Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kasesela awasihi Wananchi kukaa mbali na watu wanaotoka Dar. Mwenyewe afafanua

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Salaam,

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, amewataka wananchi wake kukaa mbali na watu wanaotoka Dar Es Salaam ili kujikinga na maambukizi ya Corona.

Japo inaonekana kama ubaguzi, lakini ndo ukweli wenyewe kwamba watu wanatakiwa wawe makini na Ugonjwa wa COVID-19.

"Sitaki kupoteza sura hata moja. Na tutaendelea kuwamonitor wale wanaotoka Dar Es Salaam, wanapoingia tupeni taarifa. Sasa hivi sio wanaotoka nje ya Nchi, anayetoka Dar Es Salaam usikae naye karibu... anayetoka Dar usikae naye karibu. Hakikisha unatupa taarifa tunaweza kumumonitor, tutakwepa hili tatizo". Amesema Richard Kasesela.

Zaidi soma: Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga - JamiiForums



DC KASESELA AFAFANUA KAULI YAKE YA WANAOTOKA DAR KUTENGWA

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema alinukuliwa vibaya, kwani alikuwa kwenye msiba na kauli yake kuwa Watu wanaotoka Dar waangaliwe, wapimwe na watu wa Iringa wakae mbali na watu wa Dar ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya msiba huo

Amesema, kulikuwa na msiba na yalienda mabasi mawili yakiwa yamebeba watu waliojazana, na kwenye msiba huo akafariki mtu mwingi hivyo familia ikawa imepoteza watu wawili, na kutokana na hilo wakaamua kuchukua hatua za kujiangalia zaidi

Katika kuchukua hatua hizo, ndio aliagiza kwa nia njema kabisa kuwa watu wa Iringa wasikae karibu na watu wanaotoka Dar na kuwa nao makini kwasababu Watu hao walikuwa hawajapimwa kwa wakati

Aidha, ameongeza kuwa hakumaanisha kuwazuia Watanzania kwenda Iringa au kuwatenga watu wanaotoka Dar. Amewaomba wale ambao hawakuelewa tangazo waelewe kuwa lilikuwa ni kwaajili ya pale msibani tu

Pia, ameongeza kuwa kauli yake ya kwamba usikae karibu na Mtu aliyetoka Dar, alikuwa akimaanisha kwenye msiba huo kwasababu walikuwa bado hawana uhakika na watu wa Dar (kiafya)
 
Sasa Kama tumeanza kunyanyapariwa hapa hapa Dar huko Kwa majirani zetu, Kenya, Uganda na Rwanda hapo baadae itakuwaje? Maaana wenzetu Nina Uhakika had mwezi wa sita mwanzoni watakuwa wamedhibiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Kama tumeanza kunyanyapariwa hapa hapa dar huko Kwa majirani zetu, Kenya, Uganda na Rwanda hapo baadae itakuwaje? Maaana wenzetu Nina Uhakika had mwezi wa sita mwanzoni watakuwa wamedhibithi.

Ni kawaida mtoto ‘mweupe’ kuamini kwa jirani wanaishi vizuri kuliko kwao, ndiyo maana wengi wao hufurahia zaidi chakula kwa jirani bila kujali ni msosi gani.

Hebu tuambie, nini kinakupa uhakika huo..?
 
Back
Top Bottom