Mkuu wa Wilaya ya Hai akanusha kumweka mahabusu Mwalimu kwa kushindwa kutaja jina lake

Mkuu wa wilaya ya Hai Mh Erasius Byakanwa ametaa madai kuwa alimweka ndani Mwl Erasto Mhagama kwa saa sita kwasababu ya Mwalimu huyo kushindwa kutaja jina la Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu wa Wilaya amesema yeye kama kiongozi mwenye akili timamu na akiamini mamlaka ya uteuzi inamwamini hawezi kumuweka mtu ndani kwa kushindwa kutaja jina lake na anafikiri akifanya hivyo basi atakuwa amepungukiwa Kitu cha msingi sana.

Lakini yeye kama kiongozi anazingatia utawala wa sheria na taratibu na pia kama kiongozi pale ambapo inonekana panalazisha kuchukua hatua anachukua hatua na taarifa ataitoa kwa ujumla kama alivyosema kupitia azam TV.

Mwalimu huyo aliwekwa ndani kituo cha Polisi Bomang'ombe kutoka saa 8:30 mchana mpaka saa 2:30 usiku.
Huku ndio kukanusha? Mbona hasemi huyo mwalimu aliwekwa ndani kwa kosa gani!
 
Wateule wa asa hiv hasa hawa MADC ni migodi inayotembea...

Yaani utajiri nje nje kwa maamuzi yao haya ya kukurupuka
 
Mimi mwenyewe nilipoiona ile Habari siku ya jana nilishangaa sana!

Hasa pale kwenye kutofautisha CUF chama cha Siasa na CAF shirikisho la Mpira wa Miguu

Unamuaminije aliyetenda kosa,ulitegemee aseme ndiyo??Hivi wale walimu wote waseme kwamba DC aliwauliza maswali hayo na aliyeshindwa aliambiwa apige push up ni waongo??

Kwa DC kama huyo wa HAI lazima angekataa hakuna mtu anayetegemea akubali upuuzi aliofanya.Labda alifikiria kwamba baada ya kumweka lock up hatasema.

Poleni mnayemuamini mpuuzi kama huyo DC wa Hai
 
Madaraka mengine yana % kubwa sana ya alcohol.
Imemkuta jamaa mmoja na jina lake lina kiambisho cha alcohol!
Amelewaje!!?

Jogi !
Kuwa mwangalifu uilitaje bure jina la Bwana Mungu kwa dhihaka! Pombe sio chai hata watoto wa chekechea wanajua kwamba haiuzwi kwa watu wenye umri chini ya miaka 18. Watanzania kwa makusudi na kwa kuvunja sheria halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar wakachagua pombe yanayowakuta ni haki yao. Mara zote pombe humtoa mtu ufahamu na mwisho wake ni fedheha na hata kifo. Sioni sababu ya kupoteza muda hapa ni kazi tu ! Unapokuwa kiongozi wa ngazi yoyote ni lazima ukubali kuwa jalala. Kama huwa kifua unatakiwa ujiuuzulu asubuhi kwani yatakushinda. Kuwa kiongozi hazina maana unajua kila kitu. Hata Yesu alidhihakiwa na yeye alikuwa Mwana wa Mungu!
 
sijaona utetezi wake kuhusu zile meseji alizokuwa anamtumia yule mwanamke wa kike.... DC anaendekeza NGONO kazini.. hafai kuwa kiongoz...
Ni mwalimu wa kike, maana wanawake wote ni wa kike. Ila alifanya hivyo baada ya kuwatisha waalim ili apate kukubaliwa kimapenzi na huu ni ubakaji.
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Mh Erasius Byakanwa ametaa madai kuwa alimweka ndani Mwl Erasto Mhagama kwa saa sita kwasababu ya Mwalimu huyo kushindwa kutaja jina la Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu wa Wilaya amesema yeye kama kiongozi mwenye akili timamu na akiamini mamlaka ya uteuzi inamwamini hawezi kumuweka mtu ndani kwa kushindwa kutaja jina lake na anafikiri akifanya hivyo basi atakuwa amepungukiwa Kitu cha msingi sana.

Lakini yeye kama kiongozi anazingatia utawala wa sheria na taratibu na pia kama kiongozi pale ambapo inonekana panalazisha kuchukua hatua anachukua hatua na taarifa ataitoa kwa ujumla kama alivyosema kupitia azam TV.

Mwalimu huyo aliwekwa ndani kituo cha Polisi Bomang'ombe kutoka saa 8:30 mchana mpaka saa 2:30 usiku.
Na hasemi kamuweka ndani kwa sababu gani. Anajitetea tu kuwa anajua sheria na bla bla nyingi.
 
Kwanini hajatoa taarifa mapema ni kujipanga na kupitisha bahasha kwanza au?
Nimeboreka kusoma halafu hakuna sababu iliyompelekesha kufanya hayo...

Asante sana naona ufahamu umekurudi....

Kwenye makosa kama haya lazima tusimamie ukweli bila kujali itikadi zetu....
 
Back
Top Bottom