Mkuu wa wilaya ya Kalambo aamuru kukamatwa kwa mganga wa zahanati ya Ilango kwa ubadhirifu wa fedha

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Bi Julieth Binyura, ameagiza kusakwa na kukamatwa mara moja mganga mfawidhi wa zahanati ya Ilango katika kata ya Kilesha, anayetuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 24, za ujenzi wa nyumba ya mganga kwenye zahanati hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kalambo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Bi. Julieth Binyura, ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akiongea na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo, kwenye kikao ambacho kimebariki kutimuliwa kazi kwa maafisa watendaji wa vijiji kumi na nne, kwa makosa ya ubadhirifu na utoro kazini, amesema kuna umuhimu wa mganga huyo kupatikana ili wajulikane wote waliohusika na ubadhirifu huo.

Baadhi ya madiwani wakiongea kwenye kikao hicho, wamekitupia lawama kitengo cha manunuzi kwa kufanya kazi bila ya uadilifu, ikiwa ni pamoja na idara ya ujenzi, hali inayoisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo, na kuchangia kufanya miradi mingi kuchelewa kukamilika kwa wakati.

Chanzo: ITV
 
Mganga anahusikaje na fedha?
Pmu na mhandisi kazi yao nini hapo.
 
Yule DMO wa Singida nae apelekewe Special Audit na PCCB kukagua Miradi ya Maendeleo asije akawa kakimbia na Mafungu ya Wavuja jasho Na Walalahoi.
Mtu akishindwa kuendana na kasi ya Mh.Rais achunguzwe
 
Utumishi wa umma imekua kazi ya kijambazi siku hizi, muda wowote unatafutwa na polisi
 
Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Bi Julieth Binyura, ameagiza kusakwa na kukamatwa mara moja mganga mfawidhi wa zahanati ya Ilango katika kata ya Kilesha, anayetuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 24, za ujenzi wa nyumba ya mganga kwenye zahanati hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kalambo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Bi. Julieth Binyura, ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akiongea na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo, kwenye kikao ambacho kimebariki kutimuliwa kazi kwa maafisa watendaji wa vijiji kumi na nne, kwa makosa ya ubadhirifu na utoro kazini, amesema kuna umuhimu wa mganga huyo kupatikana ili wajulikane wote waliohusika na ubadhirifu huo.

Baadhi ya madiwani wakiongea kwenye kikao hicho, wamekitupia lawama kitengo cha manunuzi kwa kufanya kazi bila ya uadilifu, ikiwa ni pamoja na idara ya ujenzi, hali inayoisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo, na kuchangia kufanya miradi mingi kuchelewa kukamilika kwa wakati.

Chanzo: ITV

Kama wanadiriki kufanya ubadhilifu katika zama hizi za tumbuatumbua, what about before?
 
Huyo mganga kulifanyika trainning ya finance pamoja na procurement? Cheti chake mbona hakiusiani na mambo ya ujenzi hahaha
 
Back
Top Bottom