Mkuu wa Wilaya ya Kyela, fidia ya majengo yaliyopo pembezoni mwa barabara ya Kyela Mjini - Junction hakuna uwazi

Mzinguzi

New Member
Feb 15, 2017
3
3
Sisi wananchi wa pembezoni mwa barabara ya Kyela - Junction tunauliza habari ya fidia imefikia wapi?

Watu wa TANROADS wanapitapita huku kuomba omba fedha kwa wananchi kwa mtu anayetaka malipo mazuri, malipo mmefanya Siri wahusika hatujui tunachopaswa kufidiwa mnakaribisha Rushwa na utapeli.

Bandikeni majina ya watakaofidiwa na watafidiwa kiasi gani. Meneja wa TANROADS mkoa wa Mbeya amekuwa mbogo akiulizwa na wananchi kuhusu fidia hiyo, DC Kyela na RC Mbeya elekezeni macho yenu huko kuna wizi unaendelea.
 
Kama kuna chochote wapeni mpewe vyenu mapema, unakuta mwenzako ana nyumba ya thamani ni lazima wakaipemepime
sasa mwingine ana kiwanja tupu hata hakina Hati wala Offer anadai mazao ya muda km mtama naye alipe (hapo TANROAD wanasubiri avune tu wamuondoe).

Mambo yote siku hizi ni utaratibu na kifuta jasho.
 
Vipi gogodo naye atapewa bei gani pale kwaje, nyumba za Zaire nazo vipi vipi chimbo langu la Junction lodge litaondoka.
 
Back
Top Bottom