Mkuu wa Wilaya ya Mbozi atangaza kujiuzulu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi atangaza kujiuzulu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elibon, May 4, 2012.

 1. E

  Elibon New Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa hii nimeipata kwa jamaa yangu,japo hajanipa sababu za kujiuzulu kwake,so kama kuna mtu ana habari kamili atumwagie hapa.

  NAWASILISHA!!!

  ============

  Kwa mujibu wa Bw. Kimolo, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kitendo cha yeye kukashifiwa na baadhi ya wafanyibiashara wanunuzi wa kahawa Wilayani hapo, ambao walifikia hatua ya kumtamkia kuwa hawawezi kuongea na "mbwa, bali na mfuga mbwa", wakimaanisha hawawezi kuongea naye bali Waziri Maghembe ambaye inadaiwa alikuwa akiwakumbatia.

  "Nimechoshwa na kejeli na mizengwe dhidi ya serikali. Wafanyibiashara wanadiriki kusema kuwa hawako tayari kuzungumza na mbwa bali wanazungumza na mwenye mbwa. Siwezi kufanya kazi katika mazingira ya aina hii. Wananchi waelewe hivyo. Nitabakia kuwa raia mwema na mwananchi wa kawaida kama wengine" alisema Bw. Kimolo.

  Kimolo, ambaye anakuwa kiongozi wa kwanza wa Wilaya kuachia ngazi katika kipindi cha miaka 20, ya utawala wa CCM, amesema kuwa amekuwa akikosa Ushirikiano na Wizara ya Kilimo kwa ujumla juu ya msimamo wake wa kupinga ununuzi wa kahawa mbivu (Red Cherry), kama ambavyo imekuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyibiashara wanaopata ridhaa toka Wizarani.

  Januari 7 mwaka huu, Waziri Maghembe, alikutana na baadhi ya wakulima na wadau wa zao la kahawa ambapo msimamo wa Serikali ulieleza kuwa hawako tayari kuendelea kuwaona wakulima wakiuza kahawa mbichi kwa wachuuzi hao hali ambayo Bw. Kimolo amesema ilisababisha yeye kuonekana kutothaminiwa msimamo wake na Serikali ya Wilaya na ya Mkoa.

  Kadhalika katika maelezo yake ya kujiuzulu, amesema kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa uteuzi unaofanywa na Rais, yeye uteuzi wake ulianza mwaka 2006, na kukoma mwaka 2010 ambapo hadi sasa hakuna uteuzi mpya uliofanywa na Rais jambo ambalo linamfanya ashindwe kupanga mikakati ya kazi kwa maendeleo ya Wilaya yake.

  Amesema kuwa, hivi sasa ni mwaka mmoja na nusu amekuwa akifanya kazi kwa matukio ya dharura na maagizo toka juu na hivyo kumfanya aonekane kutowajibika vilivyo katika nafasi yake na kwamba ameamua kujiuzulu akiamini kuwa uamuzi wake utalinda heshima yake.

  Aidha, inaelezwa kuwa Bw. Kimolo amekuwa ni mtu wa karibu sana na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na kwamba kitendo chake cha kujiuzulu kina baraka kutoka kwa kiongozi huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kablda ya kujiuzulu, ambapo katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni Wilayani Momba katika mji mdogo wa Tunduma, aliteta naye jambo muhimu.

  Hata hivyo, tetesi za kutokuwemo katika uteuzi ujao zinaelezwa kuwa ni moja ya sababu zinazomfanya mkuu huyi kuachia ngazi mapema ili kujijengea mazingira ya maandalizi ya kuikubali hali hiyo kabla haijatokea wakati wa uteuzi ambao unatarajiwa kufanywa na Rais wakati wowote kuanzia sasa.

  Akasema kumekuwa na baadhi ya viongozi wababaishaji na kusababisha serikali ionekane inashindwa kuwatumikia vyema wananchi na sasa yeye ameamua kuachia ngazi na anakwenda kushughulika na mambo yake binafsi.

  Alipotakiwa kueleza kama dhamira yake imejikita zaidi katika siasa, amesema kuwa wakati ukifika kuingia katika mchakato wa kisiasa atafanya hivyo kwakuwa yeye kama mtu yeyote ana uamuzi wake na katiba inamruhusu kufanya hivyo.

  Amesema kuwa, tayari amemuandikia barua Rais, Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuwajulisha hilo na kwamba huo ni uamuzi wake binafsi na jibu lolote halitabadili uamuzi wake huo.
   
 2. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kuna taarifa kutoka Mboz zina onyesha kuwa Kuna mgogoro Mkubwa Hapo Mbeya Kiasi cha DC kuachia Ngazi!!!
   
 3. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  [h=2]Friday, May 4, 2012[/h] [h=3]BREAKING NEWSSSSSS......DC MBOZI MBEYA AACHIA NGAZI[/h]
  TETESI zilizoufikia zimeeleza kuwa Mkuu wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya Gabriel Kimoro ameachia nafasi ya ukuu wa wilaya kwasababu ya Serikali kushindwa kuwawajibisha baadhi ya watumishi ambao amedai kuwa si waaminifu.  Imeelezwa kuwa ametoa msimamo huo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika ukumbi wa Beaco jioni ya leo uliopo Jijini Mbeya.  JK ANA KAZI.....

   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,895
  Trophy Points: 280
  Karibu CDM mh DC
   
 5. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  karibu kwetu kuzuri CHADEMA
   
 6. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kaamua kuvua gamba huyu anaonyesha kuwa ni mzalendo wa kweli.Majina ya Kimolo ni wenyeji wa kondoa tunamkaribisha kwenye ukombozi avae gwanda akamng'oe nkamia.
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tujuzeeni
   
 8. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hapo Mbozi kuna mgogoro wa Kahawa Mbichi ambapo DC ALIKUWA MUHUSIKA MKUBWA NA MFANYABIASHARA KWA SIRI111111111111
   
 9. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Nampongeza kama hakutaka watumishi wabovu
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kama hatokei eneo la kwa Nkamia?
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Labda alidhani atateuliwa ubunge then uwaziri so amekasirika amemwaga manyangaa,ngoja niiende vwawa.
   
 12. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Au naye anajivua gamba?
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Safi sana DC njoo CDM hao magamba wanabebana tu.
   
 14. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikweli kajiuzuru.safi sana magamba yakome ukandamizaji.
   
 15. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  kwani haswa kazi ya mkuu wa wilaya ni ipi?? wilaya hiyo ina mbunge, mkutugenzi, katibu tawala mkuu wa wilaya na wengine kibao kazi zao zipi??
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  au naye kajiunga na chadema nini?
   
 17. n

  ntawila New Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza hao wakuu wa Wilaya hawana kazi, Kama kweli kajihuzulu tutaipata taarifa rasmi
   
 18. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  m4c is working,kaogopa dhoruba na kimbunga.
   
 19. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mbeya yetu blog imepokea taarifa muda mchache ulio pita kuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Gabriel Kimolo ametangaza kujiuzulu, mpaka tunaleta tukio live hapa bado hajasema sababu za yeye kufanya hivyo..

  Taarifa kamili inakuja endelea kufuatilia.

  Source: Mbeya yetu blog.
   
 20. S

  SURA SIO SOHO Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kateuliwa mbatia
   
Loading...