Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni atoa amri ya kuzuia magari yasipaki Mwenge

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ametoa amri inayokataza wakazi wa Mwenge stand kupaki magari yao na wenye maduka kushusha mizigo yao madukani. Huu ni ulevi mwingine wa madaraka uliovuka mipaka ya uvunjwaji wa katiba, sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu tulizojiwekea wenyewe.

Ukimuuliza swali mkuu wa wilaya, ni kwanini wanazuia magari ya wananchi kupaki na wafanyabiashara kushusha mizigo yao madukani anakujibu nani amekuleta mjini?

Hii ndio serekali ya viwanda na sera zake?

Madaraka ya kulevya
 
Hii ni moja kati ya amri mbaya iliyowai kutokea toka tanzania imepata uhuru,lkn kuna tetes za chini chini kuwa wanagombea masilaya pesa za magari,na pesa wanazookota hapa mwenge ambazo hazifiki halimashauri,zinaliwa,na wajanja wachache
 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ametoa amri inayokataza wakazi wa Mwenge stand kupaki magari yao na wenye maduka kushusha mizigo yao madukani. Huu ni ulevi mwingine wa madaraka uliovuka mipaka ya uvunjwaji wa katiba, sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu tulizojiwekea wenyewe.

Ukimuuliza swali mkuu wa wilaya, ni kwanini wanazuia magari ya wananchi kupaki na wafanyabiashara kushusha mizigo yao madukani anakujibu nani amekuleta mjini?

Hii ndio serekali ya viwanda na sera zake?

Madaraka ya kulevya

Kabla sijaanza ' kutiririka ' dhidi yake nakuomba Mleta mada utuwekee hapa sababu ambazo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amezisema juu ya uamuzi wake huo ili tusije tukawa tunachangia kitu hapa kumbe ikawa ni Majungu yako tu au chuki zako tu dhidi yake. Usitutafutie dhambi za lazima kwa ' Maulana ' asubuhi yote hii tafadhali!
 
Sasa wasishushe mizigo yao madukani mwao, anataka wakashushe nyumbani kwake, mbona napata kizungu zungu
 
Kabla sijaanza ' kutiririka ' dhidi yake nakuomba Mleta mada utuwekee hapa sababu ambazo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amezisema juu ya uamuzi wake huo ili tusije tukawa tunachangia kitu hapa kumbe ikawa ni Majungu yako tu au chuki zako tu dhidi yake. Usitutafutie dhambi za lazima kwa ' Maulana ' asubuhi yote hii tafadhali!
Tulimuliza mkuu wa wilaya sababu za kukataza watu kupata,na magari yao?tukajibiwa,ni nani amewaleta mjini hilo ndio jibu tuliopewa
Kumbunga nyumba za mwenge zina hati,na maamuzi yalifikiwa kulikuwa hamna kikao chochote kilichokaa kati ya wananchi na mkuu wa wilaya,ni amri
 
Lini hayo yametokea?
Alikuja hapo Mwenge?
Magari hayo watu wanapaki masaa yote hata wakiwa madukani?
Picha ulimpiga au kumrekodi?
Sababu za yeye kuzuia amesema ni nini?

Naona haujaelezea kueleweka labda uongeze ndondo zaidi, ni kama umeamua tu kuandika ilivyo kwa sasa.
 
Tulimuliza mkuu wa wilaya sababu za kukataza watu kupata,na magari yao?tukajibiwa,ni nani amewaleta mjini hilo ndio jibu tuliopewa
Kumbunga nyumba za mwenge zina hati,na maamuzi yalifikiwa kulikuwa hamna kikao chochote kilichokaa kati ya wananchi na mkuu wa wilaya,ni amri
Nilishawahi kuandika hapa. Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar, Aache ushamba wake huko huko, Nina Imani, hata mtu aende shule kwa kiasi gani, Kama ni mshamba ni mshamba tu, Hili jiji halitakiwi kuongozwa na Mshamba.
 
Tulimuliza mkuu wa wilaya sababu za kukataza watu kupata,na magari yao?tukajibiwa,ni nani amekuleta mjini hilo ndio jibu tuliopewa
Kumbunga mwenge nyumba za mwenge zinachekesha hati,na kulikuwa hamna kikao chochote kilichokaa kati ya wananchi na mkuu wa wilaya,ni amri

Kwa ninavyomjua Hapi hasa Kiutendaji na Kiueledi nachelea kukubaliana na haya majibu yako ila ninachokiona tu ni chuki zako dhidi yake au umetanguliza uanaharakati wako wa Kisiasa juu ya hili jambo. Labda nikusaidie tu Mkuu ni kwamba Mkuu wa Wilaya hawezi kufanya jambo kwa ' kukurupuka ' tu pasipo utaratibu fulani kutangulia na ninaamini kuwa inawezekana wakazi wenzio wa Mwenge walishafahamishwa na kutahadhalishwa kitambo tu juu ya hili lililotokea leo. Tupunguze majungu, malalamiko na uanaharakati na tutambue pia kuwa hakuna haki bila wajibu.
 
Njoo uwasaidie wafanyabiashara wa mwenge waweze kushusha mizigo yao,na wakazi mwenge waende nyumbani kwao wakiwa huru kwenye nchi yao,ww unakataa uhalisia?
 
Nina Washikaji zangu hapo Buchani jirani kabisa na hiyo Benki hapo wanadai kuwa hawataki Unafiki na kwamba hayo yanayotokea leo hapo walishatahadharishwa takribani miezi mitatu iliyopita huku kuna wengine walipewa ushauri wa bure tu wa nini cha kufanya ili kuepukana na hiyo adha na kuendelea kufanya biashara zao vizuri tu lakini kama kawaida yetu Watanzania tunapenda mno kupuuza mambo, kuchukulia poa, kuishi kwa mazoea na jambo la Kisheria likitokea tu tunaanza kulalamika na kuingiza ' uanaharakati ' wetu. Kwa hizi hoja ' dhaifu ' kabisa ninazoziona hapa bado sijaona Kosa la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi bali naona tu kuwa anatekeleza wajibu wake vizuri mno na pengine nampa Kongole ( pongezi ) zangu na mpeni tu ushirikiano ili ' awafurumusheni ' vizuri hapo siku zingine muwe na adabu na mjue kufuata utaratibu.
 
Back
Top Bottom