Mkuu wa Wilaya ya Ludewa ataka wanaokataa na kufunga ndoa na kuishi bila ndoa wapelekwe lupango

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsele ameagiza watu wanaoishi bila kufunga ndoa kupelekwa mahabusu kwa kuwa watu wamekuwa wakiishi kwa muda mfupi na kupata watoto na kuachana huku wakisababisha watoto wa mitaani.

Akiwa katika Kongamano la Wanaume lenye lengo la Kupinga Mila potofu amesema watu wasiofunga ndoa wanaongeza watoto wa mtaani kwani wanakaa, wanazaa na mwisho wa siku wanaachana na kuacha Watoto wa mtaani

Amesema “Hizi ‘Lock Up’ zimetengenezwa kwa ajili ya nini? Wahalifu kama hao. Huyo ni Mualifu. Na kwenda ‘lock Up’ ni kawaida tu kwani lile ni jengo na ni la Serikali limejengwa litumike, likilala bila mtu ni hasara. Matumizi mabaya ya pesa ya Umma.”

Aidha, amebainisha “Ukishakuwa na ndoa na iheshimiwe, kuwa kwenye ndoa maana yake wote ni sawa. Kuwa kichwa cha nyumba haimaanishi hauwajibiki kuleta chakula, kwenda shamba, kutunza watoto na mke au kuleta nguo za mama na watoto nyumbani.”

Amesisitiza “Kuwa kichwa maana yake Watoto wapate chakula, waende shule na uwalipie wapate chakula shuleni. Pia ununue sare za Watoto za shule.”
 
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsele ameagiza watu wanaoishi bila kufunga ndoa kupelekwa mahabusu kwa kuwa watu wamekuwa wakiishi kwa muda mfupi na kupata watoto na kuachana huku wakisababisha watoto wa mitaani.

Akiwa katika Kongamano la Wanaume lenye lengo la Kupinga Mila potofu amesema watu wasiofunga ndoa wanaongeza watoto wa mtaani kwani wanakaa, wanazaa na mwisho wa siku wanaachana na kuacha Watoto wa mtaani

Amesema “Hizi ‘Lock Up’ zimetengenezwa kwa ajili ya nini? Wahalifu kama hao. Huyo ni Mwalifu. Na kwenda ‘lock Up’ ni kawaida tu kwani lile ni jengo na ni la Serikali limejengwa litumike, likilala bila mtu ni hasara. Matumizi mabaya ya pesa ya Umma.”

Aidha, amebinisha “Ukishakuwa na ndoa na iheshimiwe, kuwa kwenye ndoa maana yake wote ni sawa. Kuwa kichwa cha nyumba haimaanishi hauwajibiki kuleta chakula, kwenda shamba, kutunza watoto na mke au kuleta nguo za mama na watoto nyumbani.”

Amesisitiza “Kuwa kichwa maana yake Watoto wapate chakula, waende shule na uwalipie wapate chakula shuleni. Pia ununue sare za Watoto za shule.”
Kwa sheria ipi?
 
Bure kabisa huyu mkuu wa wilaya,ningependa kujua kiwango chake cha elimu,Mimi mwalimu wa urai hii topic ya ndoa iko kidato cha kwanza ,na maana ya ndoa (_marriage) inasema " is the voluntary (HIARI)union between a man and a woman , ANadhani hata waliofunga ndoa ikiwa uhiari utakosekana kati yao kuna ndoa hapo?
 
Msaada kwa anayejua JD ya wakuu wa wilaya naomba anijulishe tafadhali.
 
Ndiyo maana tunaitamani Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ipitishwe kama ilivyo, na kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili tuepukane na hii katiba mbovu na iliyopitwa na wakati ya ccm ya mwaka 1977.
 
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsele ameagiza watu wanaoishi bila kufunga ndoa kupelekwa mahabusu kwa kuwa watu wamekuwa wakiishi
...

Kabla hatujachangia tuweke Heading vema binafsi sijaielewa
Screenshot_2019-10-28-19-45-02-1.png
 
Yule wa Mbeya nae aoe yeye wanawake wote wa mbeya ambao hawajaolewa sio kulazimishana kama watoto
True yeye na wa Mbeya nadhani kuondoa tatizo hilo wangewaowa wanawake wote hili lingesaidia sana kupunguza wasioelewa
 
Kweli kuna Wendawazimu wengi mno! Lakini binafsi namlaumu baba Yao Jiwe maana huu Upuuzi aliuanzisha Nyamitako na yeye jiwe hajamkanya kuwa Aachana na Upuuzi huo maana unaivua Nguo Serikali yake.
Badala yake, anazidi Kumpa Maujiko.
 
Ndiyo maana tunaitamani Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ipitishwe kama ilivyo, na kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili tuepukane na hii katiba mbovu na iliyopitwa na wakati ya ccm ya mwaka 1977.

Ni katiba ya chama kimoja kwa sasa haiwezi to a majibu kwa hali ya sasa
 
Tamko lingine... 😃😃😃
Mashindano yanaendelea..
Duh!!!!

Hawa viongozi....mmmmmhhhhhh!!!
Naona Mpaka hapa unaweza Kuelewa kuwa tuna Utawala wa hovyo awamu hii Kuwahi Kutokea. Mnabaki Kuimba Mapambio tu. Wakina Joketi sijui wameolewa na nani? Ukiwemo wewe Demu.
 
Pamoja hakuna sheria kama hyo ila naafiki wazo lake. Watu wanazaa kama kuku hlf wanatelekeza familia zao. He has a point watoto kukosa malezi ya both parents. Mwanaume mmoja anazaa na wanawake watatu na wote anawatelekeza hataki kuwahudumia. 10- 15 years to come hasara yake itaonekana.
 
Back
Top Bottom