Mkuu wa Wilaya ya Mbozi atangaza kujiuzulu!

Nimemuona huyo jamaa kwenye habari TBC asubuhi.

Nika observe vitu vifuiatavyo, siku anaingia ofisini sidhani kama aliita waandishi na kuwaambia wananchi wake wategemee nini kutoka kwake. Na pia wakati anasoma tangazo kwamba amejiuzulu bado alikuwa amekaa ofisini kwenye ofisi za serikali sasa nimeshindwa kumuelewa kwa sababu barua ameionesha pale ambayo imeshakwenda kwa bosi wake.

Nadhani vyeo vya wakuu wa wilaya vitangazwe kama kazi nyingine wapewe wataalam kama PWC na wengine watafute watu wa kujaza hizo nafasi kitaaluma!
 
Wadau, nimesikia yasemavyo magazeti kuwa DC Mbozi aachia ngazi.Bahati mbaya niko mbali na mjini nashindwa kupata gazeti.Kuna mdau atakuwa na taarifa za kina ni kwa nini kaachia ngazi?

Source:Radio Wapo
Hii Habari iko humujavin toka jana jioni ,angali kwa makini kuna mada hiyo inaendela kuchangiwa na wadau.....
 
kwani haswa kazi ya mkuu wa wilaya ni ipi?? wilaya hiyo ina mbunge, mkutugenzi, katibu tawala mkuu wa wilaya na wengine kibao kazi zao zipi??

hana kazi yoyote kwa maslahi ya taifa,zaidi kuwa mjumbe wa kamati siasa ya wilaya CCM .mwache asepe wanatumalizia kodi zetu.:flypig:
 
huyu amebanwa ndo akaondoka, ulevi uliopindukia, pia rushwa za kijinga ndo umemponza. alichukua rushwa zaidi ya 20 m toka kampuni ya LIMA AKAWARUHUSU KUNUNUA KAHAWA BILA KIBALI, ASEPA KWENDA KUGOMBEA UBUNGE , HUKU NYUMA KIKANUKA, LIMA WAKAKAMATWA WAKAWEKWA RUMANDE WAKAMTAJA LIVE
 
huyu amebanwa ndo akaondoka, ulevi uliopindukia, pia rushwa za kijinga ndo umemponza. alichukua rushwa zaidi ya 20 m toka kampuni ya LIMA AKAWARUHUSU KUNUNUA KAHAWA BILA KIBALI, ASEPA KWENDA KUGOMBEA UBUNGE , HUKU NYUMA KIKANUKA, LIMA WAKAKAMATWA WAKAWEKWA RUMANDE WAKAMTAJA LIVE

Kinachonishangaza sana kwa nini habari hizi, ziwe za kweli au za uwongo, mnazitoa muda huu baada ya mweshimiwa kujiuzulu ? Kwa nini hamkushupalia ajiuzulu baada ya haya mliyosema hapa kutokea. Kamtido kenu kanaanza kuzoeleka maana tumeyaona kwa Millya wa Arusha.
 
Heheheheeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ukabila ndio mnatambuana? dah na sie mtasema wa wapi
Ila hongera wajina kwa uamuzi wako kama uliufanya ukiwa huna hasira au furaha iliyopitiliza kwa kuwa baadae huwa ni majuto
 
Wakuu mkuu wa wilaya ya Mbozi amejiuzulu nafasi yake, huyu alikuwa akipinga sana biashara ya kahawa ya maganda (coffee cherry) ambayo haiko kisheria lakini Maghembe alikuwa anairuhusu kwa manufaa ya wafanyabiashara wakati wakulima wakiendelea kudhoofika kiuchumi na mashamba kuendelea kufa.
Huyu mzee aliposikia Maghembe amefanya mambo yake kuwa hatakuwa mkuu wa wilaya tena ameamua kujiuzulu, na Kandoro amesema ni pre-emptive actions.
My Take. Je, huu ni uzalendo? Kwa kauli alitoa, ametuma ujumbe gani kwa JK?
 
Mwache aende kwanza anapengo jino moja halipo
Kwani kupungukiwa jino ndio akili? Muache ufala kama huwezi kuchangia soma tu inatosha,baba ritz ana meno na sura nzuri mbona kazi yake madudu tupu?
Wewe binafsi mbona una mapungufu mbona hujapewa ban humu jf?
Ukuu wa wilaya unahitaji ukweli na uwajibikaji huyu bwana anayo siri kubwa ya kilichojili na ni suala la muda tu na kitajulikana!
Yule mkuu wa wilaya aliyekataa kutukanwa kama mtoto na Lowasa mbona laana yake ilimpata lowassa na sasa tumemuelewa.
 
Jana kwenye tbc saa 2 usiku kandoro kamwaga povu lake.Kwamba jamaa aliambiwa hata kuwepo kwenye wateule wapya wa rais. Swali langu hivi siku hizi rais akitaka kumteua mtu wewe ambaye haupo una ambiwa?Au unafiki wa kandoro
 
i like the man.this is good political will, to step up or step down. alisema kiatu nilichokivaa ni kikubwa, mguu unapwaya... ha...ha...ha...!
 
kuna migogoro mikubwa inayoendelea Mbozi, moja ni hoja ya fidia ya wakulima wa kahawa ambayo hoja ya madai yake yaliyopelekwa kwa waziri mkuu na wawakilishi wa wakulima imepokonywa na Zambi na bado ameshindwa kutoa majibu kwa wakulima, nao wanamlia timing kubwa, akishindwa tu imekula kwake!
Mgogoro wa pili ni ule wa Biashara ya kahawa mbichi ambayo sheria za nchi inakataza na Kimoro amekuwa upande wa wakulima walioanzisha movement kupinga biashara hiyo baada ya kuona wakulima wanadhoofika kuichumi na mashamba mengi yamekufa. Huu ni mwanzo kwa Mbozi, yote amesababisha Maghembe
 
kama hatokei eneo la kwa Nkamia?
Ubunge unaweza kugombea sehemu yoyote Tanzania. Sio lazima atokee kwa nkamia hata kwa yule mwenzake wa kondoa mjini pale au sehemu yoyote tanzania. Lakini kondoa ilivyo nyuma kimaendeleo nina wasiwasi kama wana uongozi imara
 
Back
Top Bottom