Mkuu Wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Mhandisi Tumain Magesa ametoa saa 24 kwa uongozi wa Kijiji cha Ndirigishi kuonyesha ramani ya Kijiji ilipo

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
450
225
Mkuu Wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Mhandisi Tumain Magesa ametoa saa 24 kwa uongozi wa Kijiji cha Ndirigishi kuonyesha ramani ya Kijiji ilipo.

Mhandisi Magesa ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi Kijijini hapo ambapo alielezwa kuwa tatizo lililopo linachangia migogoro ya ardhi.

"Kijiji cha Ndirigishi kinaongoza kwa migogoro ya ardhi Kiteto, kama Kiongozi wa Serikali siko tayari kuendelea kuona hali hii"

Ili kukabiliana na migogoro hii kuna kila sababu ya kuifahamu mipaka ya Kijiji..kwa sasa hatuwezi kuitatua bila wananchi kuonyeshwa mipaka alisema.

Wakizungunza mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya wananchi hao walisema pamoja na mambo mengine Serikali ya Kijiji imechangia kwa kiwango kikubwa matatizo hayo

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ametishia kuivunja Serikali hiyo ya Kijiji kwa kuonyesha madhaifu katika kuihudumia jamii.
IMG_20180903_144144.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom