Mkuu wa Wilaya ya Iringa, R. Kasesela,akumbuka kifo mamake akiwa miaka 11, mazishi ya Mnyarwanda

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575

Mkuu wa wilaya Iringa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ameshiriki kwenye mazishi ya Mnywarwanda Jeannnete Mukashema aliyefariki kwenye ajali iliyotokea usiku Juzi. Bi Jeanette alikuwa akisafiri na mtoto wake ( pichani juu akiwa na mkuu wa wilaya ) ambaye naye aliumia kwenye ajali hiyo na bado anaendelea na matibabu.
Akizungumza katika mazishi hayo, Mh Kasesela alisema, " Imeniuma sana kwani niliupokea mwili kwa mikono yangu tukiwa na waokoaji wengine alipo tolewa juu kwenye basi, ni wazi bado tukio hilo limo mawazoni mwangu na nguo zangu zikiwa na madoa ya damu , tulimpokea akiwa tayari amefariki.


Mkuu huyo wa wilaya ya Iringa aliendelea kusema kuwa, " Kesho yake mtoto alipozinduka akaanza kumtafuta mama yake, nilipomtembelea asubuhi, nilijua mama yake amefariki dunia nilishindwa kumwambia leo alipo niona ameanza kulia amenikumbusha nikiwa miaka 11 nilipo ondokewa na mama yangu. lakini naamini yuko katika mikono salama, Mungu ni mwema baba yake na ndugu wengine wamekuja kutoka Rwanda, alisema Kasesela.
 
Jamaa kwa Promo! JK mtafutie kikundi cha sanaa anaonekana anaweza sana maigizo huyu hazina kwa taifa kwenye sanaa! Sio utendaji!
 
Ni muda muafaka tuelezwe yapi hasa majukumu ya mkuu wa Wilaya ya kila siku, maana naona sasa Sanaa zinazidi.
 
Kwa hiyo mkuu maana yake nini kabla kitambo kwenye kikapu hujawa mkuu picha za matukio kama hayo basi
 
Jamaa kwa Promo! JK mtafutie kikundi cha sanaa anaonekana anaweza sana maigizo huyu hazina kwa taifa kwenye sanaa! Sio utendaji!
Huyu anafaa sana manake ni Burudani...Ningefurahi kumuona akiwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni....(Michezo iende Wizara ya Elimu)
 
NA yeye ni mnyarwanda au alikuwa anawapeleka wapi? Uhamiaji wawe makini na viongozi wa siku hizi
 
Hivi admin wana weza kutumbia wiki hii jina la Kasesela limetwaja mara ngapi humu JF. Maana ake hata Mtanzania wamemrusha.
 
Hajapiga selfie akiwa amejipaka damu? katika hilo zoezi la uokoaji?

BTW huyo mtoto anasikitisha sana, kuondokewa na mzazi ghafla inauma sana!
 
Ha ha ha ha ha ha ha haaaaaa! Yaani nimekua nikichukia sana mienendo ya Huyu Jamaa Ila Sasa nimejikuta nacheka tu! Pole Kwa wafiwa wote!
 
Akizungumza katika mazishi hayo, Mh Kasesela alisema, " Imeniuma sana kwani niliupokea mwili kwa mikono yangu tukiwa na waokoaji wengine alipo tolewa juu kwenye basi, ni wazi bado tukio hilo limo mawazoni mwangu na nguo zangu zikiwa na madoa ya damu ,
Haya maneno hayajaandikwa au kuzungumzwa kwa bahati mbaya, anajua anachomaanisha na kukilenga... hahahaha attention seekers, unageuza msiba wa mtu kujipatia promo??
 
Na wale waliokuwa wanagombea maiti mochwari ya Mwanza mbona hamkuwasakama kuwa wanataka media coverage?
 
Huyu anafaa sana manake ni Burudani...Ningefurahi kumuona akiwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni....(Michezo iende Wizara ya Elimu)
huyu nafikiri alitokea kwenye basketball kujipendekeza kwake kwa jk ndio akapata ukuu wa wilaya ila akiachwa sijui atasema nini
 
Back
Top Bottom