Mkuu wa Wilaya ya Ludewa ataka wanaokataa na kufunga ndoa na kuishi bila ndoa wapelekwe lupango

Ni sawa na kusema mochwari imejengea ili walale maiti, watu wasipokufa ni hasara kwa serikali kwa hiyo ua watu waende mochwari.
Hao ndo viongozi wanaongoza waafrika, matako tu. Kazi ipo sana aisee
 
Kakosa kazi za kufanya. Kwa hiyo wanaofunga ndoa hawaachani? Wakati mwingine wawe wanapikwa kwanza kabla ya kupewa madaraka makubwa, ambayo wengi wa wao katika kauli zao wanapwaya sana.
 
Pamoja hakuna sheria kama hyo ila naafiki wazo lake. Watu wanazaa kama kuku hlf wanatelekeza familia zao. He has a point watoto kukosa malezi ya both parents. Mwanaume mmoja anazaa na wanawake watatu na wote anawatelekeza hataki kuwahudumia. 10- 15 years to come hasara yake itaonekana.
Sababu za watoto wa mtaani zipo nyingi: vifo vya wazazi, mifarakano katika ndoa, na hali duni za maisha ya baadhi ya wanandoa. Sasa iweje, huyu kiumbe asisitize kwamba ndoa ndiyo mwarobaini wa watoto wa mtaani? Kwa hili kapwaya sana, ingeli kuwa vema kama angeli kaa kimya.
 
naona magufuli vibaraka wako bado kuanza kutembea uchi tu, maana mengine yote wamesha yafanya bado kuchojoa tu! mwingine kakataza watu kusali.
 
Naona Mpaka hapa unaweza Kuelewa kuwa tuna Utawala wa hovyo awamu hii Kuwahi Kutokea. Mnabaki Kuimba Mapambio tu. Wakina Joketi sijui wameolewa na nani? Ukiwemo wewe Demu.

Ya kuelewa utajiju na akili yako utakavyo

Nimeolewa na mume wangu..😀
 
Msaada kwa anayejua JD ya wakuu wa wilaya naomba anijulishe tafadhali.
Unauliza Job Description? Ndio kama hizo. Kutoa tamko lolote wakati wowote popote anapojisikia. Na kuchapa wanafunzi. Na kusema jangili akikamatwa badala ya kupelekwa mahakamani apigwe risasi hapo hapo. Na kuweka viongozi wa upinzani ndani. Na jambo lingine lolote mkuu kama huyo anayeamua kufanya ili mradi anaitwa ni kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa eneo lake. Ndio Tz "Mpya" hii. Kama huwezi "kwenda na kasi yake" achia ngazi. Naamini umeelewa sasa.
 
Asubiri mpaka waachane ndio awashitaki. La sivyo labda mahakama as ccm ndio zitasikiliza kesi ya kijinga kama ya mkuu wa Wilaya.
 
Back
Top Bottom