yupo kiasiasa zaidi...sisi tutajuaje kama anajitafutia umaarufu yeye n chama chake..kuna taratibu za kumfukuza Mtumishi kazi na zote hiz ziko chini ya DED,na anatangaza kumfukuza kazi ni DED baada ya vikao kadhaa na vingine vikihusisha madiwani na wote wajiridhishe ana kosa.sasa hili LA DC ndo tunashangaa...labda kama kuna sheria mpya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom