Mkuu wa wilaya ya Ilema, hujifunzi tu kupitia kwa Sabaya?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Habarini wadau,

Serikali ya awamu ya tano pamoja na serikali ya awamu ya sita imekuwa ikisisitiza sana kwenye viwanda, kuongeza ajira pamoja na kusisitiza sana watu kujituma kufanya kazi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.

Lakini kwa research yangu ndogo biashara nyingi ambazo zimeonesha mafanikio zimekuwa zikipata vikwazo vikubwa kutoka kwa watu wa serikalini hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Afadhari kidogo wakuu wa mikoa lakini wakuu wa wilaya wamekuwa wakizidi sanaaa kuleta vikwazo kwa wafanya biashara katika wilaya mbalimbali, na hii hutokana na husda na wivu walio nao wakuu wa wilaya. Labda hawaelewi wajibu wao lakini wamekuwa wakiingiza nchi katika hasara mbali mbali zinazo onekana na zisizo onekana kama kupunguza mapato ya kodi kwa tra kufuatia kufunga biashara mbalimbali.

Nimeona mara kadhaa mkuu wa wilaya ya ilemela-mwanza akimsumbua mmiliki wa the cask bar & grill pale mwanza rock-city mall. Amekuwa akichukua mambo yake binafsi na kuyaleta kwenye biashara kumsababishia mmiliki huyo hasara zisizo na msingi, lakini amekuwa anafanya ajira za wale vijana wanaohudumu pale kuwa za mashakani kwasababu ya chuki zake binafsi.

Kuna siku nimewahi kutana na mmiliki wa the cask bar & grill kituo kikuu cha polisi-mwanza akiwa amewekwa ndani kwa masaa 48 kwa amri ya mkuu wa wilaya ya ilemela kwa kile alichodai kuwa anapiga mziki wenye sauti kubwa na kuwafanya wananchi wa maeneo ya karibu kuto kulala. Kwangu hii niliona sababu ni dhaifu sanaaa. Kwa sababu mazingira ambapo the cask na rock city mall yalipo sidhani kama yanaweza kusababisha kelele kwa watu wa karibu kiasi cha kushindwa kulala.

Hii tabia mkuu wa wilaya ya ilemela amekuwa aliendelea nayo kwa muda mrefu sana na kumsababishia jamaa kushindwa kufanya biashara yake kwa uhuru.

Jana tarehe 15/05/2021, the cask bar and grill walikuwa wameandaa tamasha la kumleta msanii kutoka south africa- focalistic na walipata vibari vyote, cha kushangaza ilipo fika saa 12 jioni kuelekea saa moja jioni kwa amri ya mkuu wa wilaya kuna vijana walikamatwa pale the cask kwa sababu ya kuwa wanapiga mziki na kuwasumbua watu, lakini pia msanii ilisemekana asiperform kwa kigezo kuwa maeneo yale mziki hauruhusiwi. Hii sababu ilikuwa ni dhaifu sana kutoka kwa mkuu wa wilaya kwasababu kupitia tamasha lile, tra wangeingiza kodi sio chini ya 2,000,000/=, boda boda wangefanya biashara, tax zingifanya biashara lakini hasara aliyoipata mmiliki ni kubwa kiasi gani? Tusishangae the cask bar & grill ikafungwa kwa hasara ambayo jana ilitengeneza kisa tuu mkuu wa wilaya.

Binafsi nimekuwa siridhishwi na namna ambavyo mkuu wa wilaya ya ilemela anaiongoza hii wilaya. Huo ni mfano mmoja lakini ipo mingi zaidi.

Swali langu ni je, hawa wakuu wa wilaya hawajifunzi kupitia wenzao wanaotumbuliwa kila siku? Wanasahahu kuwa haya madaraka ni ya kupita? Mnao husika na hizo mamlaka angalieni kwa jicho la tatu. Tanzania wanaofanya biashara za bar pamoja na entertainment wamekuwa hawana amani na biashara zao kwa kigezo cha muda na muziki. Kama haya kweli yanatoka serikalini basi ni bora wangepitisha sheria inayowataka wanao anzisha biashara za bar kufungua hata km 30 kutoka yalipo makazi ya watu na sio kuwasumbua wafanya biashara hawa. Lakini bar zimekuwa zikichangia pato kubwa sana serikalini pamoja na usumbufu kama huu.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela jitafakari.
 
Mhe. Chalamila ukifika Mwanza fanyia kazi suala la The Cask Bar & Grill iwapo RC anayeondoka atakuwa hajalifanyia kazi ili kuokoa ajira za hao wafanyakazi sababu hiyo Bar imefungwa.

Apishe uchunguzi naye.
 
Anaitwa nani huyo ? Tumtengenezee story sasa hivi mwenzake anatoa maelezo TAKUKURU huko
 
Back
Top Bottom