Mkuu wa Wilaya ya Hai na RPC Kilimanjaro wachunguzwe kwa matukio ya Kisiasa

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Alichokifanya Ole Sabaya Mkuu wa WIlaya ya Hai ni kumdhibiti OCD ndio maana Kwa sasa ukiona anayoyafanya OCD wa Hai, Mkuu wa WIlaya, Ole Sabaya yuko nyuma yake. Huyu OCD anahojiwa na Tume kuhusiana na tukio la kujibu masuala ya Uchaguzi, isitoshe kuna suala la kumrushia mawe Mgombea Urais kupitia chama cha CHADEMA OCD alikuwepo katika eneo husika. Huyu OCD alihojiwa na kuonywa asirudie tena ila yalijirudia juzi kumjibu mgombea ubunge wa Hai kupitia CHADEMA.

Huyu DC achunguzwe na RPC kuhusiana na haya, kuna matukio ambayo watu walikamatwa, walimtaja DC Ole Sabaya kwa ujira huo baadae waliachiwa kwakuwa kuna ushirikiano wa wote wawili, hadi sasa hawakufikishwa mahakamani wako mtaani wanaonekana wakitembea vifua mbele.

Je, anacho kifanya DC ametumwa na viongozi wa juu? kwa sababu ilisikika wajumbe na watendaji wakuu wa serikali wakimsifia sana akiwemo Waziri Mkuu kwa kile anacho kifanya Wilaya ya Hai si maendeleo tu ni pamoja na kuuvuruga mfuko wa jimbo kama vile wao ndio walimtuma bila kunshirikisha mgombea Ubunge, mkutano huo wa kumsifu ulifanyika miezi 2 iliyopita pale kwa Sadala wakati wa kampeni ya mgombea ubunge na madiwani.

Je kinachoendelea sio ki afya kwa watanzania waishio Wilaya ya Hai, Wilaya ya Hai imekuwa na Matukio ya kuwavamia na kuwaumiza ikiwemo kuwasulubu wapinzani zaidi ya Wilaya nyingine

Swali ni moja tu Je, Waziri wa Tamisemi na Waziri Mkuu wana mkono wao hapo kwa Sabaya kama hawana basi wajitokeze kumkemea, wananchi tusikie maana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ni kama hana maelewano na DC wa Hai, DC Alizuia Mkutano wa CHADEMA kwa kuweka vikao viwanja vyote vya mikutano ya kufanyia kampeni, hajakemewa isipokuwa mKuu wa Mkoa alikuja na kuwahoji waliokuwepo na kujikuta hawaelewi kinachoendelea aliishia kuwakemea na kuwaambia yasijirudie tena.

Tunaomba Waziri wa Tamisemi, Waziri Mkuu, tunasema kuwa Tanzania ni ya Watanzania wote sio ya Wachache, wamchunguze na matukio haya kuendelea ni kuichafua nchi.

MUNGU IPONYE TANZANIA
 
Hakujifunza kwa yaliyowapata manguli wa fitina na roho mbaya yaani makonda, musiba na Gambo Basi mwisho wake ni mbaya kuliko na hataamini Kama mfumo umemtupa jalalani! Aitafute clip ya ufunguzi wa kampeni za ccm dodoma aitazame jinsi makonda alivyokondeshwa juani na vijana Kama ana akili atajirudi na kutulia!
 
Kwani ocd atapiga kura ngapi? Ni wakala wa kuhesabu kura? Nyie fanyeni siasa acheni visingizio
 
Huyo Mkuu wa Wilaya aliwekwa kimkakati Chama twawala kilijua kuwa upinzani mkali utatokea hapo Hai ila hawakujiandaa na Tsunami hii TAL🤣🤣🤣🤣
 
Huyo ole sabaya kama wanampenda wamtumbue wasipompindua,sisi tutamshughulikia kwa sayansi za kiroho zaidi
 
Sabaya ni kipenzi cha wanakilimanjaro, huyo Mbowe hawataki hata kumuona
Sabaya ana bahati sana kwamba watu wa K'Njaro wamestaarabika sana, ingekuwa ni enzi zile za ushenzi watu wangemzika mzima mzima.
 
Back
Top Bottom